Jina la Werema nalo lipelekwe kwa OCAMPO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jina la Werema nalo lipelekwe kwa OCAMPO

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by jambo1, Dec 28, 2010.

 1. jambo1

  jambo1 JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2010
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwenye Orodha ya watu ambao moja kwa moja watakuwa wamechangia vurugu hata mauaji ya wananchi wakidai katiba mpya ni Fredrick Werema..Kwani kwa Maoni yake haoni kuwa Taifa linahitaji katiba Mpya..anataka ileile ya CCM ya Mwaka 77 iendelee kujaziwa vilaka..!majina mengine ambayo yapo kwenye orodha hadi sasa ni Celina Kombani, Lewis Makame na John Tendwa...Tusubiri Tutapata wengi zaidi tuendako..!
   
 2. D

  DENYO JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ocampo atawashugulikia werema, celina, na mwinyi 2015 angalau hao wamejotokeza na kukiri kwamba ni bora vurugu kuliko kubadili katiba -sasa tuweke haya mambo kwenye records mapema ili ikitokea wajulikane chanzo cha mtikisiko. Werema ni mwanasheria wa kikundi cha wtz wachache na anatetea maslahi ya wachache. Tatizo lake nini kuandika katiba upya?
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 416,698
  Trophy Points: 280
  Werema: Katiba mpya ya nini?

  Imeandikwa na Waandishi Wetu; Tarehe: 27th December 2010 @ 23:59


  MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amesema suala la madai ya Katiba mpya, linapaswa kuwa mikononi mwa wananchi, huku binafsi akisema haoni haja ya Katiba mpya kwa sasa.

  Jaji Werema aliyasema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu suala hilo katika Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam mara baada ya kuapishwa kwa Jaji Mkuu mpya, Chande Othman.

  Jaji Othman aliteuliwa juzi na Rais Jakaya Kikwete kuwa Jaji Mkuu baada ya aliyekuwa Jaji Mkuu, Augustino Ramadhani kustaafu kwa mujibu wa sheria jana.

  Akifafanua kuhusu Katiba hiyo ya mwaka 1977, Jaji Werema alisema, "Tunapaswa kujiuliza Watanzania wanahitaji nini? Mimi binafsi ukiweka wadhifa wangu kando, bado sioni haja ya Katiba mpya, lakini kama ni Watanzania wanataka mpya sawa, wakitaka marekebisho pia sawa."

  Alisema serikali ipo tayari kufanya kile Watanzania wanachokitaka bila wasiwasi kwa kuwa ipo kwa ajili yao, lakini si kufanya matakwa ya mtu fulani na kuongeza kuwa hoja zinapaswa
  kuletwa mezani na kuzungumzwa kwa pamoja.

  Jaji Werema ambaye pia alitumia muda huo kumsifu Jaji Mkuu mpya, Othman kuwa ni mwadilifu, mwerevu na mwenye kujua sheria ipasavyo, alisema Katiba ni sheria mama na inapaswa kuwa na maslahi ya Watanzania.

  "Kila mtu anazungumza kama bata, watu wanazungumza kibatabata, lazima tujiulize Watanzania wanataka nini? Wakati fulani iliwekwa vifungu vya haki za binadamu kuanzia kifungu cha 12 hadi 29 kwa kuwa vilihitajika, tuzungumze si kutishana," alisisitiza Jaji Werema huku akitolea mfano Katiba ya India ya mwaka 1948 iliyofanyiwa marekebisho mara 50.

  Alipoulizwa kutoa maoni yake kuhusu baadhi ya vyama vya siasa ‘kushikia bango' suala hilo, Jaji Werema alisema vyama hivyo vina haki na vipo sahihi kufanya hivyo,

  lakini si kila kitu kilicho sahihi ni sawa au kinafaa kwa wakati husika, hivyo kilicho cha muhimu ni wananchi kuulizwa wanataka nini.

  Alitumia pia fursa hiyo kuwatahadharisha waandishi wa habari kuacha uchochezi na kuandika kwa ushabiki binafsi, badala yake kuweka maslahi ya taifa mbele.

  "Waandishi nanyi muache ushabiki, msije kuipeleka nchi hii kuwa kama Ivory Coast, mtumie muda mwingi kueleza hali halisi na nini maana ya kuwa na Katiba mpya au kufanya mabadiliko," alisema Jaji Werema.

  Tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu Oktoba 31 mwaka huu, vyama vya upinzani viliibua hoja ya Katiba mpya, suala ambalo sasa kila anayepata jukwaa la kuzungumza, analigusia.

  Serikali kupitia viongozi wake akiwemo Waziri Mkuu Mizengo Pinda, wamekaririwa wakisema serikali haina kigugumizi katika suala hilo, lakini ni vyema likafuata taratibu, badala ya shinikizo la mtu kwa maslahi binafsi.

  Katika hatua nyingine, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, jana alikabidhi taarifa ya Hoja Binafsi inayolitaka Bunge kuwa chombo kinachoanzisha na kusimamia mchakato wa kura za maoni ya wananchi kuhusu Katiba mpya badala ya Tume za Rais, kwa Mkurugenzi wa Idara ya Taarifa Rasmi za Bunge, Eliakim Mrema anayekaimu nafasi ya Katibu wa Bunge, jana asubuhi kwenye ofisi ndogo Dar es Salaam.

  Mnyika alisema ataitumia wiki ya kwanza ya mwezi ujao kutangaza rasimu ya hoja hiyo ili wananchi waisome na kutoa michango atakayoijumuisha kuipa uzito unaostahili na wenye kubeba mawazo ya wananchi.

  Aidha, Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imezuia maandamano ya kuwasilisha mapendekezo ya rasimu ya Katiba mpya yaliyokuwa yafanywe leo na Chama cha Wananchi (CUF).

  Kamanda wa Kanda hiyo, Suleiman Kova, alisema maandamano hayo yamezuiwa kwa sababu wakati CUF ikitoa taarifa ya uwasilishaji wa rasimu hiyo kwenda Wizarani kupitia njia ya maandamano, taarifa waliyoituma kwa Wizara hiyo haikutaarifu kuwa wangepeleka mapendekezo hayo kwa njia hiyo badala yake waliitaarifu kuwa watapeleka mapendekezo hayo, suala alilosema lina tofauti ya maana.

  Alisema lengo la Polisi si kuzuia maandamano hayo na mengine ya namna yoyote ilimradi kama yatazingatia sheria na taratibu za kiusalama huku akisisitiza kuwa kwa upande wa CUF, suala hilo halikuzingatiwa.  Jumla Maoni (3) Maoni Uongozi ni dhamana, unayopewa na wananchi. Nina maana kwamba kiongozi ni mtumwa kwa wananchi. Sioni kama kuna sababu zozote za kuwa kinyume na matakwa ya wananchi. Kwa upande mwingine mh. Yuko sawa ukizingatia ni wananchi wangapi wanaoijua katiba. Kwa maoni yangu. Katiba ishugulikiwe kwa namna yoyote iwe ni kubadilisha au kurekebishwa. Ila tu selikali ijue ni wananchi wangapi wanataka 1 au 2 Maoni Mheshimiwa Jaji na Mwanasheria Mkuu.
  Kwa heshima na taadhima naomba nikueleze kwamba mimi ni Mtanzania, mwannchi wa kawaida kabisa, sijasomea sheria, na wala katiba inayosemwa inahitaji kubadilishwa sijawahi kuiona (kwa sababu hata kwenye maduka ya vitabu haipo). Lakini nimesikia wasomi wa sheria wakitaja baadhi ya vifungu vya katiba ambavyo vinanishangaza.

  1. Nimesikia kwamba kuna vifungu katika katiba yetu vinavyosema:-

  a) Tanzania ni nchi ya ujamaa na kujitegemea. Kama ni kweli katiba ina kifungu kama hicho, basi haifai kabisa kwa sababu Tanzania ya sasa ni ya ubepari (uwekezaji wa binafsi)- kitu ambacho ni kinyume na katiba ilyopo.

  b) Matokeo ya uchaguzi wa rais yakeshatangazwa hayawezi kupingwa mahali popote. Je, kama ikitokea akitangazwa mshindi mtu ambaye hakushinda, halafu mpinzani wake akawa na matokeo yanayoonyesha ameshinda, hali si inaweza kuwa kama Ivory Coast?

  c) Mtanzania yeyote hawezi kugombea uongozi wa kisiasa bila kupitia chama fulani. Je, kama naona vyama vyote vilivyoko havinifai, lakini nataka (na naona nafaa) kuwa kiongozi, kwa nini ninyimwe haki yangu?

  2. Mapendekezo ya marekebisho ya katiba yameshafanywa mara kadhaa miaka ya nyuma lakini vifungu vya sheria husika havikubadilishwa. Sasa mehshimiwa mwanasheria mkuu, kama huoni haja ya katiba mpya Watanzania watakuelewa kweli?

  3. Kama mabadiliko ya katiba yatakuwa yanafanywa na kundi dogo tu la watu walio serikalini, au wabunge peke yao, wanaweza kweli kuweka vifungu vinayvyopunguza maslahi yao? HAIWEZEKANI. Tunakuomba, mheshimiwa mwanasheria mkuu, uone umuhimu wa kuundwa katiba mpya kabisa. Nadhani maoni ya viongozi wa serikali yangepaswa kuwa ni kuhusu kwamba hiyo rasimu ya katiba impya iweje sio tena swali la kuwa na katiba mpya au la.

  Kama sisi wananchi tunawachagua wabunge watusaidie kutunga sheria kuna kosa gani tukiamua kutunga sheria mama (yaani katiba) sisi wenyewe?
  Maoni Katiba mpya au marekebisho makubwa ya katiba yamechelewa sana. Nchi yetu kwa hiari kabisa ilikubali kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi tangu mwaka 1992 lakini katiba haikubadilishwa. Kuna mambo muhimu sana kama vile kuundwa upya Tume ya Uchaguzi ambayo hayahitaji kusubiri hata siku moja zaidi kwa maslahi, umoja na usalama katika taifa letu na nchi yetu ambayo ni kitovu cha amani.
  Pamoja na hayo kuna kitu cha kuangalia sana na kwa makini mno kama itaundwa katiba mpya, vinginevyo ni afadhali tuifanyie marekebisho yoyote yale yanayofaa katika katiba ilitoko hivi sasa. Baadhi ya nchi zinazoendelea wameunda Katiba Mpya, bila kutarajia uchafu ukaingia kwenye hizo Katiba bila kugundulika kwa urahisi. Mfano ni sheria ya ndoa. Watu kutoka nchi fulani iliyoendelea walitumia fedha nyingi sana kuhakikisha kwamba badala ya sheria ya ndoa kusomeka kwamba, "NDOA NI KATI YA WATU WAWILI MWANAMUME NA MWANAMKE WENYE UMRI WA MIAKA 18 AU ZAIDI"; Katiba ikasomeka kwamba, "NDOA NI KATI YA WATU WAWILI WENYE UMRI WA MIAKA 18 AU ZAIDI". Kwa kuacha kipengele "Mwanamume na Mwanamke" ina maana Katiba ya nchi husika inaruhusu watu wa jinsia moja kufunga ndoa na kupata baraka zote za taifa.
  Kwingine jambo kama hilo lilifanyika lakini kilichofanyika ni kwa dhehebu fulani kuingiza mambo yake yatawaliwe na Katiba ya nchi na kugharamiwa na fedha za walipa kodi wote kwa maslahi ya wachache.
  Kama tutaunda Katiba mpya tuangalie mambo kama haya kwani wenye kutaka yao yafanyike wanaweza kutumia mabilioni ya fedha ili yanayowapendeza yafanyike

  Shitaka lake kuu ni kujikomba kwa JK ili kulinda kitumbua chake huku kwa makusudi mazima anahatarisha cha raia wote wa Bongoland..............................makosa mengine nanyi myaendeleze kuyatambua......................
   
 4. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #4
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Jinsi mambo yanavyo zidi kwenda watatokea watu wengi tu wenye mawazo finyu kama werema,TANZANIA TUMEROGWA NA NANI?CELINA KOMBANI AMEROGWA NA NANI?inatia uchungu sana kwa watu kama hao kuongea pumbaaaaaaaa.
   
 5. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #5
  Dec 28, 2010
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  najickia kulia, sema 2 cna m2 wa kunbembeleza hpa karbu. Hv huyu mbaba zna mtosha kwel? Au ka2mwa na makamba jaman? Kwenye hyo list ongeza na M. Pinda.
   
 6. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #6
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Mawaziri wasiwe wabunge
   
 7. c

  chechekali Member

  #7
  Dec 28, 2010
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 33
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Huyu werema akiliyake inamtosha mwenyewe....na anawakilisha mawazo finyu ya baadhi ya viongozi tulionao. Yani huwe amini eti mwanasheria mkuu wa nchi ndie asie ona mapungufu ya katiba ya sasa. Ivi inahitaji degree ya sheria kujua kwamba madaraka aliyonayo raisi ni makubwa sana na yananyima uhuru wa kidemocrasia wa kuopngozwa na viongozi waliochaguliwa na wananchi.Au kwasababu uliteuliwa unaona rais akipunguziwa madara utakosa mlo. were were acha njaa ulichochuma kinakutosha. but ujiandae kwenda kwa OCAMPO
   
 8. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #8
  Dec 28, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Think in a detailed manner! Kila mtu Katiba Katiba! Hivi ni sehemu ipi ya Katiba iliyopo ambayo inaonekana haifai? Je Katiba mpya italeta nini tofauti na cha sasa? Hebu nielewesheni kwanza hili, isije ikawa watu wanataka cover ya Katiba ndiyo iwe mpya yaani utoe ile alama ya ngao.....else kuna wengine twafuata upepo tu hatujui hata kinachoongelewa!
   
 9. jambo1

  jambo1 JF-Expert Member

  #9
  Dec 28, 2010
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kaka na wewe Avanti jina lako tunaliweka kwenye orodha ya kwenda ICC once machafuko ya kudai katiba yakitokea....!
   
 10. W

  Wakwetu Senior Member

  #10
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 157
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nakuunga mkono. anatakiwa haraka jina litoke kwenye Ocampo list.
  Huyu bwana ni Fisadi sana. Kwa nini anangangania katiba ya 1977? tena mtu msomi wa sheria ambaye alipaswa kuwa mstari wa mbele kuona mapungufu makubwa yaliyo kwenye katiba. Anajikomba kwa JK ili ampe hata kaubalozi au kapost kengine baada ya kazi yake hiy kuisha.
  Ni upuuzi kusema nguo iwekwe viraka wakati inatakiwa mpya. hana maslahi yake anayoyalinda ila ni ya vigogo.
  Yatamkuta very soon.
   
 11. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #11
  Dec 29, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  avanti uko serious? Kanunue katiba usome,acha uvivu ukisubiri kutafuniwa!
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Dec 29, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Werema kapewa cheo hicho na Rais aliopo madarakani, kwa maana hiyo asiposhabikia na kumkingia kifua aliyemweka madarakani kibarua kitaota mbawa.
  Umeona jaji mkuu mtaafu kushabikia katiba mpya anaonekana msaliti.
   
Loading...