Jina la Said Nassor Bagaile ndiye Hamis Andrea Kigwangalla?

Nafikiri tuchukulie kwa mtazamo mwingine....kuwa aliamua ku-officilize ile 'alias' i.e. Said Nassoro Bogoile alias Hamis Kingwangala. Sasa cha msingi ni kuwa hiyo elimu aliyopata kupitia alias ni kweli au vyeti ni vya kufoji! Kama elimu yake through alias haina mashaka, sioni tatizo. Turudi kwenye utanzania wake kama una shaka hapo ndipo tuseme, lakini kama la sioni hoja.

By the way alias watu walitumia sana huku kwetu enzi hizo kujikomboa wakati wa vita, manake hata elimu ilikuwa vita. Angalia mfano hapo jirani UG akina Generali Salim Saleh et. al. almost wote walitumia alias katika kupokea taaluma zao. Tusisahau mapema hivyo kuwa huko tulipotoka kielimu alias zilitumika sana kutafuta elimu, tumpongeze badala ya kumbeza.
wewe sasa unahalalisha fraud... forging names kupata kitu hata kama ni elimu ni fraud, and it is a criminal offense... dogo anatakiwa ajisafishe au aende jela

but naamin atajisafisha tu
 
Umenichesha sana...! Tukubali kuwa 'alias' zipo na zina meaning in life. Then twende one step further kujua 'alias' ilipatikana vipi;
1. 'alias' iliyopatikana kwa kuchukua jina la mtoto mtoro, then mwenye bidii akapewa akaliendeleza kwa kwenda kurudia shule sehemu nyingine. Kundi hili ni kubwa sana Tanganyika, wengi wako kwenye high profile sasa.

2. 'alias' iliyopatikana kwa kuchukua cheti cha ndugu/jamaa/rafiki ambaye anabidii na ameshajiendeleza (mfano yuko university, then mtu anachukua cheti chake cha form four anaenda chuo cha ualimu.....nk). Kundi hili ni kubwa sana Tanganyika hii, na limeenea kwenye sekta za umma zenye kubeba manpower kubwa.

3. 'alias' iliyopatikana kwa kuchukua jina la aliyefanya vizuri na kumpa asiyestahili ili aendelee kielimu. Kundi hili ni dogo kwa vile aliyepewa jina hana uwezo wa kumudu mikiki mikiki ya elimu hivyo nae huwa hafiki mbali.

4. 'alias' iliyopatikana katika utu uzima, kwa kujaribu kudanganya umma ghafla ili kujipatia unafuu wa mambo. Kundi hili ni matapeli. Mfano Dr. Kihiyo.

Nina washkaji wamepiga nae buku jamaa pale MUHAS ndio wamenipa data zake nyingine. Wanasema huyu Dr Kigwangala kichwani yuko njema sana katika masuala ya shule, yaani yuko fiti, ni miongoni mwa 'vipanga' academically. Hilo hakuna anayebisha wanasema. Lakini wanadai pia ni mbishi hard core, yuko arrogant na ni opportunist. Yuko tayari kulipia gharama yoyote ili afanikishe ambitions zake, ndio maana amechukua fedha za Rostam. Wanasema hata kabla hajamaliza chuo alishajaribu ubunge hukohuko Nzega 2005 wakampiga chini. Kipindi hicho ndio alikuwa amemaliza kusimamia ule mgomo wa madaktari uliosababisha anyang'anywe leseni ya kutibu wagonjwa, haruhusiwi kutibu wagonjwa huyo jamaa licha ya 'ukipanga' wake kwenye fani ya tiba.

Kama ana jina la bandia nafikiri haina nguvu hiyo maana kama ni kwenye academics yuko safi, huwezi kumlinganisha na wanaofoji vyeti au wenye degree feki. Hapo kwenye tabia sasa naona ndio kazi ipo, watu wa Nzega wanataka mbunge wa aina hii?
 
Kama ana jina la bandia nafikiri haina nguvu hiyo maana kama ni kwenye academics yuko safi, huwezi kumlinganisha na wanaofoji vyeti au wenye degree feki.

Ikithibitika kwamba hakupata 'alias' hiyo kihalali hawataangalia kama ni kipanga ama la!

Nakumbuka hapa juzi kuna mhadhiri mmoja wa Mzumbe alipoteza hadhi yake kama Senior Lecturer pale 'ilipogundulika' kuwa ni miongoni mwa waliopata PhD kutoka chuo kisichotambuliwa na TCU. Academically huyo jamaa ni kipanga hasa na nina uhakika chuo chochote atakachokwenda ataweza kupata hiyo PhD ndani ya muda mfupi . Ameandika paper nyingi na amehutubu kwenye makongamano amkubwa tu kwenye sector ya elimu na kwengineko kuliko hata hao wenye PhD kutoka vyuo vinavyotambulika (If you google his name, you will just get volumes of his contributions locally and internationally!). Kwa ukuangalia michango yake na anavyofundisha no one can ever doubt that he is a PhD holder!

So kama Dr Kingwangala alipata elimu isivyo halali hata kama ni kipanga itakula kwake.
 
Umenichesha sana...! Tukubali kuwa 'alias' zipo na zina meaning in life. Then twende one step further kujua 'alias' ilipatikana vipi;
1. 'alias' iliyopatikana kwa kuchukua jina la mtoto mtoro, then mwenye bidii akapewa akaliendeleza kwa kwenda kurudia shule sehemu nyingine. Kundi hili ni kubwa sana Tanganyika, wengi wako kwenye high profile sasa.

2. 'alias' iliyopatikana kwa kuchukua cheti cha ndugu/jamaa/rafiki ambaye anabidii na ameshajiendeleza (mfano yuko university, then mtu anachukua cheti chake cha form four anaenda chuo cha ualimu.....nk). Kundi hili ni kubwa sana Tanganyika hii, na limeenea kwenye sekta za umma zenye kubeba manpower kubwa.

3. 'alias' iliyopatikana kwa kuchukua jina la aliyefanya vizuri na kumpa asiyestahili ili aendelee kielimu. Kundi hili ni dogo kwa vile aliyepewa jina hana uwezo wa kumudu mikiki mikiki ya elimu hivyo nae huwa hafiki mbali.

4. 'alias' iliyopatikana katika utu uzima, kwa kujaribu kudanganya umma ghafla ili kujipatia unafuu wa mambo. Kundi hili ni matapeli. Mfano Dr. Kihiyo.
========
Ndugu umechambua vizuri hizo Alias lakini ukumbuke, mtu kutumia jina la mtu/mtoro kujipatia elimu kipato ni kosa la jinai hata kama umeofficialize. Kwanza si tabia njema kwa public official. Badala ya kumsaidia mzazi ampeleke shule mtoto wake, unanunua jina lake na kuhamia shule nyingine. Hapa lazima mtu awajibike.

Kuna alias nyingine umeisahau, ya mtu kutumia cheti cha marehemu!
 
Kabla sijapata details za huyu Kigwangala, nilihamaki na kushangaa sana hapa kwenye forum siku moja alipoweka post yenye jina lake na degree 3, ambazo niliona hazina uhusiano nikahoji kama ni za halali na kama ni dokta kweli au kihiyo.

Nilifanya uchunguzi wangu through my various contacts na kuridhika kuwa at least ile degree ya udaktari (MD) aliisoma Muhimbili, na wenzie wanakiri jamaa is very good in academics. Zile digrii nyingine mbili ni za magirini amezipata kwenye online universities na hazina uhusiano na tiba ya wagonjwa.

Tatizo lake kubwa huyu jamaa inaonekana ni jinsi anavyozitumia akili zake ambazo ziko kama zimepitiliza vile! Data from a very close source zinasema kuwa akiwa daktari pale Muhimbili, aliongoza mgomo mkubwa kuliko yote iliyopata kutokea hapo wakidai nyongeza kubwa ya mshahara. Alikuwa na genge la watu wanaotishia daktari yeyote atakayekiuka mgomo huo. Alikodi bendi ya matarumbeta ikawa inawatumbuiza madaktari na wauguzi wakati wagonjwa wakiendelea kufa.

Wenzie wanadai walikuwa wanashangaa anakopata ujasiri huo maana ndiye kila siku aliyekuwa anawapa waandishi wa habari briefing kila siku kwenye TV na magazeti, alikuwa haogopi chochote! Na hata waziri mkuu wa wakati huo Sumaye alipowatembelea kujaribu kumaliza mgomo, aliitisha kikao usiku kucha kabla waziri mkuu hajafika, kuwa msimamo hautabadilika. Na kweli, alimuumbua Sumaye tena mbele ya waandishi wa habari kuwa bila milioni moja waliyokuwa wanadai hawatorudi kazini, na kweli Sumaye aliondoka bila muafaka huku ndugu wakiendelea kuhamisha wagonjwa wao na maiti zikiendelea kurundikana.

Baadae ule mgomo uliisha na huyu dokta akaadhibiwa na baraza lao la maadili kwa kumpokonya leseni yake, kwa hiyo haruhusiwi kutibu binadamu popote duniani licha ya transcript safi aliyo nayo ya degree ya MD. Akajikita sasa kwenye biashara ya ulanguzi wa pamba, misheni-tauni, siasa, alimradi anajaribu kila anachoweza!

Mbunge wa dizaini hii ataifaa nini nchi? Kama hasikitishwi na vifo maelfu alivyosababisha kwa mgomo wake ule, unatarajia atasikitishwa na ufisadi? Kinachonishangaza hadi leo, hajashitakiwa kwa madhara na vifo vile! Hivyo baraza lao la madaktari linachojua ni kupokonya leseni tu basi, mtu akifa kwa uzembe wa dokta hakuna hatua zaidi! Hapa watu kibao walikufa, na kinara wa mauaji hayo kaletwa awe mbunge wa watu ambao ndugu zao walikufa sababu ya maslahi yake! Hii ndiyo bongoland!
 
Suala si degree yake ya sasa, suala ni kwamba alifikaje huko kwenye degree! Wapo wengi waliofoji vyeti vya shule ya msingi baada ya kufeli darasa la saba na kurudia katika shule nyingine kwa majina tofauti, halafu baadaye wakawa wazuri darasani hadi university. Lakini kuwa kipanga darasani hakuondoi doa la kugushi vyeti, na ni kosa la kuhujumu uchumi.

Sasa mimi sielewi huyu Kigwangala alisomaje hadi kuupata u-Dr, ila naweka angalizo kuwa kama on the way aligushi, basi hapo kuna hoja ya kujadili. Nadhani si muda mrefu M-bongo atakuja kumjibia 'Dr' humu.
 
nadhan la msingi kama mdau alivyouliza hapo juu hatujapata jibu, kwa nini achukuliwe mshindi wa tatu na si wa pili? kama wa kwanza ameonekana hana vigezo si automatic wa pili ndio anachukuliwa? kwa nini selelii atoswe? inaonekana huyu bwana selelii hatakiwi kushinda kwa namna yoyote ile!
 
Mi naona suala la jina bandia halina nguvu hapa maana jamaa hajaiba mtihani wala kufoji cheti cha kitaaluma, kwa kuzingatia hoja ilivyokuja. Na ukimjaribu kwenye qualification aliyo nayo nadhani anaweza kuthibitisha kweli anayo, japo haruhusiwi kutibu wagonjwa.

Mimi naona hoja iko kwenye kisa cha kukatazwa kutibu wagonjwa, maana hiki ndio kina ushahidi. Na je kilichosababisha anyanganywe leseni ya udaktari hakimzuii kuwa mbunge?
 
Duh..inawezekana maana miaka ya nyuma mambo haya ya kurudia shule kwa majina tofauti au kuendelea kwa kutumia jina la mtu mwingine yalikuwapo sana. Huyu tabibu ni member hapa, labda atakuja kuuondoa huu 'ukungu' hapa!

Kama alibadili jina na kujiendeleza kieleza kielimu kwa kichwa chake basi hakuna issue. Kazi itakuwa pale itakapothibitika kuwa alitumia jina la mtu kupatia nafasi ya masomo. Mfano mtu kafaulu kwenda sekondari, halafu akaona hakuna haja au akawa amefariki na kuchukuliwa na huyu jamaa. Hiyo ni jinai ya kughushi cheti
 
nadhan la msingi kama mdau alivyouliza hapo juu hatujapata jibu, kwa nini achukuliwe mshindi wa tatu na si wa pili? kama wa kwanza ameonekana hana vigezo si automatic wa pili ndio anachukuliwa? kwa nini selelii atoswe? inaonekana huyu bwana selelii hatakiwi kushinda kwa namna yoyote ile!
Nimesikiaa kuwa Chiligati alipokuwa anamhalalisha Hamis alisema kwa kuwa Gap(diff) alilypewa Seleli na Bashe lilikuwa kubwa sana inamaana Seleli hakubaliki kwa sasa katika viunga vya NZEGA so kunahitajika damu changa yenye kuleta mabadiliko.. ..nimeshangazwa kweli na majibu ya huyu Katibu uenezi wa chama!!
 
By the way, kwa nini ccm wameamua kumpa mshindi wa tatu (Kingwangala) badala ya yule wa pili (Selelii)?

Kwa mujibu wa Chiligati, baada ya Nec kumwondoa Bashe, nafasi yake imechukuliwa na mshindi wa tatu Dk Hamis Kigwangala aliyepata kura 1,800.

"Nec imeshindwa kumteua mbunge anayemaliza muda wake katika jimbo hilo Lucas Selelii aliyepata kura 2,000, kwa kigezo kwamba amezidiwa kwa kura nyingi na Bashe aliyepata kura 14,000. Kwa maana hiyo wameona kuwa hakubaliki jimboni hapo,"alisema Chiligati.

Mwananchi News paper
 
Mmmh kazi ipo! Na hawa kina Chiligati ndio watu tunaowapa nafasi kuamua mustakabali wa taifa letu.
 
Nafikiri hapa tunachanganya mambo, kama alibadili jina ili apate kurudia darasa sasa kosa ni lake au mzazi wake? kumbuka kwenye miaka ya 70, shule hata za kulipia zilikuwa chache saana mkoa wa Tabora na hasa wilaya ya Nzega imekuja kupata shule ya kulipia mwaka 77.

Na kwa wakati huo huyu kijana asingeweza kufoji, kama ni kosa ni mzazi wake na asingeweza kumkatalia baba yake kwenda shule. Ila kama kaja kufoji cheti huko mbele basi hapo ndo bango libebwe lakini la mambo ya utoto sioni hoja ya kujadili badala yake ni kujionshesha tu tuslivyo vihiyo katika maswala ya sheria
 
By the way, kwa nini ccm wameamua kumpa mshindi wa tatu (Kingwangala) badala ya yule wa pili (Selelii)?

Hata mimi najiuliza hilo ...sipati jibu. Selelii hakukumbwa na tuhuma za rushwa bcoz Takukuru waliamriwa (by you know who) kutoingia jimbo hilo ya Nzega kwa hivyo angestahili kupata, kwani alikuwa wa pili. Na hadi sasa hajakihama chama. Nadhani huu ni mchezo tu wa CCM wa kumridhisha (you know who) kwa kutomuweka hasimu wake Selleli baada ya kumtosa swahiba wake Bashe.

Huu ni mfano mzuri wa kufaulu kwa nguvu ya kundi dogo la mafisadi katika uongozi wa CCM katika azma yao ya kuwaondoa makamanda wa ufisadi. I love this party!!!!!
 
Hivi 2 na 1 ipi kubwa? Hainingii akilini eti serelii na kigwangala wamekaribiana kura then ni bora kuchukua mshindi wa tatu, hivi katiba ya ccm inasema hivyo? au ni chuki binafsi tu? Kwangu mimi hili zoezi la kura la maoni ni kupoteza pesa bure na vilevile limetuonyesha kuwa bila fedha huwezi kupata chochote ktk serikali hii, na bila ya kuwa na 'god father' ndani ya system basi hesabu maumivu!

Watu wameuza nyumba, kuuza mazao, wabunge wametumia pensheni yao kuwarubuni wananchi hii yote kuoneshana jeuri ya pesa tu!

Zoezi la kura za maoni kwangu mimi nalipa grade ya E inayoelekea F kabisa!!!

CCM stop this. 2015 turudi tulikotoka. No democrasy, ni visa na visasi tu! zaidi ni changa la macho.
 
Nafikiri hapa tunachanganya mambo, kama alibadili jina ili apate kurudia darasa sasa kosa ni lake au mzazi wake? kumbuka kwenye miaka ya 70, shule hata za kulipia zilikuwa chache saana mkoa wa Tabora na hasa wilaya ya Nzega imekuja kupata shule ya kulipia mwaka 77. Na kwa wakati huo huyu kijana asingeweza kufoji, kama ni kosa ni mzazi wake na asingeweza kumkatalia baba yake kwenda shule. Ila kama kaja kufoji cheti huko mbele basi hapo ndo bango libebwe lakini la mambo ya utoto sioni hoja ya kujadili badala yake ni kujionshesha tu tuslivyo vihiyo katika maswala ya sheria

Sina uhakika na definition yako ya mtoto. Lakini kwa mfano umewahi kusikia 'watoto' wamekatiwa matokeo ya mitihani wa kosa la wazazi/walezi wao kununua mitihani? Na kufukuzwa shule je kwa makosa ya kinidhamu? Kwa kifupi nataka kusema watoto (hasa katika muktadha wa mjadala huu) hawapo juu ya sheria. Kwa taarifa yako tu, linapokuja suala la jinai watoto wanaweza kufungwa jela (tunayo magereza ya watoto!).
 
Suala si degree yake ya sasa, suala ni kwamba alifikaje huko kwenye degree! Wapo wengi waliofoji vyeti vya shule ya msingi baada ya kufeli darasa la saba na kurudia katika shule nyingine kwa majina tofauti, halafu baadaye wakawa wazuri darasani hadi university. Lakini kuwa kipanga darasani hakuondoi doa la kugushi vyeti, na ni kosa la kuhujumu uchumi.

Sasa mimi sielewi huyu Kigwangala alisomaje hadi kuupata u-Dr, ila naweka angalizo kuwa kama on the way aligushi, basi hapo kuna hoja ya kujadili. Nadhani si muda mrefu M-bongo atakuja kumjibia 'Dr' humu.
We ulishaona wapi "uhujumu uchumi" unakuja kwa kurudia darasa? Kwa sasa hivi nyie mna bahati maana mnasoma kwenye shule za kata, enzi zetu "particularly" kanda ya ziwa tulikuwa tunarudia shule hata mara tano na bado huchaguliwi kwenda sekondari, pia ukumbuke elimu ya msingi ni ya lazima, kinachoangaliwa hapa je mitihani wa kidato cha nne, kidato cha sita, chuo kikuu ni yeye mwenyewe ndo alifanya au alichukua cheti cha mtu, kwa maana ya kwamba hakufanya hiyo mitihani? Kama jibu ni ndio basi ana kesi ya kujibu vinginevyo elimu hiyo ni halali yake, ukumbuke kuwa haku na mtu mwenye haki miliki ya jina. Ndio maana kidato cha pili walikuwa wanarudia darasa kama ikitokea hujafikisha wastani ulio wekwa.

Kuhusu Selelii labda ndo wale wachache ambao Mh Kikwete kama atashinda amewaahidi kuwateua, huwezi jua, ila ina inauma sana wewe uko wa pili halafu anachukuliwa mtu wa tatu wewe unaachwa. Mie ilishawahi kunikuta shuleni, nilimzidi mschana makisi tano, ikabidi aweke namba ya juu yangu kwa vile ni mschana nakuambia sitasahau hiyo kitu.
 
Nafikiri hapa tunachanganya mambo, kama alibadili jina ili apate kurudia darasa sasa kosa ni lake au mzazi wake? kumbuka kwenye miaka ya 70, shule hata za kulipia zilikuwa chache saana mkoa wa Tabora na hasa wilaya ya Nzega imekuja kupata shule ya kulipia mwaka 77.

Weye ndio unachanganya, huyu hakubadili jina bali alitumia NAFASI NA JINA la mtu mwingine kuendelea na masomo. Tunabadilisha majina yetu wenyewe bila kutumia majina ya watu wengine. Kwani ukitumia cheti cha mtu mwingine huwezi kuitwa umebadili jina ila umefanya UDANGANYIFU. So alichofanya huyu ndugu kama ni kweli sio KUBADILI JINA bali kufanya UDANGANYIFU.
 
Back
Top Bottom