Jina la Said Nassor Bogoile ndiye Hamis Andrea Kigwangalla? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jina la Said Nassor Bogoile ndiye Hamis Andrea Kigwangalla?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by M-bongo, Mar 17, 2010.

 1. M

  M-bongo JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 338
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wana JF nimeamua kuja hapa kuomba kutaka kumfahamu huyu Bwana ambae hivi karibuni kama wiki mbili zilizopita alitangaza nia kugombea ubunge Jimbo la Nzega.

  Huyu bwana kwa jina anitwa DK HAMIS ANDREA KIGWANGALA nimeamua kuja kuomba msaada wa kutaka kumfahamu huyu Daktari wa binaadam ni kwasababu,nikiwa mkazi wa Dar ninaetoka Kijiji cha MIGUWA kata ya MIGUWA wilaya ya Nzega jimbo la Nzega ndugu zangu baada ya kumsikia huyu mtu huko kwetu wamekuwa wakiniuliza kuwa je nmfahamu?anafaa kuwa mbunge wetu?kwa sasa jimbo la nzega watu ambao wanafahamika na wana makundi makubwa ni LUKAS SELEII,NA HUSSEIN BASHE huyu daktari amekuwa mtu wa tatu kufahamika kama mgombea mtarajiwa kupitia ccm.

  Kwanini nataka kumfahamu.
  1) nisingependa kuwajibu ndg zangu juu ya mtu nisiemfahamu na wo wamevutiwa kusikia kuna mgombea mwingine kwani sasa jimbo la nzega baada ya miaka 15 ya mbunge selelii wananchi wengi wanataka kuwafahamu hawa wagombea wapya.

  2) nimeleta hili hapa kwa kuwa naamini wapo wanaoweza kunisaidia kunipa taarifa sahihi juu ya huyu daktari na hii forum imekuwa usuful sometime kutupatia taarifa.

  Ningependa kuwasilisha kama wapo wanaoweza kutusaidia angalau kufahamu credibillity yake,leadership abillity n mengine ili kuweza kutoa majibu sahihi.

  Binafsi baada ya taarifa hizi nitamtafuta ili kuweza kuoanisha taarifa nitakazopata hapa na yy binafsi

  naomba kuwasilisha
  =================

  UPDATE:

  Majibu ya Dr. Kigwangalla (MB)

   
 2. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #2
  Jun 9, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Hi M-bongo, habari za Miguwa au za wapi?

  Jaribu kusoma hapa kigwangalla.blogspot.com na utapata wasifu wangu kama nilivyouandika mwenyewe nilipotangaza nia ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Nzega.

  Pia waweza cheki hapa PEERCORPS - Home kwa taarifa zaidi kuhusu shughuli zangu za kijamii, na jaribu kusearch kwenye Google unawezapata some hits zinazomhusu Kigwangalla.

  Kuna watu wengi sana humu wamewahi kusoma na au kufanya kazi na mimi sehemu mbalimbali, wanaweza kukupa majibu mengine na ya ukweli na uwazi zaidi kuhusu mimi na uwezo/uzoefu wangu wa uongozi, kuhusu credibility n.k., n.k.

  Jina langu kamili ni hili hapa: Dk. Hamisi Andrea Kigwangalla (wengine huandika jina langu la ukoo kama Kigwangala) hivyo unaposearch jaribu kuweka yote mawili na utapata taarifa nyingi kidogo kuhusu mimi...

  Ukitaka kujua zaidi kuhusu mimi na kutoka kwangu, nipigie kwenye namba za simu zilizopo kwenye blogu yangu [kwenye tangazo langu la nia.

  Ahsante sana mniMiguwa mwichane [nilisoma Mwanzoli shule ya msingi mnamo mwaka 1991.

  Regards,
  H.K.
   
 3. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ninaomba kuongeza kidogo kuhusu Dr. Kigwangalla,
  Mimi ni mmoja wa watu ambao nimebahatika kumfahamu Dr wakati akifanyakazi Golden Pride Mine huko Nzega, hadi akisoma Mhimbili, ninaomba kukiri kuwa nilisikitika sana pale niliposikia kuwa Dr Kigwangalla amesimamishwa kazi Mhimbili kwa kujihusisha na mgomo (yeye akiwa kiongozi wa huo mgomo) matarajio yangu yalikuwa ni kwamba Tanzania imebahatika kuwa na watu kama akina Kigwangalla, mtu makini mwenye weledi wa hali ya juu na nilitarajia kuwa angeleta mafanikio makubwa kwenye tasinia ya afya, niliongea naye binafsi kumpa pole na kueleza kusikitishwa kwangu na uamuzi wa hovyo wa serikali kumpoteza Kigwangalla (Dakitari ambeye nilitarajia awe bingwa na tumaini kubwa kwa Tanzania).

  Nilifurahi sana niliposikia kuwa Serikali imewarudisha kazini madaktari wale, lakini hata hivyo nilisikitika nilipoongea na Kigwangalla tena akaniambia hatarudi kazini, nilimsihi sana lakini tayari alikuwa amechukua uamuzi wake.

  Hata hivyo kumbe yeye aliiona nyota yake katika mambo mengine na kwa kweli waingireza husema "Quality means no Compromise" na ndivyo ilivyo kwa Kigwangalla baada ya kuamua kuingia kwenye biashara sasa ni miongoni mwa watu wa kuigwa kwa mafanikio anayoendelea kuyapata, ninamuombea kwa Mungu asije akaharibika kwenye siasa, ni miongoni mwa watanzania wachache ambao nikisikia wanagombea uraisi nitawaunga mkono kwa kila hali.

  Ningelikuwa Dr. Kigwangalla nisingeligombea ubunge sasa, ningeliendelea na biashara halafu nikaanza kufundisha watu wengine ili nao wafanikiwe katika vitu wanavyovifanya (wadhungu wanaita Public Speaking) na uandishi wa vitabu vya kuwahasisha wengine ili wafanikiwe, ningelifanya hivyo halafu baadaye nikagombea Urais (baada ya kutimiza miaka 45) nikiwa nimefanya kazi na watu (kupitia kuwafundisha) na nikiwa nimewaelewa watu. Ningefurahi sana kama nchi hii ingeweza kumpata mtu asiyejishughulisha na siasa akagombea urais..

  Atafaa sana kwani kama mfanya biashara atakuwa anaweza kuendesha nchi kama business entity na kama a public speaking person atakuwa amekutana na watu wa aina mbalimbali na nina amini kuwa Tanzania inahitaji mtu ambaye hajaharibika na makundi na tamaa za kwenye siasa awe rais wetu.

  Hata hivyo naomba nimtakie kila la kheri Dr. Kigwangalla, na ninamuombea ashinde apatiwe uwaziri wa afya ili awasaidie madaktari wenzaka ambao alishindwa kuwasaidia kipindi akiwa kiongozi wa mgomo wao, awaboreshee mafao ili waache kurukaruka na ili waweze kuitumia taaluma yao kwenye udaktari na ili tusiwapoteze watu wenye weledi kama wa kwake katika siasa.

  Kila la heri Kigwangalla
   
 4. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #4
  Jun 23, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Ahsante sana Ntemi, japokuwa umeficha jina, najaribu kukung'amua lakini wapi!

  I wish wanaJF waliokuwa wakichangia kwenye ile thread nyingine iliyofungwa kule wasome huu mchango wako labda watapata kumjua H.Kigwangalla ni nani na ana wasifu gani.

  Wengine walishaanza kutaka kusema eti ni school drop out....ha ha ha, kweli ukitaka kuchafuka we tangaza nia tu!!!

  Malengo yangu makubwa ni kuleta mapinduzi kwenye siasa za kiTanzania, kuhamasisha wimbi jipya la siasa - kutoka siasa za kuongea sana bila kutenda na kuelekea kwenye siasa za kiutendaji zaidi! Maendeleo yanawezekana tu kama tutapata viongozi wazuri, na mimi najiamini ni kiongozi mzuri, tena mzuri sana kuliko hata baadhi ya viongozi wanaozoa sifa huku sisi tunaowajua historia zao tunacheka tu pembeni!

  Kama unavyopafahamu kwetu na asili yangu, nadhani ndo maana unashangaa leo hii kuniona nimefika hapa, mafanikio yangu ni ya kazi halali ya mikono yangu na wala si ya kurithi au kupewa au kupendelewa... nimejituma kwa kufuata kanuni na taratibu na mafanikio nikayapata! Hivyo ninaamini katika kufanya kazi kwa bidii na maarifa na bila kukata tamaa. Na ndo maana nataka niwe mfano hai wa uongozi unaotakiwa ili kuleta mabadiliko nchini kwetu.

  Kuna kauli nyingi sana nazisoma kutoka kwa watu wanaoonekana kuwa makini sana, hapa JF, FB na hata kwenye mtandao wa watu tuliosoma na kufanya kazi Muhimbili, nyingi ni za kukata tamaa na pengine wengi wanafikiria kuwa hii nchi imeoza kiutawala na haiwezekani kubadilika, wengine wanakuwa na hasira tu bila hata mikakati ya kuangalia kwamba wao kama wao wanafanya nini ili kuleta mabadiliko?

  Tunashindwa kuelewa kwamba tuna tatizo moja kubwa la kimtazamo na kifikra...tunakuwa slow kwenye ku-take actions towards implementation of action plans of the change we want to see, we want to be...we feel like there is a super being called 'politician' or 'government' somewhere who is the solution to all our problems and that this super being is not doing his job, he is arrogant, deaf, corrupt, incompetent, dead etc etc etc ...na kusahau kwamba serikali ni sisi, inawekwa na sisi, inafanyiwa kazi na sisi; sasa ni nani alaumiwe? Tunafanya nini ili kuleta mabadiliko?????????????? Au tunalaumu tu na kupiga kelele kwa kuwa hatujaingia humo ndani (mjengoni - wengi wana dhana finyu ya kufikiri kuwa wenye dhamana ni wabunge na mawaziri tu) na kufanya kazi?

  Hivi wanaJF wenzangu humu wanafanya kazi wapi? Wengi watakuwa humu humu nchini, najua wachache wako nje...lakini je sisi hawa hawa tuliopewa dhamana kwenye sehemu zetu za kazi, are we the best in what we do? Au tumeshakata tamaa na sisi tumeamua kuoza tu...Kama wewe unachagua wabunge wanaokubali kila kitu na unawaacha wawakilishe jimbo kwa zaidi ya miaka 15 unategemea mabadiliko kweli? Kama unachagua mbunge ambaye hawezi kuchambua makabrasha na kuhoji unategemea mabadiliko kweli?

  Lets be realistic here! Kama unahamasisha watu wasiende kugombea wamuachie mtu asiyefaa eti kwa sababu amechangia hoja ya Richmond....atafanya kazi kweli huyu asipopambana kupata nafasi? Inabidi wabunge na hata Rais wapate Challenges kali kupata nafasi ili akiingia afanye kazi kweli kweli kulinda kura zake, maana bila hivyo hatarudi tena mjengoni! Hata mimi nikiwa mbunge, wengine na waje wagombee na kama nikiwa sijawaridhisha wapiga kura basi na wasinipe tena fursa ya kuongoza!

  Ningeongea mengi lakini naomba niishie hapa kwanza.

  Kigwangalla.
   
 5. D

  Diwani Member

  #5
  Jun 24, 2010
  Joined: Feb 3, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dr bado una safari ndefu sana nimepata taarifa toka Nzega kuwa una kila sifa ya kuwa Mbunge isipokuwa programu zako ndizo zitakazo kufanya usifike popote labda kama una tangaza jina tu
  1. Kampeni meneja unayemtumia ana sifa za kula ada na michango ya klabu mbali mbali za mpira kule Nzega
  2.Kampeni meneja huyo anatumia muda mwingi kuranda na piki piki nyekundu uliyo mnunulia mitaani akitamba kuwa kanunuliwa na wewe hi vyo kuwa nya wapiga kura wengine kunung'unika
  3.umetumia karibu laki nne au tano hivi kununua Tv na kuikabidhi kwenye kijiwe cha kahawa(BBC) il hali wapiga kura wa CCM kwenye kijiwe hicho hawazidi watano
  4.lets keep in touch Dr nipo Tinde kwa sasa
   
 6. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Dr. Kigwa,

  Nakutakia kila la heri, maombi yangu kwako ni kuwa usitusaliti kwa tamaa za siasa. Kumbuka kuwa mali na heshima zinazopatikana kwa dhuluma na hila hazileti furaha ya ndani kama umasikini unaoletwa na dhuluma. Najua utashinda uchaguzi kwa sababu najua unaweza, chonde chonde Dr, ukifanikiwa kawe mkweli na mwaminifu kama ambavyo ninakufahamu.

  Ukipata nafasi soma The Law of Success by Dr. Napoleon Hill, it will enrich your spirit for equity and fairness in your endeavours.
   
 7. senator

  senator JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Hizo facts ulizotoa zinaonesha Dr anakwenda kuuza Jina ili wananzega wamjue then 2015 atakuwa tayari na amejulikana...Huyu Bashe nasikia anafadhiliwa RA ilikumwondoa msaliti Lumambo Selelii.Bashe alikuwa mpiga debe mzuri sana kipindi cha 2005 wakati huo akiwa anamsupport Seleli baada ya kuvunjwa makundi yao..Dr Hamis ushauri tu ..kawaida mwanzo ni mgumu na ukichukulia unapambana na King maker ni vyema ukaosha jina tu wajumbe wa nzega wapate kukufahamu...karibu majengo kwa mama lyimo tupate asusaa
   
 8. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #8
  Jun 28, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  @Diwani, nashukuru sana kwa ushauri wako wa bure kabisa - ahsante sana ndugu yangu! Naomba nikujibu hoja zako kuwa huyo unayesema anazunguka na pikipiki anajua yeye mwenyewe anafanya nini na ametumwa na nani, na wala si kampeni meneja wangu kwa kuwa mimi bado sijaanza kampeni na wala sina Kampeni Meneja! Nikianza utajua na utauona tu moto wangu...

  Kuhusu TV - mimi sina mkakati wa kuwanunulia watu kitu chochote kile ili wanipe kura...sema nauza sera na mikakati yangu na kama watu wakiinunua basi na wataniunga mkono, na mpaka sasa sijaona mtangaza nia hata mmoja aliye na mikakati madhubuti ya kuleta maendeleo pale Kwetu kunishinda, na hivyo watu makini kama nyie mnatakiwa muwaelimishe wanaNzengo waniunge mkono...NINAAMINI SANA KAMA UMEWEZA KUFUATILIA HARAKATI na shughuli ZANGU PALE NZEGA BASI UNAJUA UKWELI KUHUSU MIMI NA FOCUS YANGU NA KAMA U-MKWELI UTAKUBALIANA NA MIMI KWAMBA WENGINE WANAPIGA SIASA ZA POROJO TU BASI, HAKUNA UTENDAJI! Na zama za Porojo tunatakiwa tuzizike na tupate aina nyingine ya siasa - za kiutendaji zaidi!.

  @Senator, Kuhusu Kingmaker - mimi nafahamu Kingmaker ni Mungu tu na watu wamepewa na watapewa nguvu na Mungu kufanya maamuzi sahihi...hakuna mtu mmoja anayeweza kuwatawala watu kwa muda wote! Hivyo mimi najipanga tu na wakati wa kampeni ukifika tutaeleza tunajipanga kuwafanyia nini wanaNzega (hapa namaanisha nje ya ILANI ya CHAMA - kwamba mbunge wetu anakuja na ubunifu gani kwanza yeye kama yeye???). Ni imani yangu unajua mpaka sasa hivi mimi kama mimi nimeishawafanyia nini wanaNzega?

  Mimi pia nilijitokeza kuwania Ubunge wa Nzega mwaka 2005 na niliungwa mkono sana tu na watu, nashukuru sana kwa hili na ninaamini safari hii watanipa fursa ya kugombea Ubunge kupitia CCM na nitawashinda wagombea wengine kwa kishindo na kuwa Mbunge wa Nzega...makini kuliko! Subiri uone.
   
 9. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Dr kwa mipango na mikakati yako CCM haikufaiii...hamia upinzania uwe mgombea hapo nzega!!! hufanani kabisa na matendo ya CCM!!!!!!!!!! Waachie CCM, seleli na bashe ubabaishajii wao kwani wanafananiaa naoooo...
   
 10. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #10
  Jun 28, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  @Diwani, Ijumaa au Jumamosi ya wiki hii nitapita Tinde nikusalimie, nipe namba yako.
  yangu hii 0784636963
   
 11. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #11
  Jun 28, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Ungeweza mPM mkuu hapa umeweka kwa JF yote!
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Jun 28, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hamisi, nakumbuka aliyosema hayo ni Masa na hakusema ni wewe bali alikua na mtu wanaojuana vyema ambaye alishatajwa huko nyuma...

  In your post, jaribu sana kutotupa makombora kwani wote tunaishi nyumba za vioo.... sera yako ya maendeleo ni sawa na nadhani ni generic kwani wana-CCM wote husema hivyo

  Kipindi kibaya sana, usiji-expose sana kama hakuna sababu, be a good listener hata kama unasifiwa, wengine humu tunatega tu
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Jun 28, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu, hii pikipiki siyo msala kweli huu alisema Dk. Hosea, au vipi??? unamharibia ntu eh??
   
 14. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #14
  Jun 28, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Dr Kingwangwa!

  Ur talking the obvious! maendeleo yamekuwa ni wimbo wa wanaCCM. Hebu angalia tulipo sasa tokea tumepata uhuru. Unakuja na wimbo tuliouzoea masikioni. Kipya ni kipi mazee?
   
 15. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #15
  Jun 28, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  @Masanilo, Ahsante sana. nimekosea. Nxt tym
   
 16. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #16
  Jun 28, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Unataka kuzifanyia kazi gani Mkuu?
   
 17. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #17
  Jun 28, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Ahsante sana De Novo kwa ushauri mzuri na pia kwa kujali, sasa nafahamu wazi kuwa ulisoma Muhimbili, na kwamba ulikuwa mwaka wa mbele yangu na Unatokea kanda ya ziwa...need I say more? Keep it up bro. You have a good analytical eye...I didn't know this before!
   
 18. n

  newazz JF-Expert Member

  #18
  Jun 28, 2010
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 471
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 60

  Nd. Hamis Kigwangala,

  1.Maamuzi ya kugombea ni sahihi.

  2.Kugombea kwa chama gani na wakati, umekosea

  3. Kama ambavyo watu wamedai, kwamba u mpiganaji- hata hukuridhishwa na hali pale Muhimbili.
  Kama ndivyo, hadi mkafukuzwa, imekuaje ukapata maridhiano na CCM, kwani ni serikali hiyohiyo iliyokufukuza?

  Kwa wale waliosoma Petals of Blood- Ngugi Wa Thiongo- mtu mmoja alikuwa kama Dr. Kigwangala, kafukuzwa shule/ chuo, kumbe yeye ni geresha, baadaye huyo mtu akaja kuonekana ni msaliti mkubwa. Aliwashirikisha wenzie mgomo, kumbe si mwenzio., wakaishia kufukuzwa , hali yeye akaja kusomeshwa nje ya nchi na serikali hiyohiyo..Mmh

  Mimi Dr. Kigangwala naheshimu maamuzi yako, lakini nina wasiwasi na wewe. Isije ukawa unatumika na mafisadi, kwani ipo mikakati mahususi imesukwa kuwaondoa wabunge wapiganaji bungeni.

  Kigwangala kwanini wakati huu?

  Kimtazamo kama umekielewa kilio cha wananchi juu ya mafisadi na jinsi mabadiliko yalivyo magumu kupatikana, sidhani kwa kugombea CCM hata kama ukishinda , unaweza kuleta mabadiliko yoyote. Utadhibitiwa na wazee ( mafisadi), utapenyeza vipi mikakati yao ambayo itakuwa tofauti na CCM?

  CCM wenyewe wanakataa mabadiliko, ndio maana wanawadhibiti wabunge wanaopigania maslahi ya wananchi wanyonge, inatia aibu bunge wakati linaanza kupata meno, tukiona michango mizuri ya maana kutoka kwa akina Selelii, Kyembe, Shelukindo na wengineo, baadhi ya watu wanajitokeza kudai wanataka kuleta mabadiliko kwa kuwang'oa wabunge pendwa wa wananchi, mngesubiri ili kwanza upepo huu upite, msiwasaidie mafisadi , hata kidogo.

  Muda bado upo upande wako, lakini Kigangwala na vigangwala wengine msikubali kutumia, hata kama mtadai mna uhuru wa katiba au wananchi wamewaita, bado itakuwa vigumu kuamini kuwa dhamira zenu za kugombea ni HURU.

  Naomba kuwakilisha
   
 19. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #19
  Jun 28, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Kigwagalla
  Mimi naona na wewe ni mmojawapo wa wale watu wa RA ambao wanataka Selelii, mwakyembe, anne Kilango, Sitta na yule wa kiteto waondoke. Hiyo ni timu inayotaka mabadiliko hasa iko kinyume na ufisadi. Na mafisadi wameunda mikakati ya kuwamaliza. Ikiwa unataka mabadiliko nzega ningekushauri uwe upande wa sellelii au ugombee kwa chama kingine. Mawaoz mapya hayahitajiki ndani ya CCM.

  CCm imeshafikia ukomo wa kufikiri.
   
 20. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #20
  Jun 28, 2010
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,650
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  "Doctor" Kingwangalla, naomba nifahamu ulisomea nini na lini ulimaliza masomo Karolinska Institute? Jee unaweza kutaja title ya Thesis yako? Naona hamna rekodi yoyote kama ulisoma Karolinska Institute...
   
Loading...