jina la rais kikwete latumika wananchi kuporwa ardhi mkuranga hekari 52 na kupewa armcement

ONDIECK OTOYO

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
254
44
KAMATI YA MGOGORO WA MALIPO YA ARDHI ‘ KATI YA MWEKEZAJI WA KIWANDA CHA . MAWENI LIME STONE NA WANANCHI WA . KIJIJI CHA KISEMVULE . P.O. Box 10 MKURANGA PWANI
Tarehe 13/03/2014
Kumb: KMA/KKM/MD/II/3/2014
Kwa KATIBU MKUU Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi P.O. Box 9132 DAR ES SALAAM
Kk. Katibu wa Baraza la Ardhi Kijiji cha Kisemvule P. O. Box 10 Mkuranga -Pwani
katibu:
YAH: UKIUKWAJI WA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA 1977 IBARA YA 24(2), SHERIA YA ARDHI NAMBA 4 YA 1999 KIPENGE CHA 1 (1) (G) NA SHERIA YA ARDHI YA VIJIJI NAMBA 5 YA 1999 KIPENGELE CHA 3(1)(G) , SHERIA YA ARDHI NAMBA 47 YA 1967 (ACQUISITITION), UKIUKWAJI ULIYOFANYWA MAKUSUDI NA VIONGOZI WA WILAYA MKURANGA WAKISHIRIKIANA PAMOJA NA MWEKEZAJI WA KIWANDA CHA CEMENTI CHA MAWENI LIME STONE (RHINO) KWA NIA YA UWIZI NA DHULUMA NA KUPORA ARDHI YETU BILA MALIPO STAIKI KWA KUSINGIZIA NA KUTUMIA JINA LA RAIS KWAMBA NDIYE ALIYETAIFISHA ENEO LETU BILA SHERIA KUZINGATIWA KATIKA MALIPO YA FIDIA
Katibu Mkuu husika na somo hilo hapo juu,
Kwa mujibu wa sheria ya ardhi namba 4 ya 1999 kifungu cha 15 kinavyoelekeza juu ya mgogoro wa maslai katika ardhi, tunalazimika kuleta mgogoro huu kwako ili tuweze kupata haki yetu kwa mujibu sheria husika,
Katibu Mkuu katika mgogoro huu tupo wananchi 29 tuliyo porwa ardhi yetu kati yetu 3 wamegoma kupokea Hundi zao hadi sasa na 26 walipokea malipo yasiyo lingana na thamani halisi ya mali na bila kupewa ardhi mbadala kwa mujibu wa sheria, baada ya kulagaiwa na viongozi wa wilaya mkuranga kuwa tathmini ingefanyika upya na kuongeza malipo na mwekezaji, pamoja na kupewa viwanja mbadala, hivyo baada ya kuangaika kwa muda mrefu bila mafanikio tumelazimika kuchangua kamati ya watu 3 miongoni mwetu kufuatilia malamiko yetu, ambao ni 1. Abrahamu Mathayo 2.Sauda Omari 3.Mwamedi Heri ,kielelezo ‘’MD1 na MD2’’ taarifa ya kikao cha tarehe 04/06/03 na majina ya waligoma kuchukua hundi zao hadi sasa
1. Katibu Mkuu Kwa niaba ya wananchi wenzetu wa kijiji cha kisemvule tupenda kuleta malalamiko yetu kwako juu ya ukiukwaji wa makusudi wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya 1977 Ibara ya 24(2), sheria ya ardhi namba 4 ya 1999 kifungu cha 1(1) (g) na sheria ya ardhi vijiji namba 5 ya 1999 kifungu cha 3(1)(g) Sheria ya Ardhi namba 47 ya 1967(acquisition Act,) na kanuni ya 6 ya madai ya fidia ya Ardhi,2001 jambo iliyotekelezwa na viongozi wa wilaya ya mkurunga,afisa ardhi wa wilaya mkuranga pamoja na mwekezaji wa kiwanda cha MAWENI LIME STONE(RHINO) kilichojengwa katika kijiji cha kisemvule kwa kupora ardhi yetu yenye ukubwa wa hekari 52 bila kuzingatia matakwa ya kisheria katika msingi ya dhuluma na uwizi kwa maslai ya mwekezaji.

2. Katibu Mkuu viongozi wa wilaya mkuranga na idara ya ardhi wilaya ya mkuranga kwa kushawishiwa na mwekezaji walikiuka sheria makusudi sheria ya ardhi vijiji na 64 (1)(2)(3) na (44) ya 1999 corrupt transactions na sheria namba 4ya 1999 na kushindwa kuzingatia sheria katika kutupora ardhi yetu na kushidwa kutumia form 70 wala form 1 kwa mujibu wa sheria ya ardhi namba 4 ya 1999 kifungu 179 na kanuni za ukadiriaji fidia GN78(2001)katika kutathmini mali zetu, pamoja na kutupa ardhi mbadala kwa mujibu ya sheria ya ardhi namba 4 ya 1999 kifungu1(1)kipengele g(v) inavyoelekeza katika kutafisha ardhi, huku tukilalamika kwa muda mrefu bila ufumbuzi huku mkuu wa wilaya akigoma kujibu barua zetu na kusababisha sisi tuendelee kukosa haki yetu kwa muda mrefu bila ufumbuzi, kielelezo ‘’MD3”orodha ya majina na tathmini ya nyumba pamoja na mazao,

3. Katibu mkuu sheria ya ardhi namba 4 ya 1999 kifungu cha156, 158(3)(f) na sheria ya ardhi namba 47 ya 1967 (acquisition act,) kifungu cha 4(c) vilikiukwa kwa makusudi na washirika wa uwizi na dhuluma katika mazingira ya rushwa, tena bila kujali matakwa ya kisheria

4. Katibu Mkuu kitendo cha viongozi wa wilaya mkuranga kutangaza kuwa ardhi yetu imetaifishwa na mweshimiwa rais, bila kuwepo na tangazo la serikali kwa mujibu wa sheria ya ardhi namba 4 ya 1999, sheria ya ardhi vijiji namba 5 ya 1999 na sheria ya ardhi namba 47 ya 1967 (acquisition act,) kwa lengo ya dhuluma na uwizi, inathibitisha bila kuacha shaka juu ya washirika hao kupanga na kutekeleza uwizi huo, dhidi ya mali zetu, na maeneo yetu.

5. Katibu Mku mnamo tarehe 09/03/2013 tulipeleka malamiko yetu kwenye baraza ya ardhi kijiji cha kisemvule na Meneja wa kiwanda ndg; GODFREY MWAILONDA simu 07555000568 na wenzake wawili walifika na baadaye baraza ikatoa maamuzi tarehe 11/04/2013 kuwa mkuu wa wilaya ahandikiwe barua, mkuu wa wilaya mkuranga ndg MARCY SILLA simu 0754600458 akandikiwa barua tarehe 27/05/2013 kutoka baraza la Ardhi kijiji cha kisemvule , yeye alipokuja aliingia tu kiwandani na kuongea na viongozi wa kiwanda na kuondoka kimya kimya bila kutueleza wananchi wanao lalamika juu ya dhuluma iliyotekelezwa na kiwanda kwa kutumia jina la Rais jambo ilisababisha wananchi wachukie na kutaka kuandamana tukawasii wasiadamane tuendelee kufuatilia

6. Katibu Mkuu mnamo tarehe 08/07/203 baraza ya ardhi kijiji ikaandika tena barua kwenda kwa mkuu wa wilaya mkuranga ndg MARCY SILLA simu 0754600458 ikiwa na orodha ya wadai na thamani ya madai barua ambayo akuweza kujibu hadi leo na kusababisha wananchi kuchukia zaidi, pamoja na jitiada hizo zote ufumbuzi iliendelea kushindikana, baada ya kuona dhuluma inaendelea na wananchi wamekata ikiwa ni pamoja na jitiada zetu zote na kutumia gharama na kuzuia wananchi wenzetu wasifanye maandamano wala ujuma lakini mpaka sasa serekali imeshindwa kutusadia pamoja na swala hili kuifikisha kila pahali wilayani mkuranga pamoja na mkoani pwani huku wananchi wakiendelea kukata tama na kukosa imani na serekali, Kuwa imewapora ardhi yao na kuwapa mapepari, wanyonyaji katika misingi ya rushwa bila malipo katika misingi ya kisheria

7. Katibu Mkuu Madai ya Msingi katika Sheria za Ardhi ni:- (a) ardhi mbadala kwa mujibu ya sheria za ardhi (b) malipo staiki katika bei ya soko juu ya mali (c) bei halali ya thamani ya mazao kulingana na bei elekezi ya sasa kutoka wizara ya kilimo na chakula (d) gharama ya usumbufu (e) gharama ya usafiri (f)6% ya gharama zote kwa mujibu wa sheria


Wako katika ujenzi wa taifa

…………………………… …………………………… ……………………….. 1. Abrahamu Mathayo 2. Sauda Omari 3. Mwamedi Heri Simu 0762763252, 0655763252 Waathirika/Wakilishi wa Wanakijiji wa Kisemvule Waliyoporwa Ardhi yao
Nakala kwa
1. Mwenyekiti wa kamati ya Bunge Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi P.O. Box 9133 Dar es Salaam

2. Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Na Biashara P.O. Box 9503 Dar es Salaam

3. Mtathmini Mkuu Wizara ya Ardhi Na Maendeleo ya Makazi P.O. Box 9132 Dar es Salaam

4. Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Kuzui na kupambana na Rushwa (Takukuru) P.O. Box 4865 Dar es Salaam

5. Katibu wa Mkuu wa Mkoa Pwani P.O. Box 30080 Kibaha – Pwani

6. Mkuu wa Wilaya Mkuranga P.O. Box 1 Mkuranga – Pwani

7. Mkurugenzi wa Wilaya Mkuranga
P.O. Box 1
Mkuranga –Pwani

8. Mkurugenzi Mtendaji
Maweni Lime Stone (RHINO CEMENT)
P.O. Box
Mkuranga
 
Back
Top Bottom