Jina la Magufuli labamba Uingereza: Ukumbi mzima wa Chuo Kikuu cha Coventry wazizima baada ya kusoma jina la muhitimu kutoka Tanzania.

Maprofesa wa Chuo Kikuu cha Coventry nchini Uingereza, wakiongozwa na Mkuu wa Chuo, Irene Glendinning, pamoja na Ukumbi mzima, ulizizima wakati jina la Mtanzania aitwaye Dk. John Pima lilipotajwa wakati wa Mahafali ya wahitimu wa Kozi ya Uzamivu wapatao 11 waliotoka katika Mataifa tisa duniani.
Dk. Pima ambaye alikuwa shuhuda, alieleza kuwa, baada ya jina lake kusomwa ili aende mbele kutunukiwa shahada ya Uzamivu, walipotaja tu John Pima from Tanzania, shangwe ziliibuka wakitaja Magufuli .... Magufuli ... Magufuli ... Tanzania."
Dk. Pima alieleza kuwa, baada ya mahafali, maprofesa na wahitimu wenzake walimfuata na kumuulizia habari za Rais Magufuli wanazosikia kwenye vyombo vya habari wakitaka kujua ni mtu wa namna gani? Wengi walipongeza kasi na msimamo wake wa:
  • kukusanya mapato,
  • kudhibiti matumizi ya fedha za umma,
  • kushughulikia mafisadi,
  • ununuzi wa ndege,
  • upanuzi wa bandari
  • ujenzi wa barabara za juu
  • uanzishwaji wa viwanda.
Walidai Nchi nyingi za kiafrika zina rasilimali nyingi lakini Viongozi wao hawana uthubutu wa kufanya maamuzi magumu na hawana maono kama ya Rais Magufuli, na kwamba hawatambui kuwa kama wanaweza kujiletea maendeleo pasipo kutegemea misaada kutoka mataifa makubwa.

View attachment 842223
There are so many ways to become popular.

As one who is famous is popular so is the notorious! Amuulize Mpoto:sio kila wakupigiao makofi wanakushangilia. Waingereza? Gentlemen! Kwani wale learned advocates waliomwandikia barua hawamfahamu mpaka kuulizia habari za Magufuli? Mgambilwa unajua kutafuta sana habari. Mbona unazipata tu. Uzipendazoooo. Za kujipendekeza!
 
katajwa john pima watu wanashangilia, kwani hawezi kua ni mtu mwingine? Kwa hio john pima ndio john pombe? Au mie ndio sijaelewa!!?
 
hadi Aliens watamkubali mkuu wetu,acheni wenye roho mbaya wafe kwa wivu huku tz
PhD mara nyingi ni miaka 3 au zaidi, iweje wasiulize maswali hayo siku zote hizo waje wamwulize siku ya graduation? Au alikuwa anasoma online? Kuna uwongo na propaganda hapa.
Huenda ukumbi ukizizima baada ya kusikia kuna mtu kutoka nchi ya ajabu ajabu inayonunua watu naye amefanikiwa kutunukiwa PhD.
 
Maprofesa wa Chuo Kikuu cha Coventry nchini Uingereza, wakiongozwa na Mkuu wa Chuo, Irene Glendinning, pamoja na Ukumbi mzima, ulizizima wakati jina la Mtanzania aitwaye Dk. John Pima lilipotajwa wakati wa Mahafali ya wahitimu wa Kozi ya Uzamivu wapatao 11 waliotoka katika Mataifa tisa duniani.
Dk. Pima ambaye alikuwa shuhuda, alieleza kuwa, baada ya jina lake kusomwa ili aende mbele kutunukiwa shahada ya Uzamivu, walipotaja tu John Pima from Tanzania, shangwe ziliibuka wakitaja Magufuli .... Magufuli ... Magufuli ... Tanzania."
Dk. Pima alieleza kuwa, baada ya mahafali, maprofesa na wahitimu wenzake walimfuata na kumuulizia habari za Rais Magufuli wanazosikia kwenye vyombo vya habari wakitaka kujua ni mtu wa namna gani? Wengi walipongeza kasi na msimamo wake wa:
  • kukusanya mapato,
  • kudhibiti matumizi ya fedha za umma,
  • kushughulikia mafisadi,
  • ununuzi wa ndege,
  • upanuzi wa bandari
  • ujenzi wa barabara za juu
  • uanzishwaji wa viwanda.
Walidai Nchi nyingi za kiafrika zina rasilimali nyingi lakini Viongozi wao hawana uthubutu wa kufanya maamuzi magumu na hawana maono kama ya Rais Magufuli, na kwamba hawatambui kuwa kama wanaweza kujiletea maendeleo pasipo kutegemea misaada kutoka mataifa makubwa.

View attachment 842223
Hakuna kitu kama hicho in uk. Huyo cjui mpina aendelee kuwadanganya wadanganyika. Hapa Ni uk co tz
 
Mod, hebu uondoe uchafu huu hapa jukwaani kwani hautufikirishi!
Hivi huyu mgambilwa anaijua lugha ya kebehi (satire )? Alijuaje kuwa wale walikuwa wanashangilia kwa mazuri na sio kumsanifu? Akarudie kusoma juu ya perception ndio alete hui upuuzi hapa?
Hivi kumbe kujikomba ni shughuli pevu eeeh
 
Huyu Dr Pima atakuwa anafanya publicity ili apate attention na hatimaye kazi baada ya kumaliza chuo.Hata hivyo hongera kwa ku-graduate,hatutegemei GPA ya 32 hapo.
 
....ulizizima wakati jina la Mtanzania aitwaye Dk. John Pima lilipotajwa wakati wa Mahafali.... Je? ndiye yule alikuwa Mwl wa Computer iaa Njiro na baadae akala uteuzi wa Mh na kuwa afisa elimu huko tabora? Kama ndiye ntarudi baadae!

Nadhani kwa sasa ni DED wa Kaliua maana ndio anaitwa Pima na alikuwa anatafuta PhD
 
Back
Top Bottom