Jina la Khamis Mgeja hatarini kukatwa CCM

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=2][/h]JUMATANO, SEPTEMBA 19, 2012 08:48 NA MWANDISHI WETU, SHINYANGA

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Shinyanga, anayewania nafasi hiyo, Khamis Mgeja, jina lake liko hatarini kukatwa. Mkakati huo umedaiwa kuwa ni moja ya mikakati ya baadhi ya vigogo walioko katika harakati za kupanga safu zao zitakazowawezesha kushiriki ipasavyo kampeni za kumpata Mgombea Urais wa mwaka 2015 kupitia CCM.

Chanzo chetu kimesema kuwa, wanaoongoza mkakati huo ni wanaompinga Mgeja kwa kuwa hayuko katika kambi yao.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, hivi sasa vigogo hao wanafanya kila aina ya ushawishi kwa wajumbe wa ngazi za juu, ili kuhakikisha jina la Mgeja linakatwa na kubakizwa mgombea wanayemtaka wao, kwa kuwa atawasaidia wakati wa kampeni hizo.

Mmoja wa wajumbe wa CCM mkoani Shinyanga, alisema ili kufanikisha mkakati huo awali vigogo hao walimshawishi mwanachama mmoja, ili aweze kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo ya Uenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga, kwa lengo la kumng’oa Mgeja, katika nafasi hiyo.

“Kuna vikao vinafanyika katika maeneo mbalimbali mjini hapa na taarifa hizi hata baadhi ya watu wamezifikisha TAKUKURU, ili iweze kuwafuatilia maana kuna madai ya kumwaga fedha kwa wajumbe na hili linafanyika kwa sababu watu wanapanga safu zao za viongozi.

“Kibaya zaidi aliyekamiwa sana ni Mgeja, huyu inashinikizwa jina lake lisirudi kabisa, maana ndiye anayeogopwa na baadhi ya vigogo hao wa kitaifa, wanafanya kila juhudi akatwe na tayari wamemuandaa mtu wao ili achukue nafasi hiyo, kwa sababu wanaamini atawasaidia,” alisema Samwel Steven mkazi wa Ibadakuli.

Kwa upande wao baadhi ya wazee wa CCM waliohojiwa na mwandishi wa habari hizi, walielezea masikitiko yao kuhusiana na mikakati hiyo ambayo walisema haina maslahi yoyote kwa chama bali kwa watu binafsi.

“Iwapo kweli haya tunayoyasikia yatakuwa ni ya kweli, basi viongozi wetu hawakitendei haki chama chetu, mara kwa mara tunaelezana wanachama tudumishe ushirikiano na mshikamano, lakini wao wanaonekana kutenda tofauti na wanafanya kampeni chafu zitakazosababisha tugawanyike, hii ni hatari,” alisema mwana CCM huyo kwa sharti la kutotaja jina.

Kwa upande wake, Mkazi wa Kata ya Shinyanga Mjini, Juma Amani, alisema kuwa ili kuondoa malumbano yasiyo na tija ndani ya chama, ni vizuri vikao vya mwisho vya uteuzi vikawa makini katika kuteua majina ya wagombea.

“Mimi nashauri ni vyema vikao vya uteuzi vikapuuza propaganda zozote chafu zinazoweza kusababisha CCM kupoteza watu muhimu na makini, hii itasaidia kuepusha mambo ambayo yamewahi kutokea huko nyuma, maana baadhi ya wana CCM waliobaini kuchezewa mchezo mchafu kama unavyoandaliwa sasa walikimbilia vyama vya upinzani, mfano Dk. Slaa,” alisema Juma.

 

Sijasikia wakifikiria kukata JINA la PRINCE - Ridhwani...
 
Alternative moja iliobakia katika kukuzwa kwa demokrasia ya kweli ni kuwepo kwa private candidacy. corruptive thoughts za vyama na nguuvu zao zitakuwa balance na khofu ya private candidate ili kuondosha khatamu za nchi kuongozwa na vyama ana kurudisha heshima ya uongozi kwa wananchi.
 
Ni kawaida yao CCM kufanyiana umafia na vp Prince wa MR.President hataki nafasi nayeye mna havumi lakini yumo..
 
kambi ya membe haimtaki mgeja..huyu ni kambi ya lowassa na haogopagi kumchana sitta kila anapopata mda..
 
Wasimkate mgeja, maana hajui siasa na wala hana ushawishi. Nguzo yake kuu ni udini.
 
Eti TAKUKURU wameshapewa taarifa ili kufuatilia nyendo za watu!! This is bullshit, hawa jamaa wanakuwa active wakati wa chaguzi za ccm tu tena wanatumiwa kuchafua watu! Lol, bora taasisi kama takukuru zisingekuwapo kwenye ramani ya nchi yetu!
 
Mimi nadhani huyu jamaa anajihisi na kutumia vyombo vya habari kutaka kujinasua,mimi ningekuwa Mwenyekiti wa chama taifa,ningehakikisha yoyote ambae hakutumikia chama vyema,ikiwemo kupoteza idadi ya majimbo ya uchaguzi ambayo yalichukuliwa na chama tofauti na chama cha huyu Mwenyekiti wa mkoa.

Kama Mwenyekiti wa mkoa umeshindwa kuhakikisha majimbo hayaendi kwa wapinzani wa chama chako,kwa hakika hufai kuendelea kuwa Mwenyekiti wa chama mkoa!hii ni kwa chama chochote kile!kwa kifupi ni kwamba kashindwa kazi!haijalishi yuko kambi gani ndani ya chama husika.
 
Back
Top Bottom