Jina la Gavana wa BOT Prof. Luoga linavyowanufaisha matapeli

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Jeshi la Polisi Mkoani Arusha linawashikiliwa watuhuniwa wawili wa utapeli wa kutumia mtandao ambao wamekuwa wakitumia jina la Gavana wa Benki kuu Tanzania (BOT),Prof,Frorence Luoga kutapeli watu mbalimbali baada ya kufanikiwa kusajiri jina lake kwenye laini ya simu.

Kamanda wa polisi Mkoani hapa akiongea na vyombo vya habari Jana ,amewataja watuhuniwa hao kuwa ni Juma
Yahaya(33) mkazi wa Sakina na Amani Mbise(32) mkazi wa Sombetini na Maji ya Chai Mkoani Arusha ambaye amejenga jumba la Kifahari kupitia zao la uhalifu huo.

Amesema kuwa watu hao wamekutwa na vitambulisho nane vya watu mbalimbali ,mtambo wa kusajiri laini za simu pamoja na simu sita wanazojishughulisha kusajili laini za
simu kinyume cha sheria.

Kamanda Shana amedai kwamba mtuhumiwa Amani kupitia utapeli huo amefanikiwa kujenga nyumba ya kifahari Maeneo ya maji ya chai fedha zilizotokana na zao la uhalifu huo wa kutumia jina Profesa Luoga.

Amesema kuwa watuhumiwa hao wamekuwa wakitapeli kupitia mitandao ya kijamii na Facebook kuwatapeli watu mbalimbali kwa kutumia jina hilo ambapo baada ya upelelezi wamekiri kosa hilo.

“Baada ya kuwapekuwa watuhumiwa tuliwakuta na simu 6,mashine mbili ya kusajili kwa alama za vidole,laini mbalimbali,vitambulisho 9 ya wateja ambao walishawasajilia laini zao za simu na kwamba tumebabaini mtuhumiwa huyu anamiliki jumba la kifahari eneo la Maji ya Chai wilayani Arumeru mkoani hapa,hali ambayo aiendani na kipato chake” alisema

Aliongeza kuwa jeshi hilo lilipokea malalamiko kutoka kwa Gavana Luoga kuhusiana na watu hao kutumia jina lake na ndipo walianza upelelezi na kufanikiwa kupata akaunti ya face book na kubaini namba 0785349763 iliyosajiriwa kutumia hati ya kusafiriabya Norrish Andrew James RAIA wa Australia.

Alisema kuwa raia huyo wa Australia alifika nchini akitokea Nchini Kenya na kufanya usajiri wa namba ya simu kwa wakala aitwaye Juma Hussein ambapo wakala Huyo alishirikiana na mtuhumiwa Alan Mbise kwa kutumia hati hiyo ya kusafiria

Kamanda alisema watuhumiwa wote wanashikiliwa na polisi kwa upelelezi zaidi na watafikishwa mahakamani Mara baada ya uchunguzi kukamilika.

Wakati huo huo jeshi la polisi kwa kushirikiana na Idara ya ustawi wa jamii jiji la Arusha imefanya operesheni ya kuwaondoa watoto wadogo wanaofanya biashara mbalimbali ikiwemo kubebeshwa mizigo kati masoko mbalimbali ya jijini hapa.

Amesema watoto wapatao 105 wamekamatwa ambapo kati yao 46 wana umri chini ya miaka 18 na 59 wana umri wa zaidi ya miaka 18 na kwamba polisi inaendesha operesheni kwa wazazi wasiotaka kuwapeleka shule watoto wao.

IMG_20191111_102902.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom