Mbowe anaenda kubadilisha historia ya Tanzania

NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
1,281
2,020
Huyu bhana pamoja na kuzaliwa kipindi cha uhuru lakini dalili zinaonesha anaenda kukuza uhuru wa kufurahia demokrasia hapa nchini.

Ninatamani sana kesi yake ingurume ili tuone matendo ya kigaidi aliyoyafanya ili nilinganishe na ya Ole Sabaya na ya Mnyeti halafu ikiwezekana afungwe kabisa si mchezo.

Wakati mwingine unawaza pia kwa kuwa inasemekena anaumwa, hivi ikitokea anafariki mikononi mwao itakuwaje?

Tunakosa hekima na busara katika kiwango cha kutisha! Ninamkumba JK kwa kweli!
 
Akifariki jela na bibi anafariki ikulu muda mfupi baadaye.
 
Huyu bhana pamoja na kuzaliwa kipindi cha uhuru lakini dalili zinaonesha anaenda kukuza uhuru wa kufurahia demokrasia hapa nchini.

Ninatamani sana kesi yake ingurume ili tuone matendo ya kigaidi aliyoyafanya ili nilinganishe na ya Ole Sabaya na ya Mnyeti halafu ikiwezekana afungwe kabisa si mchezo.

Wakati mwingine unawaza pia kwa kuwa inasemekena anaumwa, hivi ikitokea anafariki mikononi mwao itakuwaje?

Tunakosa hekima na busara katika kiwango cha kutisha! Ninamkumba JK kwa kweli!
Huyu maza ni katili sn na hatari zaidi ya shetani
 
Historia ya nchi hii ni ndefu na pana.

Lakini sasa mh mbowe anakwenda kuibadirisha na kuwa ya kusikitisha badala ya kutia moyo kwa upande mmoja. Na kwaupande wa pili vizazi vijavyo vitakuja jifunza ujasiri wa Mbowe ktk kusimamia haki na kuitaka mikononi mwa wadhalimu.

1. KUSIKITISHA
Mh. Mbowe ni MtanMbowetunayemfahamu vizuri, kitendo cha kudai tume huru na katiba mpya mpaka kumtengenezea kesi ya ugaidi, INAUMIZA SANA!

Miaka ile ya kikwete Zanzibar makanisa yalichomwa moto na paroko mmoja kuuawa. Mihadhara ya kiislam ilitukana sana dini ya kikristo, karate zilifundishwa misikini. Intelijensia ya kikwete ikawabaini mashehe kadhaa kuhususika na ugaidi.

Mh Samia amewatoa mara alipoingia. Watu tunajiuliza intelijensia gani hii iyobaini kuwa mbowe ni gaidi?
Amefanya jambo gani la kigaidi au amekutwa na kitu gani kinachotia mashaka au kuonesha Moja kwa mmoja kuwa anastahiri kutuhumiwa ugaidi?

2. UJASIRI
Toka mbowe ameingia upinzani, hajapata raha na radha ya siasa kama wanavyopata wengine -- Misukosuko, taabu, dhiki na madhira kibao. Lakini amesimama imara kuitetea na kuidai haki na kuidai kutoka kwa wadharimu. Hii inaenda tengeneza historia nyingine, kumpata mtu mwingine jasiri anayekubali kudhalilika kwa maslahi ya wengi.

Tumeona wengine wamefutiwa mashtaka lakini Mbowe mashitaka yapo palepale. Hii inatuonesha serikali ya samia suluhu lengo lake ni Mbowe.

Jumuia za kimataifa zitamuweka Mbowe kwenye orodha ya mashujaa hasa tukipata Uhuru wa kweli na katiba mpya.
 
Eti anashutumiwa kupanga njama za kulipua vituo vya mafuta na mikusanyiko ya watu. 😂😂😂
2859525_cab442ed-ce7a-4892-bf0b-b8e9f509d46f.jpg
2859526_4aadc128-1f17-4fe4-83c2-6c06e642c090.jpg
2859527_3ecd8307-2380-4cb4-9ec6-4e3ea9734069.jpg
 
Moyo wa mtu msitu. Mbowe anaweza akawa gaidi au sio gaidi, ukweli utajulikana na mahakama itaamua. Hata enzi za Zaire kuna watu hawakuamini kama Mobutu ameshiriki mauaji ya Lumumba kutokana na wema alioanza kuuonesha kwa wazaire wa wakati ule, lkn baadae ikaja kujulikana na kugundulika kuwa yeye (Mobutu) ndio alikuwa chanzo cha mauaji yale ya kinyama kwa waziri mkuu wao, pia wakaja kugundua kuwa Mobutu alikuwa ni mtu katili kuliko ukatili wenyewe.
 
Back
Top Bottom