Jina Dr. Magufuli latawala kila mahali uchaguzi mkuu wa Kenya. Tanzania tunapata ujumbe gani?

ujumbe unaoupata ni kuwa tz yaweza kuingia matatizoni watu watajua ili rais wa kenya ashinde, lazima nguvu au mchango flani utatoka tz, na hatimae kesi kama ya marekani na urusi
Sijui mnalaana gani nyinyi.
Kila jambo ni kujitisha tu. Mbona hamjiamni ndan ya nchi yenu?
Uchaguzi ufanyike kenya tz ndio ishtakiwe ,, kivp?
 
Naongezea kidogo, wanamsifia mamba anayekula mtoto wa jirani yao, siku akiliwa mtoto wao ndo watajua kwamba mamba si mdudu rafiki kwa binadamu.

Sent from my HUAWEI G610-U20 using JamiiForums mobile app
 
Kila mgombea huko Kenya anaposimama na kumwaga Sera zake na jinsi atakavyo wahudumia wakenya atakapochaguliwa baada ya uchaguzi ni lazima ajifananishe na Rais wa Tanzania Dr Magufuli Katika suala nzima la uwajibikaji bila kumuogopa yoyote.

Kila mikutano ya hadhara jina la Dr Magufuli limekuwa likitumika Katika kijinadi kwa wagombea.

Hii inatoa ishara gani kwa nchi za Africa Mashariki?

Kuwa Magufuli ni mchapakazi na anayewajali wananchi wake, ila nitacheka kama Kenyatta anakuja na sera kama hii. Alikuwa wapi siku zote wakati yeye alikuwa rais kabla ya Magufuli?
 
Marais wastaafu ??? Hawa ambao magufuli anasema walibakia kidogo tu wauze nchi???? Ama marais gani hao???? Nipe credible source ya kenya kuwa wanamkubali magufuli sio mnalazimisha hoja za kuokoteza eti PLO lUmumba!!!!who the hell is he
Save your energy Bro! Utakufa kwa stress bure.
Hasa utakapokuja jikuta umebaki wewe na BAK na Salary slip tu!
Wapinzani makini wote wanajua ukweli kuwa JPM ndio story ya dunia.
Akina Lema wameshaanza kuumiza vichwa nani atakayeweza kuvaa viatu vyake 2025? Hajaona! kasema hata ndani ya CHADEMA hajaona MALAIKA kama JPM.
 
Sijui mnalaana gani nyinyi.
Kila jambo ni kujitisha tu. Mbona hamjiamni ndan ya nchi yenu?
Uchaguzi ufanyike kenya tz ndio ishtakiwe ,, kivp?
Waambie hao nashangaa wanahangaika na uchaguzi wa Kenya na kuleta maneno ya utata tu.oooh tz tutashitakiwa na wengine wameenda mbali zaidi eti kama Marekani na Urusi.
 
Pro chadema wana vijiba sana wakimsikia Rais Magufuli anakubalika

Mimi niko Kenya haya ni kweli tupu
 
Kila mikutano ya hadhara jina la Dr Magufuli limekuwa likitumika Katika kijinadi kwa wagombea.

Hii inatoa ishara gani kwa nchi za Africa Mashariki?
hawaelewi kinachoendelea Tanzania, wangekuwepo Tanzania hata siku moja wasingeendelea kulitaja hilo jina.
 
Libya, Gadafi aliwapa kila kitu na nchi yao ilikuwa na maendeleo lakini Walibya wakamkataa. Ilinichukua muda kuelewa kilichowasibu Walibya. Kumbe haki ndio huinua taifa na Watawala, kumbe Walibya walikosa utawala wa sheria - Uhuru ambao ni fundamental, kuheshimika kama binadamu anayetaka kuongea juu ya machungu yake, kuongea juu ya mustakbali wa nchi yake na maisha yake.
Sidhani kama kuna mmoja wetu humu jukwaani atakubali kufungwa mdomo halafu ukafunguliwa wakati wa kula na wakati waliokufunga wanataka useme wanalotaka wao tu. Huku ndio tunakopelekwa Watanzania.
Ndo maana wanavuna walichopanda. Libya ya utawala wa gadafi huwezi kufananisha na nchi yoyote duniani. Majority wa Libya walimpenda sana ila mapadikizi ya wazungu ndo walimuua wakisaidiana nao. Jiulize je ukipewa Uhuru wa kutukana utapata huduma za jamii zinazohitajika ?
 
Kila mgombea huko Kenya anaposimama na kumwaga Sera zake na jinsi atakavyo wahudumia wakenya atakapochaguliwa baada ya uchaguzi ni lazima ajifananishe na Rais wa Tanzania Dr Magufuli Katika suala nzima la uwajibikaji bila kumuogopa yoyote.

Kila mikutano ya hadhara jina la Dr Magufuli limekuwa likitumika Katika kijinadi kwa wagombea.

Hii inatoa ishara gani kwa nchi za Africa Mashariki?
Wahenga walisema "adhabu ya kaburi aijuaye maiti".

Wenzao wakatilia msisitizo Kiingereza kwa kusema "The grass is greener on the other side".

Sent from my Kimulimuli
 
Magufuli nampa asilimia 70 zakua na nia nzuri na maendeleo ya Tanzania lakini nampa 30 kwa namna ya utekelezaji wa nia yake. Kwa hiyo hata wakenya wakimsifu wapo sahihi kabisa kwa sababu utamu wa ngoma uingie kuicheza.

mafisadi hayana chama
 
Back
Top Bottom