Jimboni Kalenga: CCM wamsimamisha Geodfrey Mgimwa kugombea ubunge

Kamati Kuu ya CCM, chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, imempitisha Godfrey William Mgimwa kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM, katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, utakaofanyika Machi 16, mwaka huu.
Akizungumza na waandfishi wa habari leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, Katribu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema, Kamati Kuu ya CCM imemridhia Godfrey kupeperusha bendera ya CCM baada ya kukidhi vigezo licha ya kuongoza katika kura za maoni jimboni humo
Godfrey ni Mtoto wa aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Kalenga na pia Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa ambaye ameliacha wazi jimbo hilo baada kufariki dunia Januari 1, 2014.
Pichani, Nape akimtambulisha Godfrey kwa waandishi wa habari, leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam
 
Yasije yakatokea kaama yale ya Sioi Sumari, yule kijana aliyetaka kurudhi jimbo la baba yake na kuishia kukosa kura za huruma.

2. Nape akimnadi Sioi Makumira.jpg
 
mgimwa.jpg

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akimtambulisha mgombea wa Ubunge kwa tiketi ya chama hicho katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa, Godfrey William Mgimwa jana. Picha na Bashir Nkoromo

KWA UFUPI
Kabla Kamati Kuu haijampitisha, Mgimwa wiki iliyopita alishinda kura za maoni kwa kupata 342, huku mshindi wa pili Jackson Kiswaga akipata kura 170, watatu ni Hafsa Mtasiwa aliyeambulia kura 42.

Dar es Salaam. Wakati Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM ikimpitisha Godfrey Mgimwa (32) kuwa mgombea wa chama hicho Jimbo la Kalenga, mkoani Iringa, Kamati Kuu ya Chadema inakutana keshokutwa kuteua jina la mgombea wake.

Mgimwa ni mtoto aliyekuwa Mbunge wa Kalenga na Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa aliyefariki Januari Mosi mwaka huu, Afrika Kusini alikokuwa akipata matibabu.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nauye alisema jana kuwa jina hilo lilipitishwa kwenye kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika Ikulu chini ya Mwenyekiti wake, Jakaya Kikwete.

"Kwa hiyo tunatangaza rasmi kwamba Godrey Mgimwa ndiye mgombea wa chama chetu Jimbo la Kalenga," alisema Nape.

Tayari Tume ya Uchaguzi imepanga Machi 16, mwaka huu kuwa siku ya uchaguzi Jimbo la Kalenga.

huku kampeni zikifanyika kuanzia Februari 19 hadi Machi 15.

Akifafanua, Nape alisema wana CCM wana imani na mgombea huyo kuwa atashinda kwa kishindo na kulichukua jimbo hilo.

Naye Ofisa habari wa Chadema, Tumaini Makene, alisema mbali na CC kufanya uteuzi, pia itapokea ya uchaguzi wa madiwani uliofanyika mwishoni mwa wiki.

Makene alisema pia kuwa Kanda mbalimbali kulikofanyika uchaguzi huo, zilipewa jukumu moja la kuhakikisha mambo yanakwenda vema, lakini kutokana na matokeo yaliyopatikana, kila Kanda inatakiwa kuandika ripoti ya uchaguzi huo kabla ya CC kutoa kauli rasmi ya kufanyika uchaguzi huo.

Nape ajibu hoja

Akijibu shutuma kwamba, jimbo hilo linarithishwa kifamilia, Nape alisema chama hicho hakiwezi kumnyima mwanachama yeyote haki ya kuwania kwa sababu tu wazazi wake waliwahi kuwa viongozi. "CCM haiwezi kumzuia Godfey kuwania eti kwa sababu ni mtoto wa marehemu Dk Mgimwa, yeye ana haki ya kuwania kama watu wengine tunachoangalia ni uwezo wake na hilo limeonyeshwa baada ya wananchi wa Kalenga kumpa ushindi wa kishindo," alisema.
Alivionya vyama vya upinzani kwamba muda wa kampeni ukifika kufanya mikutano ya kistaarabu kwa sababu chama hicho hakitavumilia vurugu.

Aliwapiga kijembe Chadema kuwa wanatakiwa kuandaa Chopa nyingi zaidi ili ziweze kuwazungusha katika kata 13 ilizopo kwenye Jimbo hilo ili wajaribu bahati yao.

Naye Mgimwa akizungumza, aliishukuru Kamati Kuu kwa kumpitisha kuwa mgombea ubunge katika jimbo hilo.

"Natoa shukurani zangu za dhati kwa Kamati Kuu kunipitisha kugombea ubunge, sitawaangusha," alisema Mgimwa ambaye anafanya kazi katika Benki ya Stanbic.

Kamati Kuu jana jioni iliendelea na kikao chake ikiwa ni maandalizi ya Kikao cha Kamati ya Maadili kitakachokaa kesho mjini Dodoma.

Kikao hicho kinatarajia kuwahoji baadhi ya vigogo wa chama hicho waliokiuka maadili ikiwemo kutangaza kugombea urais kinyume na taratibu za chama hicho.AFYA YA NGOZI : Hamira na madhara yake kwa kinywa, koo

Kwel kabisa naona tunaanza kurudia tawala za kifalme...hapo hakuna cha uwezo wala babu yake uwezo..sympathy tu ndo imewafanya wakamchagua!
 
Jimbo la Uchagunzi la Kalenga Tanzania haliko kama unavyofikiria.Si jimbo ambalo mtu ametawala miaka kumi.Kama kitatoa mtu makini wa Kalenga penyewe hapo shughuli itakuwa nyingine.
Ujumbe hiyo barometa ya Jimbo la Uchagunzi la Kalenga Tanzania haliko kama unavyofikiria.Si jimbo ambalo mtu ametawala miaka kumi.Kama kitatoa mtu makini wa Kalenga penyewe hapo shughuli itakuwa nyingine.
Ujumbe hiyo barometa ya Jimbo la kalenga ya tarime cha mtoto.mtu kama vitus innocent lawa kwa chama chochote kalenga atasumbua.babu yake vangisada makendi ni alikuwa sub chief makini wa kalenga mpenda watu na maendeleo.mzee vitus beatus lawa ni kati ya walimu wa kwanza wa sekondari,nyerere akiwa st msry's tabora na pugu yeye alikuwa tosamaganga.

Baba(mwalim innocent vitus lawa) na mama yake(angelica vangisada makendi) ni watu waliofanya kazi katika jimbo hilo.kama kweli atapitishwa na chadema kwa uwezo aliouonesha akiwa mwalimu wa sekondari funguni tanga,bumbuli lushoto na akiwa headmaster mlalo ngwelo lushoto.pale chuo kikuu st augustine university mwenge moshi,akiwa waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi,he proved to be an astute politician,a politician with a profound vision.ţ,a cynosure of this era of political transformation in the country.kama ni vitus innocent lawa vs geofrey mgimwa.mgimwa atadhalilika.
 
ningechangia lakini nimepata kichefuchefu,najua kuna watanzania wapumbavu, halafu kuna watanzania wananunuliwa kuwa wapumbavu,ili upumbavu huo upumbaze wengine,ni kama uchawi hivi,lakini huu unatokana shida zetu!
 
mgimwa.jpg

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akimtambulisha mgombea wa Ubunge kwa tiketi ya chama hicho katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa, Godfrey William Mgimwa jana. Picha na Bashir Nkoromo

KWA UFUPI
Kabla Kamati Kuu haijampitisha, Mgimwa wiki iliyopita alishinda kura za maoni kwa kupata 342, huku mshindi wa pili Jackson Kiswaga akipata kura 170, watatu ni Hafsa Mtasiwa aliyeambulia kura 42.

Dar es Salaam. Wakati Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM ikimpitisha Godfrey Mgimwa (32) kuwa mgombea wa chama hicho Jimbo la Kalenga, mkoani Iringa, Kamati Kuu ya Chadema inakutana keshokutwa kuteua jina la mgombea wake.

Mgimwa ni mtoto aliyekuwa Mbunge wa Kalenga na Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa aliyefariki Januari Mosi mwaka huu, Afrika Kusini alikokuwa akipata matibabu.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nauye alisema jana kuwa jina hilo lilipitishwa kwenye kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika Ikulu chini ya Mwenyekiti wake, Jakaya Kikwete.

"Kwa hiyo tunatangaza rasmi kwamba Godrey Mgimwa ndiye mgombea wa chama chetu Jimbo la Kalenga," alisema Nape.

Kabla Kamati Kuu haijampitisha, Mgimwa wiki iliyopita alishinda kura za maoni kwa kupata 342, huku mshindi wa pili Jackson Kiswaga akipata kura 170, watatu ni Hafsa Mtasiwa aliyeambulia kura 42.

Tayari Tume ya Uchaguzi imepanga Machi 16, mwaka huu kuwa siku ya uchaguzi Jimbo la Kalenga.

huku kampeni zikifanyika kuanzia Februari 19 hadi Machi 15.

Akifafanua, Nape alisema wana CCM wana imani na mgombea huyo kuwa atashinda kwa kishindo na kulichukua jimbo hilo.

Naye Ofisa habari wa Chadema, Tumaini Makene, alisema mbali na CC kufanya uteuzi, pia itapokea ya uchaguzi wa madiwani uliofanyika mwishoni mwa wiki.

Makene alisema pia kuwa Kanda mbalimbali kulikofanyika uchaguzi huo, zilipewa jukumu moja la kuhakikisha mambo yanakwenda vema, lakini kutokana na matokeo yaliyopatikana, kila Kanda inatakiwa kuandika ripoti ya uchaguzi huo kabla ya CC kutoa kauli rasmi ya kufanyika uchaguzi huo.

Nape ajibu hoja

Akijibu shutuma kwamba, jimbo hilo linarithishwa kifamilia, Nape alisema chama hicho hakiwezi kumnyima mwanachama yeyote haki ya kuwania kwa sababu tu wazazi wake waliwahi kuwa viongozi. "CCM haiwezi kumzuia Godfey kuwania eti kwa sababu ni mtoto wa marehemu Dk Mgimwa, yeye ana haki ya kuwania kama watu wengine tunachoangalia ni uwezo wake na hilo limeonyeshwa baada ya wananchi wa Kalenga kumpa ushindi wa kishindo," alisema.
Alivionya vyama vya upinzani kwamba muda wa kampeni ukifika kufanya mikutano ya kistaarabu kwa sababu chama hicho hakitavumilia vurugu.

Aliwapiga kijembe Chadema kuwa wanatakiwa kuandaa Chopa nyingi zaidi ili ziweze kuwazungusha katika kata 13 ilizopo kwenye Jimbo hilo ili wajaribu bahati yao.

Naye Mgimwa akizungumza, aliishukuru Kamati Kuu kwa kumpitisha kuwa mgombea ubunge katika jimbo hilo.

"Natoa shukurani zangu za dhati kwa Kamati Kuu kunipitisha kugombea ubunge, sitawaangusha," alisema Mgimwa ambaye anafanya kazi katika Benki ya Stanbic.

Kamati Kuu jana jioni iliendelea na kikao chake ikiwa ni maandalizi ya Kikao cha Kamati ya Maadili kitakachokaa kesho mjini Dodoma.

Kikao hicho kinatarajia kuwahoji baadhi ya vigogo wa chama hicho waliokiuka maadili ikiwemo kutangaza kugombea urais kinyume na taratibu za chama hicho.AFYA YA NGOZI : Hamira na madhara yake kwa kinywa, koo

Lazima Wampoze Kwani Kuna Makubwa Juu Ya Baba Yake Kulala Pumzi Ya Milele na Wanafamilia Wangehoji Ya Yangekuwa Mengine na Hali Ya Hewa Ingechafuka Hivyo Kwenye Udhia Penyeza Rupia na Kinachomtokea Huyo Dogo Ndiyo Kile Kile Alichofanyiwa Huyo Aliyenae hapo ktk Picha Kwani hata Yeye Pia Amepewa hicho Cheo Kama Sehemu Ya Kupoza Hasira Za Kifamilia Juu Ya Kifo cha Mdingi Brigedia MN baada Ya Kuwa ktk Mapambano Afghanistan............................. Ngoja Niishie Hapa ila CCM Nawakubali Sana Kwa Strategies Zao. Namalizia Kwa Swali Hili : Je Mnadhani baada Ya Dogo Kupitishwa Kugombea Ubunge Ule Muendelezo wa Familia Ya Marehemu WM wa Kuhoji Nini Kilipelekea Kifo Cha Mpendwa Wao hadi Wao Wenyewe Kudai na Hata Kutamka Kuwa Alilishwa Sumu Utaendelea????????????? Jamani Njaa na Dhiki ni Mbaya Sana.
 
hawa ccm hawana akili wamesahau arumeru huu siyo utawala wa kifalme bhana
 
Wanatafuta kura za 'huruma' hawa..hawakujifunza tu walipozikosa kwa 'Sioi Sumari' Dogo-Janja akachukua jimbo kiulainiii!
 
Ngoja tusubili wa Vyama vya Upinzani watakao pitishwa hasa kile chama cha M4C.
 
Back
Top Bottom