Tetesi: Jimboni Bumbuli: Hii tunaisubiria hadi kesho hamna utekelezaji

Baba wa Mapaka

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
1,813
1,629
Bumbuli Development Corporation (BDC)
December 3, 2013 ·


Bodi ya Barabara Mkoani Tanga (TANROADS) imepitisha maombi ya kupandishwa hadhi barabara zenye urefu wa kilometa 130 zinazounganisha vijiji 9 katika Halmashauri mpya ya Bumbuli, mkoani Tanga.

Barabara hizo ni muhimu kwani zinaunganisha makao makuu ya Bumbuli na halmashauri za wilaya ya Lushoto na Korogwe kupitia kwenye barabara za mkoa za Mombo/Lushoto/Soni/Bumbuli/Dindira na Kwamote pamoja na Mashewa na Bombo Mtoni.

Barabara zitakazounganishwa na vijiji 9 kuwa ni Soni/Mponde/Funta/Tamota/Kerenge ambazo zina urefu wa kilomita 60. Barabara nyingine ni pamoja na Mbelei/Mgwashi/Milingano/Mashewa zenye urefu wa kilomita 70.

Kupandishwa hadhi kwa barabara hizo kutasaidia usafirishaji wa mazao ya wakulima katika jitahada za kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na hatimaye kuinua maendeleo ya Halmashauri ya Bumbuli kwa ujumla.

Habari kamili: http://bit.ly/IHCzaD
 
Zitasaidia sana wananchi kwakweli ila bado kunahaja ya kuendelea na maeneo mengine kwani yapo maeneo ambayo barabara ni muhimu pia mfano, Barabara ya Chekelei, Kwemzuza, Kiluwai, Kishewa, Bazo, Kihitu, Shashui, Soni,

Pia ukifika kihitu unaenda Kwemhafa, Mponde, Kweminyasa, Tekwa, Wena, Bumbuli,

Pia kihitu, Kwendoghoi, Kwepunda, Kivilicha, Kwemzuza nayo itafungua uchumi wawana bumbuli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom