Jimbo la Ukonga Vepe!?

Ngonepi

JF-Expert Member
Jun 2, 2013
1,872
1,206
Nikiwa kama mkazi wa jimboni humu Ukonga nasikitishwa na hali ya maendeleo ilivyo jimboni humu!!

Ubovu wa barabara kwangu ni kikwazo na kero kubwa sana!

Barabara ni chache sana lakini ni mbovu sana pia!

Barabara zilizo katika kata za Kitunda yote na Kivule vitongoji ambavyo ndio vikubwa na vyenye wakazi wengi sana jimboni humu, barabara ni mbovu mmno na hazijajengwa tangu Uhuru!!

Jimbo hili limeongozwa na chama tawala tangu kuundwa kwake isipokuwa mwaka huu ambapo upinzani wanaongoza!
Tukiachana na mambo hayo ya siasa, binafsi nawaomba wahusika watujengee miundombinu jimboni humu maana imekuwa kero kubwa kwa wakazi wa jimbo hili kwa kweli!!

Wakazi wa Ukonga na wana Daresalaam wote tusaidiane kupeleka kilio hiki kwa wahusika wote!!

Nawasilisha.
 
Makusanyo ya kodi yanakua kwa mujibu wa TRA na Hazina hivyo nafikiri mtaanza kuona matunda ya kulipa kodi.
 
Sijui kama watasikia maana hawa Watawala wa Serikali hii ni zigo la misumali.
 
Back
Top Bottom