Uchaguzi 2020 Jimbo la Ukonga kuna shida, isiposhughulikiwa CCM tutampa tena mpinzani. Waliochukua fomu wengi ni mamluki wa tuliyemkataa 2015

msaboi2020

Member
Jun 20, 2020
11
9
Ukonga ni miongoni mwa majimbo 3 ambayo yapo katika Wikaya ya Ilala. Wengi wa wakazi ni wa kipayo cha chini na wachache cha kati.

Mwaka 2020 ni mwaka wa uchaguzi, kama kawaida mengi hujitokeza. CCM Ilala, DSM na taifa wasipotafakari 2020 jimbo tutaligawa kwa Upinzani tena. Zaidi ya wanachama 150 wamechukua fomu kuomba ridhaa ya kupitishwa na CCM kugombea ubunge Ukonga. Hii inaleta shaka kwa mustakabali wa jimbo wilaya na CCM kwa ujumla.

Jamaa asiyetakiwa Ukonga (MATOKEO YA 2015 YALIDHIHIRISHA HATA BAADA YA KUMWAGA PESA NYINGI). Amekuwa na hila za ajabu mno ili ashinde:

1) Amekuwa akifanya mikutano na kugawa kiasi kikubwa cha fedha chini ya uangalizi wa TAKUKURU Ilala, Mf: jana alikuwa Kata ya Majohe na Ukonga na briefcase yake ya hela, si sawa.

2) Ameingiza mamluki ya wachukua fomu ili waweze kuiba kura eneo la kuhesabia (CCM wananielewa staili yetu ya kuhesabu kura za maoni).

# Watu zaidi ya 70 wote ni mpango kazi wake na wamepanga kumzunguka wakati wa kuhesabu wamepanga kumzunguka wakati wa kuhesabu kumuongezea.

MY TAKE: HAPA PAANGALIWA.
NB: Wachukua fomu ambao ni mpango kazi wengi wanafahamika

Mjumbe wa Mkutano Mkuu Jimbo la Ukonga wa dhati.

Msalika A
 
Jimbo la wajanja hili au bado kuna watu wanaikubali ccm hapo mjini?
 
Ila huyu nyau wa slaa anasumbua watu na hela zake. Huku Kata ya Majohe tushasema CCM IKIMPITISHA TUTAMPA TENA MPINZANI KAMA 2015. Sababu anafanya haya mbele ya takukuru kisa aliwahi kuwa meya , mnec; kawashika ! Na tukimpa mpinzani sijui kama watarudisha tena jimbo .
CCM Oyee
 
Wauza mayai haohao unaowananga hapa ndio walibeba hilo jimbo 2015 kupitia kwa muuza mayai mwenzao Waitara.
Ambaye badae akawasalit kwa kupewa vipande vya hela na sasa kawakimbia kaenda kwa chuma Heche huko ataambulia kipigo cha mbwa koko.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom