Elections 2010 Jimbo la Ubungo: CCM kutoana macho mwaka huu

Tonge

JF-Expert Member
May 7, 2010
695
12
KWELI MWAKA WA UCHAGUZI UNA MAMBO YAKE.

JANA NIMEMSIKIA NAPE AKIELEZA NIA YAKE YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA UBUNGO HUKU AKIMPIGA VIJEMBE SHAMSA, NAPE ANAKUWA MWANACCM WA TATU (SHAMSA, ALFRED NCHIMBI NA NAPE) KUELEZA NIA YA KUGOMBEA JIMBO HILI PAMOJA NA MNYIKA WA CHADEMA. KAZI IPO MWAKA HUU, MWENYE JIMBO LAKE KEENJA KAKAA KIMYA LICHA YA KUSEMA TANGU MWANZO KUWA HAGOMBEI TENA.HIVI HAKUNA MAJIMBO MENGINE MPAKA MBANANE HAPO HAPO UBUNGO AU MAJIMBO YALIYOPO DAR?.HII INA NIDHIHIRISHIA WAZI KUWA ASILIMIA 95% YA WABUNGE WETU HUKAA DAR NA KUYAACHA MAJIMBO YAO YA MIKOANI WAZI.JE HAWA NI WABUNGE WA DAR AU MIKOANI? ONDOKENI BWANA MNATUZIDISHIA FOLENI NA MIGARI YENU YA KIFAHARI, NENDENI MAJIMBONI KWENU KUWATUMIKIA WALIOWACHAGUA.
:becky:
 
Kwa vile Mwangunga ni waziri, CCM haitamtosa, hivyo Nape na Nchimbi ni wasindikizaji tuu, na huo ndio mteremko wa Mnyika kujitwalia jimbo hili kiulaini kama anamsukuma mlevi. Angesimama Nape, JJ Mnyika angekuwa na kibarua kigumu, Nchimbi ni hakuna kitu pale. Kama CCM hili ninaloliona nayo inaliona, wakaamua kumsimisha Nape, then jimbo la Ubungo kazi ipo.
 
Mama Mwangunga angeenda tu Mpwapwa akawaachia hawa vijana wapambane hapa Ubungo.
 
Ntafurahi sana vijana wakipambana katika jimbo! Lakin swali moja kwa wanaJF hivi kweli hao wote waliotangaza nia hapo Ubungo wana uwezo wa kiliongoza. Kaenja alishindwa kabisa licha ya jimbo kuwa na kero nyingu. Je wote walitangaza wanawezaaa! Tuwajadili
 
Tukiacha nia zao za kugombea, je hao wote akina Nape, Shamsa, John, n.k...wanazo sifa za kuwawakilisha wana- Ubungo?
 
N-Handsome.....Sasa usipochafua vidole si ndo MAFISADI watachukua nchi Tena. Twende bwana kujiandikisha.
 
Binafsi namuunga mkono Nape, atleast ameweza kusimama na kuwapinga "wakuu" wa ndani ya chama chake, ni ujasiri wa kuungwa mkono.
 
Kwa vile Mwangunga ni waziri, CCM haitamtosa, hivyo Nape na Nchimbi ni wasindikizaji tuu, na huo ndio mteremko wa Mnyika kujitwalia jimbo hili kiulaini kama anamsukuma mlevi. Angesimama Nape, JJ Mnyika angekuwa na kibarua kigumu, Nchimbi ni hakuna kitu pale. Kama CCM hili ninaloliona nayo inaliona, wakaamua kumsimisha Nape, then jimbo la Ubungo kazi ipo.

Mbona hata 2005 Mnyika hakuwa na kazi kubwa. ccm wanafanya kila Hila, kuwashindisha wagombea wao.
 
John Mnyika jimbo ni lako!!! Tuombe Mungu ateuliwe Shamsa Magunga ili akusafishie njia.
 
KWELI MWAKA WA UCHAGUZI UNA MAMBO YAKE.

HIVI HAKUNA MAJIMBO MENGINE MPAKA MBANANE HAPO HAPO UBUNGO AU MAJIMBO YALIYOPO DAR?.HII INA NIDHIHIRISHIA WAZI KUWA ASILIMIA 95% YA WABUNGE WETU HUKAA DAR NA KUYAACHA MAJIMBO YAO YA MIKOANI WAZI.JE HAWA NI WABUNGE WA DAR AU MIKOANI? ONDOKENI BWANA MNATUZIDISHIA FOLENI NA MIGARI YENU YA KIFAHARI, NENDENI MAJIMBONI KWENU KUWATUMIKIA WALIOWACHAGUA.
:becky:

Mkuu kwani huko mikoani umeambiwa hakuna candidates? hao wanaishi na kufanya kazi zao Dar, maisha yao yako Dar sasa wewe unawambia wakagombaa meatu ili iweje? watakuwa wabunge wa Mpanda wenye shughuri binafsi na makazi Dar, unadhani kutakuwa na uwakilishi kwa sisi wa mikoani hapo?? Acha walioamua kuishi dar wabanane huko huko Dar
 
Kwa vile Mwangunga ni waziri, CCM haitamtosa, hivyo Nape na Nchimbi ni wasindikizaji tuu, na huo ndio mteremko wa Mnyika kujitwalia jimbo hili kiulaini kama anamsukuma mlevi. Angesimama Nape, JJ Mnyika angekuwa na kibarua kigumu, Nchimbi ni hakuna kitu pale. Kama CCM hili ninaloliona nayo inaliona, wakaamua kumsimisha Nape, then jimbo la Ubungo kazi ipo.


Yes Comrade. Najua Nape ana kazi nzito kupita ndani ya CCM.Hata hivyo,sioni kwa nini watu wanamwona Nape kama kijana Tishio sana.Namjua inside out na mojawapo ya weakness zake kisiasa ni 1......2.....3.....4....6.sitaki kuzitaja hapa kwa kuwa atajirekebisha,Najua kutokana na hizi weakness hataweza kupambana na John mnyika.Anybody can beat Nape Nnauye.Nataka CCM wampitishe ili iwe rahisi zaidi kwa Mnyika,ingawa naamini Mnyika hahitaji mtu legelege kulitwaa jimbo la Ubungo but nataka atumie resources chache Ubungo huku akizielekeza nyingine ktk kampeni general za Chama

Pia hii arrogance wanayoonyesha UVCCM,watashangaa na matokeo watakayopata.So far,katika kambi ya CCM,vijana wooote waliojitokeza kugombea,sijaona hata kijana mmoja tishio katika kujenga hoja au sera zaidi ya hoja dhaifu na kurudia sera za kawaida kabisa.Ni lazima uwe na ujasiri wa kujenga hoja,sera mpya na zenye nguvu kuliko waliotangulia.Unaposhindwa kutumia taaluma yako kuepuka siasa za kashfa,matusi ,na majungu na baadala yake ukaonyesha ustaarabu wa kisasa kidemokrasia,then you are doomed!

Nasema ubungo,Mnyika akipambana na Shamsi Mwangunga ndiyo kutakua na kazi kidogo ambayo sioni kama itamzuia mnyika kulishinda hilo jimbo.Kinachohitajika ni aggresive campaign
 
Ushindani mkali kama huo ndiyo utakaotoa sifa halisi za mgombea anayefaa. Mimi naona hii ni fursa nzuri wa wakazi wa jimbo la ubungo kupima uwezo wa uwakilishi na kujiridhisha kabla ya kufanya maamuzi.
 
Wanaubungo hawahitaji watu toka CCM, wapo hapo toka mwanzo na hakuna kinachoeleweka. Tatizo sio mtu hapa ni Chama kwa hiyo yoyote ndani ya CCM hakuna mabadiliko sio Ubungo tu hata Tanzania kwa ujumla wake.
 
As what i see bandugu, Nape is a good character ila tatizo mahala alipo ndio pabaya, na kama tujuavyo mwenyekiti halisi wa CCM bwana EL aligombana na Nape bse he was against ufisadi wa jengo la umoja wa vijana.
For this reason, he will not stand as candidate.
 
Back
Top Bottom