Kama ilivyokuwa kwa mkoa wa California mnamo mwaka jana sasa mambo si mambo viunga vya Texas ambapo mahitaji ya nishati ya umeme yamezidi ugavi, na miundombinu imeelemewa.
Watu wapatao milioni mbili wako gizani. Viongozi wa kisiasa na kijamii wamewaomba wakazi wa baadhi ya viunga vya mkoa huo, ikiwemo wilaya Harris na mji wake mkubwa wa Houston, wajifungie ndani maana nje si salama. Mstahiki Meya Slyveater Turner wa jiji la Houston amelitupia lawana shirika na ugavi wa umeme ERCOT lililotangaza mgao huo na kusema anataka majibu.
Mkuu wa Mkoa wa Texas bwana Greg Abbott amemuomba Rais Biden atangaze hali ya hatari na kuelekeza misaada mkoani humo.
CNN News
Washington Post
The Texas Tribune