Jimbo la Texas Nchini Marekani latangaza mgao wa umeme

Kwameh

JF-Expert Member
Dec 3, 2011
1,483
2,000
1613443622470.jpeg

Kama ilivyokuwa kwa mkoa wa California mnamo mwaka jana sasa mambo si mambo viunga vya Texas ambapo mahitaji ya nishati ya umeme yamezidi ugavi, na miundombinu imeelemewa.

Watu wapatao milioni mbili wako gizani. Viongozi wa kisiasa na kijamii wamewaomba wakazi wa baadhi ya viunga vya mkoa huo, ikiwemo wilaya Harris na mji wake mkubwa wa Houston, wajifungie ndani maana nje si salama. Mstahiki Meya Slyveater Turner wa jiji la Houston amelitupia lawana shirika na ugavi wa umeme ERCOT lililotangaza mgao huo na kusema anataka majibu.

Mkuu wa Mkoa wa Texas bwana Greg Abbott amemuomba Rais Biden atangaze hali ya hatari na kuelekeza misaada mkoani humo.

CNN News
Washington Post
The Texas Tribune
 
Root

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
39,542
2,000
Texas sio Mkoa, ni Jimbo la Pili kwa Ukubwa Marekani kwa Ukubwa wa Eneo na Wingi wa Watu.

Texas ndilo jimbo lenye kuzalisha umeme mwingi Marekani

Sababu ya Umeme kukatwa ni kutokana na hali ya hewa kuwa ya ubaridi mno kiasi cha kuathiri mifumo ya usafirishaji kwani baridi ni -22 C
Pia barafu imetanda kila mahali.

Texas ni Robo 3 ya Tanzania kwa eneo maana ina 695000km za mraba wakati Tanzania ni 98000km + za mraba

Ina watu 29mil ambayo asilimia 50 ya Tanzania.

Kipato kwa kila mtu ni zaidi ya Milioni 140.

Kuita Texas mkoa ni kosa kubwa mno.
 
Ollachuga Oc

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
15,139

Dah kosa kubwa sana aise.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom