Uchaguzi 2020 Jimbo la Musoma Mjini limetawaliwa na kelele za Mabomu na mizunguko ya FFU

Sigara Kali

JF-Expert Member
May 28, 2017
3,623
8,428
Tangu asubuhi jimbo la Musoma Mjini limetaliwa na kelele za Mabomu ya shabaha yanayofanywa na FFU mkoa wa Mara maeneo ya Kamnyonge/ Nyamatare.

Mida ya jioni nimeshuhudia askari wengi wa FFU wakiwa kwenye gari mbili huku wamevalia mavazi yao yaliyopambwa na Mabomu ya machozi wakiranda randa maeneo ya mjini Kati.

Je wanatishia wananchi wa Musoma mjini? Ambao wameonesha wazi hawamtaki mgombea wa CCM ndugu Mathayo na wanamhitaji wa moyo mmoja mgombea wa CHADEMA ndugu Mwita.

Nimepita maeneo ya kambi ya FFU pale Kamunyonge nimekuta gari la maji ya kuwasha linafanyiwa service,hii yote ni kukabiriana na raia wa Musoma ambao wameonesha wazi hawaitaki CCM hawamtaki Mathayo.

CCM acheni kung'ang'ania madaraka na kutumia vyombo vya dola mmbaki madarakani,mmeshachokwa mmekataliwa na wananchi.
 
Tangu asubuhi jimbo la Musoma Mjini limetaliwa na kelele za Mabomu ya shabaha yanayofanywa na FFU mkoa wa Mara maeneo ya Kamnyonge/Nyamatare...
Kapige kura acha ndoto zenu za kijiweni. Ukileta za kuleta utapimiwa fungu lako linalokutosha. Ina maana kazi huna we unatazama tu FFU au mara service mara nn, kwa hiyo unataka magari yasifanyiwe service au
 
Zanzibar ndio usiseme. Hali ni mbaya zaidi, wananchi wamechezea mabomu na risasi kama zote ila wananchi nao hawajakubali wakaanza kutumia mawe mpaka askari wakakimbia na kusahau mabomu yao mtaani.

Video na Picha msisahau kuzituma kwa "MABEBERU" ili wapate kila sababu ya kuwaburuza Mahakama Ya Jinai hawa wadudu wanao umiza raia.
 
Tangu asubuhi jimbo la Musoma Mjini limetaliwa na kelele za Mabomu ya shabaha yanayofanywa na FFU mkoa wa Mara maeneo ya Kamnyonge/Nyamatare...
Wako hapo kupambana na wanaotaka kulinda kura na kuingia barabarani pia kule Tarime wanakotaka kuleta mapigano ya koo kama ilivyokuwa miaka ya 80s nasikia wanataka pia kuleta maburuki toka nchi jirani.

Hivyo acha waendelee na kulinda amani yetu kama wewe unaogopa basi utakuwa mkosaji.
 
Wamepoteza ridhaa hao, Watu wanataka HAKI na MAENDELEO yao, wewe unapeleka POLISI na MABOMU yao
 
Tangu asubuhi jimbo la Musoma Mjini limetaliwa na kelele za Mabomu ya shabaha yanayofanywa na FFU mkoa wa Mara maeneo ya Kamnyonge/Nyamatare.

Mida ya jioni nimeshuhudia askari wengi wa FFU wakiwa kwenye gari mbili huku wamevalia mavazi yao yaliyopambwa na Mabomu ya machozi wakiranda randa maeneo ya mjini Kati.

Je wanatishia wananchi wa Musoma mjini? Ambao wameonesha wazi hawamtaki mgombea wa CCM ndugu Mathayo na wanamhitaji wa moyo mmoja mgombea wa CHADEMA ndugu Mwita.

Nimepita maeneo ya kambi ya FFU pale Kamunyonge nimekuta gari la maji ya kuwasha linafanyiwa service,hii yote ni kukabiriana na raia wa Musoma ambao wameonesha wazi hawaitaki CCM hawamtaki Mathayo.

CCM acheni kung'ang'ania madaraka na kutumia vyombo vya dola mmbaki madarakani,mmeshachokwa mmekataliwa na wananchi.
Wanatuongezea Morali TUMEDHAMIRIA ...is The Honorabo Prezidaa TL
 
Back
Top Bottom