Jimbo la Mlalo: Taarifa ya maendeleo toka Ofisi ya Mbunge

Popcon

Member
Aug 12, 2018
28
12
OFISI YA MBUNGE MLALO

SLP 32 .MLALO -LUSHOTO

TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI KWA KIPINDI CHA JANUARY -2018-DESEMBA-2018)

Ndugu wana Mlalo -Lushoto

Salaam,

Sifa Njema anastahili Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema.

Wakati Tuko kamilisha na kuaga mwaka 2018 ,na kuukaribisha Mwaka Mpya 2019 .

Ninayo heshima kubwa kutumia nafasi hii kuwashukuru kwa namna tulivyoshiriki Pamoja katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika Halimashauri Yetu na Jimboni letu.

Aidha kwa mara nyingine tena nitumie nafasi kutoa Pole kwa wale wote waliopoteza ndugu ,Jamaa na marafiki katika Ajali mbaya ya Barabarani iliyotokea Pale Kibaoni-Longoi Kata ya Rangwi ikihusisha Bus la Maqaadir linalofanya Safari zake kati ya Mtae na Tanga.(Mwenyezi Mungu aziweke Roho za Marehemu wote mahali stahili na inshallah ajaalie kuwaponya majeruhi wote)

Ndugu wana Mlalo

Pamoja na kuwa na mahitaji na matarajio tofauti kutoka kwenye vijiji vyote 78 na Kata zote 18 na vitongoji 599 bado tumekuwa Pamoja sana hasa kupitia ukurasa huu kubadilishana mawazo na kukumbushana ,kukosoa kwa njia za kistaarabu kwa mustakabali wa Maendeleo ya Jimbo letu.

Ndugu wana Mlalo

Kipekee ni washukuru sana wale wachache walioibua kero na hoja kupitia ukurusa huu na sisi Ofisi ya Mbunge tukazichukua na kuzishughulikia imekuwa ni jambo la faraja sana Kwetu na ni matumizi sahihi ya Mtandao.

Aidha kwa niaba ya wana Mlalo Wote nawashukuru sana wadau wetu wa Maendeleo (Friends of Rashid Shangazi) Ambao kwa kiasi kikubwa wamefanikisha shughuli mbalimbali za Maendeleo kwa uchache niwataje-
-Mission Possible UK🇬🇧 Uingereza
-Malaysian Humantarian Aid
-Islamic Help of Tanzania 🇹🇿
-The Bilal Muslim Mission of Tanzania
-Beta Charitable Trust Uk 🇬🇧
-Tulia Trust ya Tanzania 🇹🇿
-Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania 🇹🇿 Dkms
-Essex United Kingdom 🇬🇧
Kwa kiasi kikubwa walivyosaidia kusukuma miradi mbalimbali Jimboni.

Aidha nawashukuru Sana wenyeviti na watendaji wote wa vijiji ,na watendaji wa Kata Pamoja na,Waheshimiwa Madiwani,

Wataalaam wote wa Idara mbalimbali wa Halimashauri yetu ya Wilaya ,Serikali kwa Ujumla,bila wao Mipango Yetu isingeweza kutekelezeka kwa ufanisi weledi na umakini mkubwa.

Kipekee Pia tunashukuru Mchango mkubwa wa Chama cha Mapinduzi kwa usimamizi na ufuatiliaji wa utekelezaji wa ilani Yetu.

Ndugu wana Mlalo.

SEKTA YA ELIMU.

Elimu ya msingi na sekondari imeendelea kuwekewa mkazo kuhakikisha hali ya ufaulu na ubora wa elimu unaongezeka. Bado tunaendelea na ujenzi wa maabara za Sayansi kwa kila sekondari Lakini baadhi ya maeneo zipo ktk hatua ya usafi. Zipo baadhi ya Kata zina sekondari zaidi 2-3-4 hivyo imekuwa ni mzigo mkubwa kiasi ,Lakini tunapambana kuhakikisha tunawaunga mkono.

Pia vipo vijiji ambavyo vimeanzisha miradi ya shule nyingine za msingi kutokana na kupanuka na kukua kwa vijiji husika na kuongezeka kwa idadi ya watoto wanaoandikishwa.

Aidha katika kuunga mkono juhudi za Serikali ktk kuiboresha Elimu mwezi Agosti mwaka huu tumekarabati Madarasa mawili katika Shule ya Msingi Maito, Kata ya Shaghayu na kujenga vyoo vya wanafunzi matundu 12 na mfumo mdogo Wa maji, mradi uliogharimu fedha za kitanzania zaidi ya Shilingi milioni kumi na tano.(15,000,000x/-)
Mradi huu utekelezaji wake ni kwa kushirikiana na Taasisi rafiki ya Mission Possible kutoka Uingereza Uk 🇬🇧 toka Nchi ya Uingereza.

Miradi ya madarasa ya Awali na Shule chipukizi (satellites)

1-Mkundi Mtae-tumechangia mifuko 20 na mbao za kupaulia.(limekamilika)

2-Kisima-(Lunguza), Bati 40 na Saruji mifuko 60(limeezekwa)

3-Manyunyu -(Mbaramo) Liko ktk
hatua za Kuezekwa ambapo tayari Sisi ofisi Ya Mbunge tumeshachangia Mifuko 40 ya Saruji na Bati 120, kwa ajili ya kazi kuezeka.

4-Kishumai-Mifuko 40 ya Saruji rola 4 za Maji (Mng'aro) lipo katika hatua za usafi

5- Mlesa/Kasanga (Malindi) maandalizi

6-Kwefivi- mifuko 20 ya Saruji (Mwangoi) limekamilika.

7. Ngwalu Kitivo-liko hatua za uezekaji, ambapo tayari tumeshawapatia mifuko 40 ya saruji kwa ajili ya kumalizia ujenzi hatua ya boma.

8-kuongeza Chumba cha Darasa Shule ya Msingi Nkunkai -Mifuko 30 ya Saruji.

9-Mifuko 30 ya Saruji-Ujenzi vyumba vitatu vya madarasa Shule ya Msingi Hamboyo -Manolo

10-Mifuko 20 ya Saruji-Ujenzi wa vyumba vya madarasa Shule Ya Msingi Lokome-Manolo

11-Uboreshaji Miundo Mbinu ya madarasa Shule ya Msingi Futii-Mtae-tumekabidhi mifuko 35 ya Saruji.

12- Uboreshaji Miundo Mbinu ya Darasa Kifulio Shule ya Msingi Pamoja na vifaa (7,500,000/-)

13-Ujenzi Chumba cha Darasa Shule ya Msingi lewa-Mwangoi

14-Mradi wa Ujenzi Nyumba ya walimu Madala Shule ya Msingi-Manolo-Mifuko 20 Saruji.

15-Mradi wa Ujenzi vyumba vya madarasa Shule ya Msingi Rangwi
Idara ya Sekondari -mifuko 50 ya Saruji.

16-Ujenzi wa shule chipukizi Mwendala-Madala -Manolo tumekabidhi bati 46

IDARA YA SEKONDARI

1-Uboreshaji Miundo mbinu ya madarasa Chambogo Sekondary -Mbaru-Mifuko 40 ya Saruji

2–Uboreshaji wa Maabara za sayansi Shume Sekondari -Manolo(mifuko 20 ya Saruji roli tatu za mchanga)

3-Uboreshaji wa Miundo mbinu ya madarasa Mizai Sekondari -Shume(mifuko 20 ya Saruji)

4-Uboreshaji wa Miundo mbinu ya madarasa Kisaba Sekondari -Kwemshasha .Tumekabidhi Saruji mifuko 50.

5-Uboreshaji wa Miundo mbinu ya madarasa Mavumo Sekondari -Shume -Saruji mifuko 20

6-Mradi Ujenzi wa Hostel Mnazi Sekondary hatua za awali.-Mnazi(kwa kuanza tumetenga saruji mifuko 30)

7-Ukamilishaji wa Miundo Mbinu Maabara za sayansi-Kwemaramba Sekondari-DuleM(vifaa vyenye thamani ya shilingi Milioni mbili .

8-Uboreshaji Miundo Mbinu ya madarasa Rangwi Sekondari mifuko 100 ya Saruji.

9- Uboreshaji wa vyumba vya madarasa Mtae Sekondari -Mtae (tumekabidhi Saruji mifuko 20)

Ndugu wana Mlalo

AFYA HUDUMA ZA MACHO

Kwa ushirikiano wa Taasisi ya Beta Trust na The Bilal Muslim mission of Tanzania 🇹🇿 .
Zaidi ya Wananchi 1900 kutoka Maeneo mbalimbali walinufaika na huduma hii ikihusisha uchunguzi,utoaji Dawa,utoaji miwani Pamoja na upasuaji wa Mtoto wa Jicho (cataract)
Zoezi hili limegharimu zaidi ya Milioni Mia tatu na upasuaji wa Mtoto wa Jicho kwa watu 117 huku 586 walipata miwani Bure

SEKTA YA AFYA UJENZI

Huduma za Afya hasa kwenye Kituo cha-Mlalo ambacho kwa sasa ndio kituo Pekee kinachofanya Upasuaji Jimboni.

Wagonjwa wameendelea kupata huduma za awali na za kati kimsingi tumepunguza kwa kiasi kikubwa safari za kupeleka wagonjwa Lushoto katika Hospital ya Wilaya.

Aidha tumeweza kununua Ultrasound katika kituo hiki kwa mwaka 2018 ambapo, Ultrasound itatumika hasa katika kuimarisha huduma za upasuaji na huduma zingine za Kitabibu katika Kituo hiki.

Mradi wa wodi ya Mama na Mtoto unaendelea vizuri na kwa sasa upo katika hatua ya Usafi, aidha tumejenga Chumba Cha Maabara katika Kituo hiki ambacho kwasasa pia kipo katika hatua ya Usafi.

Kituo cha Afya-Mnazi.

Tumeweza kufanya upanuzi na kuboresha Miundo Mbinu ya Kituo cha Afya Mnazi kwa kujenga Majengo ya Wardi za wagonjwa Wa aina zote, Nyumba ya watumishi, Chumba cha Kuhifadhia maiti na Chumba Cha Upasuaji, ikiwa ni mradi Wa fedha toka Serikali kuu zaidi ya Shilingi milioni mia nne( 400,000,000/-).

Ambapo hadi Sasa mradi umefikia Asilimia 60%.
Kukamilika kwa mradi huu itapunguza kama sio kuondoa kabisa safari za wagonjwa kuifuata huduma ya upasuaji na huduma zingine katika hospitali ya Wilaya ya Lushoto na Wilaya jirani ya Same.

Kituo cha Afya Kangagai-Mwangoi

Tumefanya upanuzi na kuboresha Miundo Mbinu ya Kituo cha Afya Kangagai kwa kujenga majengo ya wardi za Wagonjwa wa aina zote,
Nyumba ya watumishi na Chumba cha Kuhifadhia maiti,
Mradi huu umefikia Asilimia 80% ya kukamilika ikiwa ni fedha zaidi ya Shilingi milioni mia Tano toka Serikali kuu (500,000,0000/-)
Kukamilika kwa mradi huu kutaimarisha upatikanaji wa huduma ya Afya kwa wakazi wa Mwangoi na Kata jirani ikiwemo, Hemtoye,Malindi, Lukozi, Dule-M ,Rangwi Sunga na hata Mlalo.

KATA YA MNG'ARO.

Tumefanya upanuzi wa Zahanati ya Mng'aro kwa kujenga wardi, lengo likiwa kupandisha hadhi kuwa kituo cha Afya hapo baadae, tayari Jengo limeshapauliwa na Ofisi ya Mbunge imeshachangia Bati 120 zilizoezeka Jengo hilo.

KATA YA MTAE

Ahadi ya Serikali ya awamu ya Tano ni kujenga Kituo cha Afya katika Tarafa hii ya Mtae kwa Mwaka wa Fedha unaoendelea.
Nawashukuru sana wananchi wa Mtae kwa kujitoa na kuandaa uwanja wa katika eneo la mradi.

KATA YA MANOLO NA MALINDI

Utekelezaji wa Ujenzi wa Kituo cha Afya kila Kata unatulazimu kuwa na Mpango madhubuti wa kuipandisha hadhi Zahanati za Manolo na Malindi ili ziweze kuwa kwenye Mpango wa maboresho kuzipandisha hadhi kuwa vituo kamili vya Afya.

Aidha kwa Mwaka huu tumefanikiwa kufungua zahanati zifuatazo.

1-Hambalawei kata ya Shume
2-Tema Kata ya Mbaru
3-Mphanga Kata ya Shaghayu
4-Nywelo Kata ya Manolo
5-Mgwashi Kata ya Lukozi
6-Zimbiri Kata ya Mbaramo
7-Mkunki Kata ya Manolo

Zahanati zilizopo katika hatua za Usafi kuelekea kukamilika.
1-Mtii Kata ya Mtae
2-Kibandai Kata ya Kwemshasha
3-Hemtoye Kata ya Hemtoye
4-Kinko Kata ya Lukozi
5-Baghai Kata ya Mlalo
6-Kalumere Kata ya Mbaru.

Miradi ya sekta ya Afya iliyoko kwenye hatua mbalimbali za Ujenzi.

1-Kwekifinyu-(Kata ya Hemtoye)Saruji Mifuko 20

2-Mangika (Kata ya Hemtoye)Mifuko ya Saruji 20

3-Kiranga (Kata ya Rangwi)Saruji mifuko 30

4-Nkelei (Kata ya Rangwi)hatua za awali.

5-Dule Juu (Kata ya Dule)Mifuko 20 ya Saruji

6.Kishangazi(Kata ya Shagayu).Mifuko ya Saruji 20

7- Lunguza (Hatua za kupandisha Boma)zaidi ya mifuko 50 na rola za Maji na Shilingi laki tao kwa ajili ya Fundi (500,000/-).

8-Sunga (Ujenzi wa Ward)mifuko 80 ya Saruji

9-Mng'aro (Ujenzi wa Ward)Saruji 60 na bati 120

10- Kwekangaga Ndabwa -Lukozi (Zahanati)hatua za awali.

11-Nkhombo(Mbaramo) hatua za kupandisha Boma- Mifuko 40 ya Saruji

12-Viti -zahanati(Hatua za kupandisha Boma )mifuko 50 ya Saruji.

13-Langoni Kata ya Mnazi hatua za awali

14-Rangwi Ujenzi wa Ward.Tumekabidhi Saruji mifuko 30 na mifuko 20 ukarabati wa Zahanati ya Rangwi.

Ndugu wana Mlalo

KILIMO NA MIFUGO

Dhamira Yetu ni kukuza uzalishaji wa zao la Pamba ambalo limeonekana kuwa mbadala wa mazao ya biashara katika Tarafa ya Umba. Kwa Mwaka huu Pekee Kata ya Lunguza inatarajia kuvuna zaidi ya kilo laki Moja.

Pia msukumo utaongezeka kuhamasisha wananchi kupanda tena zao la Kahawa haswa Maeneo ya Milima kwani Sasa Mazingira yake ya kibiashara na masoko yanazidi kuboreshwa.

MIFEREJI YA UMWAGILIAJI KITUANI MWEZAE NA KWEMGIRITI.

Kazi ya Ujenzi Wa Mifereji Miwili ya Kituani Mwezae na Kwemgiriti inaendelea, Mradi huu unajengwa kupitia wizara ya Maji na Umwagiliaji na Zaidi ya Shilingi Milioni mia tisa za Kitanzania zitatumika kukamilisha mradi .
Mradi huu unakusudiwa kuongeza uzalishaji katika kilimo kupitia umwagiliaji kwa Kwa Wakazi Wa Kata ya Lunguza na Kata Jirani.

Aidha kwa upande wa sekta ya Ufugaji tumejenga Josho kwa ajili ya mifugo katika eneo la Antakaye Kijiji cha Kivingo ,Pamoja na lambo la kunyweshea mifugo ,dhumuni letu ni kukarabati Josho na birika lingine lililoko katika Kijiji cha Mkundi Mtae hali ya kifedha itakapo ruhusu.

Ndugu wana Mlalo

MIUNDOMBINU YA BARABARA

Barabara zetu zinazounganisha Jimbo letu na Maeneo jirani haswa zile TANROADS msimamo wetu upo kuisukuma Serikali na kuhakikisha zinatengeneza kwa kiwango cha Lami- Tunashukuru Naibu Waziri wa Uchukuzi na mawasiliano alitembelea Barabara hii kuanzia Wilaya ya Mkinga-Maramba hadi Magamba Lushoto.

Kupitia Mngaro-Mlalo -Lukozi Pamoja na Barabara zote zilizopo chini ya uwakala wa Tanroads.

1-Magamba-Lukozi- Makose-Mtae
2-Magamba-Lukozi-Manolo-Mtae
3-Magamba-Lukozi-Mlalo
4-Maramba-Kikumbi-Lunguza-Mnazi mpaka Mkomazi
5-Maramba-Kikumbi-Mngaro hadi Mlalo.

Kwa hiyo Pamoja na Kwamba kwa sasa zinapitika lakini malengo yetu nikupigania kuwekwa lami ili kurahisisha usafiri na usafirishaji na suala hili tumelipa msukumo mkubwa na Serikali inalifanyia kazi haswa utafutaji wa Fedha.

Aidha Ujenzi wa daraja jipya kubwa limekamilika pale Lukozi baada ya lile la awali la culvert kushindwa kuhimili wingi wa Maji haswa nyakati za masika.

Ndugu wana Mlalo.

BARABARA ZA TARURA.

Mnazi -Kwenda Mtae nayo ni muhimu na ni Barabara ya kihistoria kwa kuwa Sasa Mamlaka ya Barabara vijijini TARURA Iimeanza rasmi kazi tunaamini huu ndio muaraobaini wake Lakini pia kuwashirika na wadau wengine wakiwepo MIVARF na ROAD FUND.

Mtae-Mphanga-Kweshindo-Kishangazi hadi Mnazi tutongeza msukumo kwenye bajeti ijayo ili Barabara ikamilishwe kama ilivyokusudiwa kuunganisha kata 4 za Mtae-Shaghayu-Mbaramo na Mnazi.

Mlalo-Ngwelo-Makanya Mlola
Hii nayo ni muhimu sana kwa kuwa ni kiunganishi kizuri cha Lushoto/Bumbuli na Korogwe .

Aidha Upasuaji wa Mawe 360 Barabara ya Baghai -Tewe umekamilika lengo ni kuhakikisha Barabara hii inapitika ili kurahisisha mawasiliano kwa wakazi wa Maeneo haya, na kuziunganisha kata za Mlalo-Lunguza-Mbaramo- Shaghayu -Mtae.

Tumeweza kutengeneza Barabara ya Mlalo-Mgwashi-Dule Juu-Kibomboi hadi Emao Kata ya Rangwi kupitia TARURA, na kwasasa barabara hii inapitika na imerahisisha usafiri katika eneo hili linalounganisha Tarafa za Mlalo na Mtae.

Hekicho-Kwekanda-Lugurua

Hii ni barabara muhimu sana kiuchumi Kwa sasa kwani inaunganisha Jimbo letu na wilaya za Same na Korogwe tunakwenda kuipa msukumo mpya hasa baada ya TARURA kukabidhiwa jukumu hili.Barabara hii pia imeingizwa katika circuit ya kukuza utalii ili kuunganisha Hifadhi ya Mkomazi na Maeneo ya ukanda wa Juu Kiutalii taratibu nyingine bado zina endelea.

Kwa Mwaka huu wa Fedha utekelezaji wa kutengeneza Barabara ya Manolo-Madala-Mamboleo hadi Mambo Kilometers 14 umekamilika na Mkandarasi ataingia kazini muda wowote kuanzia January 2019.

Tumekarabati barabara ya
Mnadani -Zigha -Mziaghembe-Kwekanga, japo kipo kipande kidogo cha zaidi ya mita kilomita Moja hakijakamika lakini, tunaimani kipande hiki cha kuanzia mnadani-Darajani kitatengezwa hivi Karibuni ili kuondoa usumbufu uliopo katika eneo hili.

Nyasa-Hemtoye-Msale-Kwekanga pia tunaenda kutia msukumo ili iweze Kutengenezwa mwaka huu wa fedha.

Barabara nyingine zote zilizobaki zimehamishiwa wakala wa Barabara vijijini

Ndugu wana Mlalo

UPATIKANAJI WA MAJI

Tumeweza kuboresha mfumo wa upatikanaji Wa Maji katika Mradi Wa MAJI-MLALOWASSO unaohudumia Kata NNE za Kwemshasha,Mlalo,Mwangoi na Dule-M na jumla ya Vijiji kumi na moja(11).
Ambapo Maji yanapatikana kwa masaa Yote 24 kwa siku.

Aidha katika Kipindi cha Januari-2018 hadi Desemba-2018 tumeweza kujenga miradi midogo
mbalimbali ya Maji kwa kushirikiana na Wahisani wa maendeleo.(Friends of Rashid Shangazi)

Tumejenga Visima vya kina kifupi (HandPamps) zaidi ya 40-zenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni mia moja na Ishirini( 120,000,000/- )
kwenye
1-Kata ya Hemtoye -8
2-Kata ya Malindi, -vitongoji -5
3-Kata ya Mwangoi,-3
4-Kata ya Rangwi, -6
5-Kata ya Sunga, -5
6-Kata ya Kwemshasha vitongoji-5
7-Kata ya Lukozi, -vitongoji -2
8-Kata ya Mbaru-vitongoji-3

vijiji Vilivyonufaika na Mradi huu ni Mnadani 3, Sunga3, Kwemtindi 01, Nkukai 1, Makose 01,Hemtoye 02, Zaizo 1, Mwangoi 2, Kifulio 01, Mhelo 01 Kibandai 1, Nkelei-2, Emao-3, Maringo 1, 01 ,Ndabwa 01 Majulai 02 ,Butui 01, Kinko 01 na Kwekifinyu 5, Msale 2, Nyasa 2 na Masereka Mbaru-3

ZINGATIO:- Ujenzi umeanza Desemba ktk vijiji vya Nyasa, Maringo na Kwekifinyu pamoja na Emao...na umekamilika mwezi Decemba pia kwa baadhi ya pamp.
Aidha zaidi ya Pampu 15 zimejengwa katika Kata ya Mnazi katika kipindi cha Novemba-Desemba 2018...na huduma inatumika.

Aidha Tumejenga Matanki na miradi midogo ya Maji ktk Vijiji vya Zaizo-Hemtoye,Mgwashi- Mlalo, Dule Juu-Dule M, Majulai-Mwangoi na Nyasa-Kwemshasha.

Vile vile mumeendelea kuchangia rola ktk ujenzi wa miundombinu ya Maji ktk vijiji vifuatavyo:-

Zimbiri-Mbaramo-05
Tewe-Lunguza-08
Lunguza-Lunguza-05
Baghai-Mlalo -13
Zaizo-Hemtoye -13
Bungoi-Mlalo- 14
Majulai-Mwangoi-08
Mphonde-Shagayu-07
Mwambangoo-Malindi-05
Mbokoi-Kwemshasha-23-Nyasa)
Kishumai-Mng'aro-04
Nkhombo Mbaramo-09

Vile vile tunaendelea na zoezi la kutafuta wahisani kushirikiana nao kuchimba visima virefu katika vijiji vya Mkundi Mbaru/Mkundi Mtae Kata ya Mnazi na kitongoji cha Ngwalu Mazinde -Mng'aro Eneo la Magereza.
Na Mradi huu unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Ujenzi wa mradi mkubwa Gologolo-Nywelo-Mkunki-Manolo na Madala unaendelea vizuri kwa kukamilika ujenzi Wa vituo vyote vya kuchotea maji, Matanki na Utandikaji bomba kwa sehemu kubwa, aidha tayari baadhi ya maeneo wameshaanza kutumia Maji ya mradi huu ikiwemo kijiji cha Nywelo na kitongoji cha Lokome.

Hatua iliyobaki inahusisha upatikanaji wa Fedha kutoka Hazina na jitihada zina endelea ili kukamilisha Mradi huu.

KATA YA MBARU

Mabwawa ya Mbokoboko na Makeyui pia yatazalisha maji kwa kuyahifadhi ya Mvua na chemchem, kwani tayari Bwawa la Mbokoboko limekamilika, na hivyo kupunguza adha ya maji katika baadhi ya vijiji vya Kata ya Mbaru, ikiwemo Masereka na Mamboleo.

Lengo ni kutoa Huduma za maji safi kwa wakazi wa Masereka ,Kwemtindi,Tema,Mbaru Chambogo na Mkundi Mtae & Mkundi Mbaru -Mnazi

Ndugu wana Mlalo

BIASHARA NA MASOKO.

Tumeendelea kukazia upatikanaji wa soko la mbogamboga kwa kuweka miundo mbinu wezeshi kupitia Halimashauri na baraza la Taifa uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Kituo cha kuongeza thamani ya Mazao(Post harvest station) Kilichopo Kata ya Malindi, tayari kimefunguliwa na WAZIRI Mkuu Wa Tanzania Mh, Kasim Majaliwa, Majaliwa (Mbunge)mapema mwishoni mwa mwezi Oktoba, zipo taratibu ndogo ndogo za kukamilisha ikiwemo uudaji Wa bodi ili Kituo hiki kianze kazi Iliyokusudiwa.

Tumeendelea kupigania haki ya wakulima kwa kutokomeza kabisa ufungaji wa mazao kwa mtindo wa Lumbesa na kuna mafanikio ya kutosha. Changamoto liliyopo ni kukosa ushirikiano haswa kutoka kwa viongozi wa vitongoji na vijiji ambako mazao haya ndio hutokea kwenda kwenye Magulio na Masoko.

SHAMBA LA KATANI MNAZI

Muwekezaji Mpya anaendelea na shughuli za upandaji,uzalishaji na uchakataji wa Mkonge.
Kurejea kwa shughuli hizi kumeboresha kiasi kikubwa uchumi wa wananchi wa Tarafa ya Umba na kujenga mahusiano mapya ikiwa ni Pamoja na kutengeneza Ajira zinakadiriwa kufika 300 .

Ndugu wana Mlalo

UMEME VIJIJINI.

REA awamu ya tatu inakuja kusambaza umeme Maeneo yaliyosalia katika Jimbo la Mlalo, katika kipindi cha Miezi 36 ijayo ,Kufikia Mwaka 2020-2021
Jimbo letu na Tanzania kwa Ujumla litakuwa na Umeme na kimsingi ndio Mwisho wa miradi ya REA.
Tayari kwasasa mradi huu unaendelea Vijiji vya Nkelei-Rangwi, Ngazi-Mlalo na Handei- Dule-M,Mgwashi-Lukozi,Emao Rangwi na Mizai Shume
Tunawaomba wananchi wasubiri ili changamoto za kibajeti zikitengemaa miradi hii itaanza kwa kasi kubwa zaidi.
Mbaramo,Shaghayu ,Mbaru na Hemtoye(Kata hizi hazina umeme kabisa)zitazingatiwa na maeneo mengine yaliyosalia ya vijiji na vitongoji vilivyosajiliwa kwa mujibu wa sheria.

Hata hivyo tumeweza kugawa Solar panel kwa kaya za wazee na wajane katika Kata ya Shaghayu ambapo Kaya 30 zilinufaika.

HITIMISHO

Yapo yaliyofanikiwa kwa kiasi kikubwa na yapo yanayo onekana kwa macho na yapo pia yasiyo onekana kwa macho .

Utekelezaji wa ilani/manifesto ni miaka mitano hivyo tupeane muda tuongeze ushirikiano na ushiriki wa kujitolea ktk kuijenga Mlalo .

Nawashukuru wana Mlalo Wote kwa kuniamini na Kuniunga mkono ,changamoto zilizopo tuzikabiri kwa Pamoja na wala zisiwe kikwazo kwa maendeleo Yetu.

Nawatakia ,Wote Kwa Pamoja "

HERI YA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA 2019 UWE WA NEEMA NA MAFANIKIO KWETU SOTE

Rashid Shangazi
Mbunge Jimbo la Mlalo.
 
Taarifa ya kila mwaka ipo. Tembelea Ukurasa Wa Rashid Shangazi na Mlalo Tutakayo,#FB...utaona kila kitu.
 
Mbona hayo maendeleo hayaendani muda wa kuongoza Jimbo?? Miaka zaidi ya 50 maendeleo ya kusuasua!!
 
Hicho kijiji cha masereka mbona kinapitiwa mbali na miradi mingi? Hakuna maji wala umeme, au mnapendelea vijiji vyenye wasambaa wengi mnakipuuza hicho chenye wapare?
 
Hicho kijiji cha masereka mbona kinapitiwa mbali na miradi mingi? Hakuna maji wala umeme, au mnapendelea vijiji vyenye wasambaa wengi mnakipuuza hicho chenye wapare?
Tindo, Masereka kuna Visima vipya, 3 kisuwani,Masereka shule, na Chambogo Sekondari...wewe unaongelea Masereka IPI?
 
Taarifa ya kila mwaka ipo. Tembelea Ukurasa Wa Rashid Shangazi na Mlalo Tutakayo,#FB...utaona kila kitu

Mbunge naona unapendelea vijiji vya wasambaa wenzako unaviruka vijiji vya wapare. Maendeleo hayana kabila lakini nakuona wazi ukabila wako.
 
Tindo, Masereka kuna Visima vipya, 3 kisuwani,Masereka shule, na Chambogo Sekondari...wewe unaongelea Masereka IPI?

Masereka hapa juu hakuna maji mpaka watu washuke bondeni shule ya msingi masereka. Hapo maserek hakuna umeme japo umepita kwenda Ludende, Mtae nk. Au kwakuwa kijiji hicho kimejaa wapare? Nilikuwa hapo mwezi wa tisa, hizo adha nimeziona kwa macho.
 
Mbunge naona unapendelea vijiji vya wasambaa wenzako unaviruka vijiji vya wapare. Maendeleo hayana kabila lakini nakuona wazi ukabila wako.
Mbona huongei kapendelea wapi...maana Masereka kajenga visima 3 milioni 9, Kajenga Bwawa LA Mbokoboko Milioni 10, Katoa Mifuko 40 Ujenzi Chambogo Sekondari, Katoa mifuko 30 ujenzi Wa ofisi ya Kata pale Masereka, sasa upendeleo unaouongea NI UPI? Fafanua
 
H
Masereka hapa juu hakuna maji mpaka watu washuke bondeni shule ya msingi masereka. Hapo maserek hakuna umeme japo umepita kwenda Ludende, Mtae nk. Au kwakuwa kijiji hicho kimejaa wapare? Nilikuwa hapo mwezi wa tisa, hizo adha nimeziona kwa macho.
Hata hakuna chanzo, yawepo? Hujui Shule ndo bondeni ndo yanapatikana?
 
Mbona huongei kapendelea wapi...maana Masereka kajenga visima 3 milioni 9, Kajenga Bwawa LA Mbokoboko Milioni 10, Katoa Mifuko 40 Ujenzi Chambogo Sekondari, Katoa mifuko 30 ujenzi Wa ofisi ya Kata pale Masereka, sasa upendeleo unaouongea NI UPI? Fafanua

Nimekaa hapo masereka mwezi wa tisa, nilikuwa nanunua maji toka kwa vijana wa bodaboda. Kila baada ya siku 2 nilikuwa nanunua maji ya shilingi 5,000. Hakuna umeme ila umepita umeme mkubwa kwenda Mtae kwa wasambaa. Acha hizo mbunge.
 
Una mpango gani wa kumalizia maabara ya shule ya sekondari ya Rangwi? Inaonekana dhahili kuwa wananchi pumzi imekata
 
Nimekaa hapo masereka mwezi wa tisa, nilikuwa nanunua maji toka kwa vijana wa bodaboda. Kila baada ya siku 2 nilikuwa nanunua maji ya shilingi 5,000. Hakuna umeme ila umepita umeme mkubwa kwenda Mtae kwa wasambaa. Acha hizo mbunge.
Kama una umri na uelewa mzuri, umeme ulienda MTAE kipindi cha MBUNGE alopita, ila ninawasiwasi wewe bado unajua hata Tz Raisi ni Nyerere
 
H

Hata hakuna chanzo, yawepo? Hujui Shule ndo bondeni ndo yanapatikana?

Huo sio utetezi wa kiufundi eti hakuna chanzo!. hapo bondeni shule ya masereka maji yapo miaka na miaka toka niko mtoto. Nimetembea sehemu kibao nchi hii isiyo na vyanzo vya na maji yapo itakuwa hapo masereka? Acha hizo kaka, upendeleo haulipi. Kwenye kura unaongea maneno mengi, ikifika utekelezaji unaanza usanii eti hakuna chanzo.
 
Mimi
Una mpango gani wa kumalizia maabara ya shule ya sekondari ya Rangwi? Inaonekana dhahili kuwa wananchi pumzi imekata
Mimi nilivyokopi hiyo taarifa na kuipaste, nimeisoma vzuri ...naona MBUNGE amepiga tafu sana hiyo shule, na kwakuwa ni mdau...naamini akiona hii post ataongea kitu
 
Huo sio utetezi wa kiufundi eti hakuna chanzo!. hapo bondeni shule ya masereka maji yapo miaka na miaka toka niko mtoto. Nimetembea sehemu kibao nchi hii isiyo na vyanzo vya na maji yapo itakuwa hapo masereka? Acha hizo kaka, upendeleo haulipi. Kwenye kura unaongea maneno mengi, ikifika utekelezaji unaanza usanii eti hakuna chanzo.
Inaonekana wewe bado ni mchanga wa kuelewa na unaamini unaongea na MBUNGE. Wacha nikuache uendelee kulaum tu,ila mengi yamefanyika Masereka, soma post usikimbilie kulaum tu
 
Kama una umri na uelewa mzuri, umeme ulienda MTAE kipindi cha MBUNGE alopita, ila ninawasiwasi wewe bado unajua hata Tz Raisi ni Nyerere

Kama mwenzako kapitisha umeme, ww. Umekushinda nini kuushushisha hapo masereka? Au napo utasema hamna chanzo kama maji?
 
Back
Top Bottom