Jimbo la Mh Matayo (Same) na madini yanayopelekwa Kenya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jimbo la Mh Matayo (Same) na madini yanayopelekwa Kenya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mahoza, Apr 23, 2012.

 1. m

  mahoza JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 1,242
  Likes Received: 411
  Trophy Points: 180
  Wana JF naomba niwasilishe ombi kwa makamanda wasaidie kuchunguza mradi wa madini yanayotolewa Mbaga wilsya ya Same vie kijiji cha Mwembe kupelekwa Kenya.

  Kwa miaka mingi zaidi ya mitano kuna huo mradi lakini wananchi hawajafaidika na chochote kila leo milori inakuja kuchukua hayo madini. Makamanda huo mradi ni wanani na kwanini wanavijiji wamefungwa midomo. Huyo mtu ambaye anaambiwa ni mradi wake anaitwa Wille ( ndio jina linajulikana kwa wanakijiji). Naomba hili lifuatiliwe ukiyaona hayo maloro kwa mkupuo yanaweza yakaja mapya saba ukiweka na yazamani! Jamani chinde wasaidieni wapare wamelala..

  Ni ombi wakuu.
   
 2. s

  simon james JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 283
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kile tunachokiita vuguvugu la mabadiliko Jumapili tar 29/04/ 2012 sa 8 mchana kutakuwa na mkutano Mkubwa katika Kitongoji cha Nkwini kata ya makanya wilaya ya Same ambapo watasimikwa mabalozi wa CHADEMA na baadaye wananchi wanataratjiwa kutoa maoni juu ya mashamba yao ya Mabono waliyonyang'anywa na kupewa mwekezaji huku diwani na Mbuge wakionyesha dhahiri kukataa kushughulikia matatizo hayo. Kwa wapenzi wa CHADEMA na Viongozi Wanaofurahia harakati hizi huku vijijini hasa wilaya ya Same. Tunaomba mtusaidie Bendera 50 na kadi 500 kwaajili ya kazi hii kwani uongozi wa CHADEMA wilaya na mkoa tumewasiliana nao na wamesema hawana kadi na bendera wanasubiria hadi watakapo pewa toka makao makuu. Kwa kiongozi au mwanaharakati mwenye vifaa hiv tuwasiliame 0788177315 kabla ya siku kufika
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  haya madini ndio yale yanayochimbwa kwenye msitu wa shengena? huo msitu na ule msitu ni hifadhi ya taifa..sasa sijui nani alitoa kibali cha kuchimba madini kwenye hifadhi ya taifa
   
 4. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #4
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hii nchi ni wapi hakuna madini!! Hii nchi ni wapi hakuna vilio vya wananchi kudhulumiwa madini yao! Ni nchi gani hapa duniania haijafaidi madini ya Tanzania kwa bei ya bure kupitia kwa Wabunge na Mawaziri Wa Tanzania ..wanaotarajiwa kujiuzulu rasmi Leo?????!!!
   
 5. m

  mahoza JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 1,242
  Likes Received: 411
  Trophy Points: 180
  Nadhani ndo hukohuko ila kwa nini wananchi hawafaidiki? Huyo Wille ni nani na kwa niaba ya nani na kibali kutoka wapi? Sanasana m/ kiti kapewa sukari ila wanakijiji hamna kitu ni avae du mithi hose.
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Apr 23, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  pale serikali ya kijiji inakata kila lori linalokuja ts 100/= ya kutengenezea barabara na kufukia mashimo ila hizi taarifa ni za miaka mitatu iliyopita sasa hivi nadhani kutakuwa kumebaki mahandaki tu ..na huu msitu ni chanzo cha maji ya mto saseni huu mto unaenda hadi kwenye mbuga ya mkomazi na bwawa la ndungu na kihurio kama wakiendelea hivi ni wazi kuwa kutakuwa na impact kubwa sana siku za usoni...
   
 7. m

  mahoza JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 1,242
  Likes Received: 411
  Trophy Points: 180
  Uchumi tunao tumeukalia. Lori Tshs 100? Naona km matusi vile maana hata $ 200 kwa lori ni ndogo. Jamani nani wakusaidia? Au tumuombe Mh Zitto akimaliza kikao kinachoendelea aende wilaya ya Same akafichue? Jamani msaidieni Mh Zitto nawengine nao wafhatilie hili na mradi wa tangawizi kwa Mh Anna Kilango.
   
 8. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #8
  Apr 23, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280
  Hayo madini yanatumika kutengeneza cement huko Kenya.Willy ana mkono wa wakubwa ndani ya serekali karibu tenda zote za kujenga nyumba za polisi kapewa sasa hivi kaanzisha kampuni nyingine ya uchimbaji wa maji naambiwa miradi ya uchimbaji wa maji vijijini kapewa pia.
   
 9. m

  mahoza JF-Expert Member

  #9
  Apr 23, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 1,242
  Likes Received: 411
  Trophy Points: 180
  Jamani Thame twafa tuokoni. Nakubali kuwa huyu wille anatumika na wakubwa nadhani hata Mh Mathayo anafahamu kwa kuwa mradi aliukuta alipochaguliwa akashindwa kumvisha nyau kengele.
   
 10. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #10
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,587
  Likes Received: 1,563
  Trophy Points: 280
  Ni lazima tuliangalie jambo hili kwa umakini mkubwa.
  Kwanza ni kuwa mwenye kampuni ni mzawa wa kijiji hicho.Pili rushwa ni kubwa sana kilimnjaro yote na viongozi wa vijiji naamini wanazipokea pesa lakini hazifiki.
  Uharibifu ni mkubwa na kuna wakati watu nzumba zimevunjika kutokana na maporomoko na wakayamaliza kienyeji.
  Mwandishi wa habari nguli wa mazingira Johnson Mbwambo huko ni kwenu hebu fuatalia
   
 11. m

  mkizungo JF-Expert Member

  #11
  Apr 23, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 247
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nipo na wewe sunyelani vukiken,,,,,,ninakuja,,,,,,,,tuoshwa virundu,,,,,,,
   
 12. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #12
  Apr 23, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  wale wazee wa kijini wanajua kitu basi..wakishapewa hio pesa wanaenda kufukia mashimo barabarani na kwenda kunywa dengerua basi biashara imeisha
   
 13. Planner

  Planner JF-Expert Member

  #13
  Apr 23, 2012
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 296
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Huyu bwana(Willy) anaonekana anakibali ambacho kapewa huko juu manake hata miundo mbinu anayotumia ni ya kisasa inaonekana ana confidence na hilo dili,na ni kweli kuwa tenda za ujenzi wa nyumba za polisi bara na visiwani amepewa,so yuko intact na system.
  Ila Mh Mathayo nashindwa kumuelewa juu ya issue ya umeme katika kata ya mhezi(eneo hilhilo la machimbo),huyu muwekezaji alivuta umeme juu kwa juu kupeleka kwenye mradi wake baada ya hapo wananchi walio jirani wakaahidiwa kuwa umeme utasambaa kwa wote na TANESCO wakaleta mpaka nguzo na kuzilundika ila ni miaka sasa imepita kimya,sijui mbunge ameweka kuwa ndo strategy ya kuombea kura manake kila anapokuja anadai umeme utafika nipeni kura,mimi ni mwananchi wa kata husika nayaongea haya with empirical evidence,saivi anadai eti tusubiri sijui ndo rural energy agency,yaani nia aibu!MH funguka sasa tumechoka story zako !
   
 14. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #14
  Apr 23, 2012
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Una-mtetea?:A S 41:
   
 15. Captain22

  Captain22 JF-Expert Member

  #15
  Apr 23, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Hayo malori ni ya willy Enterprises. Ana tenda ya kusupply udongo unao tumika katika uzalishaji wa cement. Anatenda Athi river kenya, bamburi kenya na tanga cement.
   
 16. agatony8l

  agatony8l JF-Expert Member

  #16
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkuu ukistaajabu ya Afghanistani nafikiri ya Bongo huyajui, kwenye huo msitu si tu kuwa ni Hifadhi ya Taifa, bali pia ina vyanzo vingi vya maji ambavyo kwa namna uchimbaji wa huo mchanga unavyoendelea ni hatari tupu vingine vishaanza kukauka. Wananchi wanalalamika, serikali ya kijiji inalalamika AJABU NI KUWA HATA WILAYA IMESHINDWA KUINGILIA KATI NA KUKOMESHA UCHAFUZI HUU WA MAZINGIRA. jamani iko wapi nchi yetu ile ilokuwa inaitwa nchi ya vijito, mito na maziwa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! IMG_0923.JPG IMG_0924.JPG IMG_0925.JPG
   
 17. m

  mahoza JF-Expert Member

  #17
  Apr 23, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 1,242
  Likes Received: 411
  Trophy Points: 180
  Am just tired with these magamba people. Je hiyo tenda ya nyumba za polisi ilitangazwa.? Inaniuma mno jamani Mh Matayo pembeni tunataka kamanda huko atainua upzo wote. Ila wakati hui naomba hii issue ya madini iende mbdle. Wananchi wameambiwa nyumba zitabolewa ili hayo malori yapita ila haluna ambaye amefanya valuation kuwa kila mwenue nyumba au kibanda atalipwa nini. Wasaidieni hawa wapare jamani it is ova 2 much now. Lets stick 2gether.
   
 18. m

  mahoza JF-Expert Member

  #18
  Apr 23, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 1,242
  Likes Received: 411
  Trophy Points: 180
  Asante kwa picha mwanaJF
   
 19. n

  nakuru Member

  #19
  Apr 23, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyu jamaa mwenye mradi ni wille yupi..........au ni wille interprises wa Arusha?

   
 20. m

  mahoza JF-Expert Member

  #20
  Apr 23, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 1,242
  Likes Received: 411
  Trophy Points: 180
  Nadhani ndo huyo kutokana na mchango wa captain 22. Km waweza kasomepitia mchango wake. Asante.
   
Loading...