Uchaguzi 2020 Jimbo la Kibamba lipo wazi kwa CCM, kazi kwenu

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,122
7,707
Miongoni mwa majimbo katika mkoa wa DSM Jimbo la Kibamba ambalo lipo katika wilaya mpya ya Ubungo limetendewa haki na ilani ya CCM licha ya kuwa chini ya mbunge wa upinzania John Mnyika lakini maendeleo makubwa katika jimbo eneo hilo yameletwa na kusimamiwa kwa jitihada ya CCM.

Katika jimbo hilo kuna miradi mikubwa inayo endelea kwa mfano; Mradi mkubwa wa ujenzi wa stendi ya mabasi mbezi, ujenzi wa njia sita Kimara -- Kiluvya, ujenzi wa tank kubwa la maji, ujenzi wa hospitali ya wilaya, ujenzi wa soko kubwa la ndizi Kiluvya Bwawani, n.k

Kuna miradi lukuki inaendelea katika eneo hilo. Kwa jitahada hizo ni dhahiri jimbo hilo tayari limesha gombolewa kutoka mikononi mwa Chadema, sasa CCM msifanye kosa, teueni mtu makini mwenye amsha amsha ya maendeleo, tayari jimbo ni lenu hilo, hili ni jimbo muhimu sana kwani ndio lango kuu la uchumi wa DSM.

Kipenga kimesha pulizwa waliotia nia uwanja kwenu.
 
Mkuu kwani wewe ndo box la kura Hadi utoe kauli za kibabe hivi?
Je huoni Kama uwepo wa Mnyika katika Jimbo Hilo ndo chanzo Cha kuletwa hayo maendeleo ili CCM wapate Cha kuongea kwenye kampeni za Jimbo la kibamba?

Sasa akitoka hujui Kama serikali itarelax maana haitakuwa na ushindani tena kwa kurudisha Jimbo lake Kama ulivyo Sasa?

Think big Usiombee upinzani ufe. Upinzani Ni mhimu sana katika kukisukuma chama kilichopo madarakani kuleta Maendeleo.

"Leo hii bila kuwepo upinzani mkali Rais lMagufuli A.K.A jiwe la Afrika Asingeweza kuwa Rais badala yake Angekuwa Membe au Lowassa ili upigaji uendelee. Ila kutokana na Hali ilivyokuwa tete ndani ya CCM kipindi hicho Wakaona Magufuli ndo mtu pekee anaeweza kushindana na nguvu ya upinzani kutokana na nature yake ya uchapa Kazi.
 
tatizo mbunge aliye kuwepo hakuwa karibu na wanananchi wake ktk kushughulikia kero za wana nchi wake.
..yote yanayo fanyika ktk jimbo la kibamba sio kwa jitihada za Mnyika bali ni kwa nguvu sa serikali sasa tunajiuliza je? kama ange kuwa mbunge wa chama cha Rais si wananchi wange nufaika mara dufu.
nadhani octoba 2020 jibu litapatikana
 
Siasa hizi kiukweli mnyika katusahau wana kibamba
Hyo miradi si ya watanzania wote au?
 
Mnyika ni wa ajabu sana mie toka nianze kukaa hii wilaya mara ya mwisho kumuona anazungukia huku ni last election na mbaya zaidi tunachangamoto nyingi ila kila siku tunamuona akipinga kila kitu mbungeni yeye na mdee wapumzike tu maana changamoto zao zinafanana
 
Kwamba kwa kuwa Kuna miradi inatekelezwa Basi ndo Jimbo liko wazi kwa CCM?
Kwa hiyo unadhani majimbo mengine ya wapinzani Hakuna hata miradi inayofanyika?Na Mimi naweza kukwambia kwa Dsm Jimbo la Temeke,kigamboni na kinondoni,ukonga na kule kwa Bonna Karua hawezi kupita yako wazi kwa chadema.kwa kuwa hakuna Cha maana serikali imefanya huko.
Kuchaguliwa kwa chama chochote haihusiani na miradi Bali inategemeana na unayemsimamisha anamvuto gani kwa jamii anayogombea.Nani alikuwa Wassira angeshindwa kwa aibu?Nani alijua shein angeshindwa urais Zanzibar 2015?Ni kwa sababu ya ushawishi.
 
Tumia akili kazi ya kodi ni kujenga nchi

Wewe tahira umetokea wapi

Madhara ya shule za kata ndio haya

Soma shule, Ujue wananchi tunalipa kodi na anayekusanya ni ccm na serikali yake yawapasa hata kutuletea chakula bure majumbani

Hivi matahira kama nyinyi mna shida gani?
 
tatizo mbunge aliye kuwepo hakuwa karibu na wanananchi wake ktk kushughulikia kero za wana nchi wake.
..yote yanayo fanyika ktk jimbo la kibamba sio kwa jitihada za Mnyika bali ni kwa nguvu sa serikali sasa tunajiuliza je? kama ange kuwa mbunge wa chama cha Rais si wananchi wange nufaika mara dufu.
nadhani octoba 2020 jibu litapatikana
Utopolo mtupu.

Unapaswa umsifie aliyekukimbiza,sio kujisifia wewe binafsi kwa jitihada zako.
Asingekuwa Mnyika kumhenyesha Jiwe,leo Ubungo ingekuwa kama majimbo mengine yaliyopo chini ya chama twawala.
 
Mnyika ni wa ajabu sana mie toka nianze kukaa hii wilaya mara ya mwisho kumuona anazungukia huku ni last election na mbaya zaidi tunachangamoto nyingi ila kila siku tunamuona akipinga kila kitu mbungeni yeye na mdee wapumzike tu maana changamoto zao zinafanana
Akili yako imejaa tope,huyo m bunge wako ungemuona vipi wakati hakuruhusiwa hata kufanya mikutano ya shukrani?
Pale makabe alitaka kufanya mkutano 2018,policcm wakauzuia,mimi nilikuwepo.
 
tatizo mbunge aliye kuwepo hakuwa karibu na wanananchi wake ktk kushughulikia kero za wana nchi wake.
..yote yanayo fanyika ktk jimbo la kibamba sio kwa jitihada za Mnyika bali ni kwa nguvu sa serikali sasa tunajiuliza je? kama ange kuwa mbunge wa chama cha Rais si wananchi wange nufaika mara dufu.
nadhani octoba 2020 jibu litapatikana
Polisisiemu wanazuia mikutano yote hata ya ndani, angeonana vipi na hao wananchi?? Wa kulaumiwa ni sisiemu
 
Majimbo mengine yapi yenye wabunge wa chama cha Rais ambapo wananchi wamenufaika maradufu.?

Elimu! Elimu! Elimu!
 
Polisisiemu wanazuia mikutano yote hata ya ndani, angeonana vipi na hao wananchi?? Wa kulaumiwa ni sisiemu
mikutano ktk jimbo lake haikuzuiwa, ila yeye alikuwa bise na mambo mengine sio kero za jimboni kwake
 
Majimbo mengine yapi yenye wabunge wa chama cha Rais ambapo wananchi wamenufaika maradufu.?

Elimu! Elimu! Elimu!
bilashaka, mbunge aliye karibu kuzungumza na Rais ni yule mwenye chama alicho Rais husika, ukaribu uliopo huraisisha na hulainisha zaidi kazi
 
Kwani ccm isiwekeze nguvu kwenye majimbo ya wabunge wake ambao Hali ni mbaya Kama Jimbo la ndugai, na kwenda majimbo ya upinzani hivi ni akili kweli
kuna majimbo ni strategic, mfano majimbo yote ya DSM ni Muhimu sana kuwa chini ya chama tawala iwe ccm chadema au chama chochote kile kitakacho chukua dola, ni lazima maeneo muhimu yadhibitiwe na chama tawala, na majimbo mengine utakuwa unayajua,
 
Back
Top Bottom