Uchaguzi 2020 Jimbo la Iramba hakika ni kumi yatosha!

Mnambua

JF-Expert Member
Jan 6, 2020
246
233
Kutokana na CCM kuweka mazingira mazuri ya kuzuia watia nia kujipitisha pitisha kwa ajili ya kugombea katika Uchaguzi huu na msisitizo wa kutotumika kwa rushwa, imejulikana kuwa kigezo kikubwa kinachoenda kumtoa Dkt Mwigulu Nchema kwenye kinyanganyiro ni vitendo vyake vya kifisadi amabavyo ameshavifanya. Wapinzani wake wameshakusanya ushahidi wa kutosha ambao watautumia kukata rufaa iwapo Uongozi wa Chamawa Juu utaamua kumkumbatia. Kuna ambao atayari wameahidi kuhama Chama iwapo itataokea dkt. Mwigulu anapewa nafasi ya kugombea tena. Wanaamini katika usemi wa "KUMI YA DKT. MWIGULU YATOSHA".

Rafiki yangu mmoja akiongea na mimi kwa simu kutoka Dodoma alipoenda kwenye Mkutano Mkuu juzi alieleza wazi kuwa ameona baadhi ya viongozi wa CCM wa Mkoa wakimzunguka Mwenyekiti Ndugu Juma Kilimba na kwenda na Dkt Mwigulu maeneo ya Hotel ya Fantasy na kuweka mikakati ya ushindi kwa kuwa Dkt Mwigulu anaamini kati ya majina matatu yatakayorudishwa na la kwake litakuwepo. Inasemekana hao jamaa waliondoka na kiasi fualni cha fedha amabazo Dkt Mwigulu amewapatia ili wakaanze kumpangia Timu ya Ushindi.

Wakati Dkt Mwigulu akiendela na mikakati yake Mtia nia ambaye anaonekana kumpa kiwewe zaidi ni Eng. Jumbe Katala ambaye ameshashika Tarafa zipatazo nne za Wilaya ya Iramba wakati Tarafa ya Kisiriri ambayo amejenga Shule yake ya Sekondari inaongoza kumuunga mkono. Jumbe Katala ameonesha kuwazidi wenzake kama akina David Jairo, Grace Mkoma na Timoty Lyanga ambao wanaonesha wazi kuwa na kusudio la kugombea katika Jimbo hilo. Ndugu wa karibu wa Kijana anayetoka Kata ya Kyengege Mwanasheria Kitandu Ugula amesisitiza kuwa Mwanasheria huyo pia atagombea bila kuonesha nia kwani anafuata taratibu za kichama za bila kujitangaza. Wengine wanaotarajiwa kugombea lakini hawajasema chcochote kwa kipindi hiki ni akina William Shila wa Ulemo, Richard Mkumbo wa Uwanza ambaye ni Ndugu yake na Prof. Kitila Mkumbo ambaye ameonesha nia kuwania Ubungo Dar-es-Salaam.

Wengine ambao wamejitokeza wazi kugombea kwa upande wa upinzani ni pamoja na Jeska Kishoa kwa upande wa CHADEMA. Chama cha Act Wazalendo pia kinasemwa kuweka Mgombea mabaye kwa sasa atashiriki kwanza kinyanganyiro kupitia CCM na akishindwa ndiyo atahamia Act Wazalendo. Watia nia wageni wote wamepanga kuhakikisha Dkt. Mwigulu harudi kwa sababu wamechukizwa na kile anachojitamba nacho na kukosa unyenyekevu kuwa yeye ni Mamba aliyepo kwenye kina kirefu.
 
Wanyiramba akili zenu zina shida Mwigulu atawatesa sn, bahati mbaya hata wakituma ushahidi chama ni mali ya mtu binafsi na Mwigulu sasa ni lulu kwa mwenye chama chake. Hopeless nyie chagueni upinzani
wewe ndo pathetic hopeless.., kushikiwa akili, kuwahusudu na kua dictated na walevi wa kabila fulani, hta kama kweli mwigulu hafai si lazima wanyiramba wachague upinzani, mabadiliko yawezekana hta ndani ya chama hicho hicho cha mkulu.
 
Acha kupotosha uma kwa chuki binafsi na mihemuko yako ya kichadema, hakuna kabila lisilokunywa pombe zake za kienyeji. Wanyiramba ni moja ya wachapakazi wazuri sana na si wavivu kama ulivobwata...
Sio KiCHADEMA bali ni chuki binafsi zake tu huyo!
 
Acha kupotosha uma kwa chuki binafsi na mihemuko yako ya kichadema, hakuna kabila lisilokunywa pombe zake za kienyeji. Wanyiramba ni moja ya wachapakazi wazuri sana na si wavivu kama ulivobwata...
Wangekuwa siyo wavivu mgemchangua Mwigulu pamoja na kuwa na nyumba za tembe? chapeni kazi nitajie mnyiramba mmoja tajiri anayejulikana hapa nchini
 
Wangekuwa siyo wavivu mgemchangua Mwigulu pamoja na kuwa na nyumba za tembe? chapeni kazi nitajie mnyiramba mmoja tajiri anayejulikana hapa nchini
Tehe tehe. Matajiri wa Tanzania ni kabila gani kwani - WaSukuma tuna Kishimba ati!
 
Back
Top Bottom