Elections 2015 Jimbo La Bukoba mjini mmefanya makosa makubwa kumuondoa Sued Kagasheki

Mbunge Sued Kagasheki,
1. Mikopo Kwa Kina Mama,
2. Vijana Wanapatiwa Pikipiki Kwa Kurejesha Ela Taratibu, Mwaka Huu Kawapatia Pikipiki 300,
3. Ukarabati Wa Hospitali Ya Mkoa Na Kuwapatia Ambulance Na Kugharamia Mafuta Yake,
4. Bill Ya Umeme Ya Hospitali Zote Na Vituo Vya Watoto Yatima Bado Analipa Yeye
5. Kuwapatia Fursa Vijana Kucheza Ligi Yenye Thaman Ya Mil 35 Kwa Miez 6,
6. Kubadilisha Furniture Za Shule Zote Za Serikali Kila Zinapochakaa
7. Katoa Fursa Ya Ajira Kupitia Vick Fish,
8. Kapambana Na Fisad Aman Anatory Katika Sakata La Viwanja Bukoba
9. Kina Mama Wamepewa Fursa Ya Ufugaji Kila Mama 5 Ng'ombe 1 Bule
10. Kuweka Mitego Ya Radi Kila Shule Kuzuia Vifo Vilivyotokea Siku Za Nyuma, Kaweka Tv Na Umeme Shule Zote, Na Kujenga Darasa Moja Moja Kila Shule,
Je Mlitaka Afanye Nin Zaid Ya Icho? Pia Mmelalamika Eti Anaweza Chukua Ambulance Alizogawa Hospitalin, Nahs Dhana Ya Mabadiliko Hamkuielewa

inawezekana hayo hayakuwa vipaumbele vya wapiga kura wake, wao walitaka mabadiliko ya kuzungusha mikono na wamepata, alipaswa awape kazi twaweza na repoa wamfanyie research ili ajue priorities za wananchi wake. Isitoshe watu wa kagera ni wa ajabu sana kama walimshangilia Idd Amin huku wamebeba majani ya migomba pamoja na kuwapiga risasi.
 
hakuna mji wenye unafiki kama ule Tanzania hii...we jua hivyo tu...ila vicfish ni yake kweli?..mi najua anamiliki ASU ambapo pia kuna ajira za kutosha...wataona mabadiliko.
 
Hakika watu wa Bukoba na Kagera kwa ujumla miaka yote wamesifika kwa ujasiri wa kujitegemea, ujasiliamali na kusaka elimu. Kwa historia yao iliyotukuka wana Bukoba wanahitaji kuwezeshwa kimiundombinu na kimitaji ili waweze kuinua maisha yao. Mbunge au kiongozi wa aina ya Kagasheki anayejikita katika uhisani wa wateule wachache hafai. Mbunge na wote wenye madaraka wanahitaji kuelekeza nguvu kwenye miradi mikubwa na endelevu yenye kugusa maisha ya maelfu ya wenyeji waliopigika kiuchumi na sasa kielimu.

Bukoba tunahitaji SOKO jipya na la kisasa ili kuwawezesha maelfu ya wauzaji na wanunuzi kuendesha shughuli zao kwa ufanisi na tija. Zile chokochoko baina ya Kagasheki na mtu wake Aman zilizosababisha kushindwa kwa mradi huu ni sababu tosha ya kumkosesha ubunge Kagasheki. Bukoba tunahitaji stendi mpya na ya kisasa ya mabasi. Wana Bukoba na Kagera tunahitaji usafiri wa meli wa uhakika zaidi ya miaka 15 tangu tuwapoteze ndugu zetu zaidi ya 800 kutokana na matumizi wa meli mbovu.
Mwisho Kagera tunahitaji Chuo Kikuu kikubwa na cha hadhi ya kimataifa - siyo matawi ya vyuo vya makanisa vya SAUT na TUMAINI. Kwa mkoa wenye zaidi ya wakazi millioni mbili na historia ya wenyeji wapenda elimu (nshomile) ni aibu kuzidiwa sana na mikoa ya Morogoro na Kilimanjaro yenye vyuo vikuu zaidi ya vitatu vyenye hadhi ya kimataifa. Wabunge wetu wapya walete mabadiriko katika maeneo haya na siyo kuleta bodaboda na ambulance ambalo ni jukumu la serikali.
 
Wewe ndio umemaliza, mambo yote aliyoongea huyu ni ya hisani, hatuwezi kuwa na wabunge wa aina ya Dewji, miaka 5 hajawakilisha wananchi mara anachimba kisima hapa na pale.

Sisi wabunge maskini tutawezaje kufanya kazi za serikali?

Kweli kabisa mkuu na yote haya ni kuishi chini ya mfumo mbovu wa watawala wetu ambao wanawadanganya wananchi eti kazi ya mbunge ni kuchimba visima au kujenga mitalo na kuiacha serikali ikitumia kodi kwa anasa
 
Hiyo misaada inatolewa na WAHISANI na si yeye acheni kutudanganya. WANABUKOBA WAMEGUNDUA KUA ANACHOWAPA SIO ANACHOPOKEA.
 
Mbunge Sued Kagasheki,
1. Mikopo Kwa Kina Mama,
2. Vijana Wanapatiwa Pikipiki Kwa Kurejesha Ela Taratibu, Mwaka Huu Kawapatia Pikipiki 300,
3. Ukarabati Wa Hospitali Ya Mkoa Na Kuwapatia Ambulance Na Kugharamia Mafuta Yake,
4. Bill Ya Umeme Ya Hospitali Zote Na Vituo Vya Watoto Yatima Bado Analipa Yeye
5. Kuwapatia Fursa Vijana Kucheza Ligi Yenye Thaman Ya Mil 35 Kwa Miez 6,
6. Kubadilisha Furniture Za Shule Zote Za Serikali Kila Zinapochakaa
7. Katoa Fursa Ya Ajira Kupitia Vick Fish,
8. Kapambana Na Fisad Aman Anatory Katika Sakata La Viwanja Bukoba
9. Kina Mama Wamepewa Fursa Ya Ufugaji Kila Mama 5 Ng'ombe 1 Bule
10. Kuweka Mitego Ya Radi Kila Shule Kuzuia Vifo Vilivyotokea Siku Za Nyuma, Kaweka Tv Na Umeme Shule Zote, Na Kujenga Darasa Moja Moja Kila Shule,
Je Mlitaka Afanye Nin Zaid Ya Icho? Pia Mmelalamika Eti Anaweza Chukua Ambulance Alizogawa Hospitalin, Nahs Dhana Ya Mabadiliko Hamkuielewa

Said Kagasheki ndio nani aisee
 
Kweli kabisa mkuu na yote haya ni kuishi chini ya mfumo mbovu wa watawala wetu ambao wanawadanganya wananchi eti kazi ya mbunge ni kuchimba visima au kujenga mitalo na kuiacha serikali ikitumia kodi kwa anasa

Sijui kama watakuelewa
 
Mbunge Sued Kagasheki,
1. Mikopo Kwa Kina Mama,
2. Vijana Wanapatiwa Pikipiki Kwa Kurejesha Ela Taratibu, Mwaka Huu Kawapatia Pikipiki 300,
3. Ukarabati Wa Hospitali Ya Mkoa Na Kuwapatia Ambulance Na Kugharamia Mafuta Yake,
4. Bill Ya Umeme Ya Hospitali Zote Na Vituo Vya Watoto Yatima Bado Analipa Yeye
5. Kuwapatia Fursa Vijana Kucheza Ligi Yenye Thaman Ya Mil 35 Kwa Miez 6,
6. Kubadilisha Furniture Za Shule Zote Za Serikali Kila Zinapochakaa
7. Katoa Fursa Ya Ajira Kupitia Vick Fish,
8. Kapambana Na Fisad Aman Anatory Katika Sakata La Viwanja Bukoba
9. Kina Mama Wamepewa Fursa Ya Ufugaji Kila Mama 5 Ng'ombe 1 Bule
10. Kuweka Mitego Ya Radi Kila Shule Kuzuia Vifo Vilivyotokea Siku Za Nyuma, Kaweka Tv Na Umeme Shule Zote, Na Kujenga Darasa Moja Moja Kila Shule,
Je Mlitaka Afanye Nin Zaid Ya Icho? Pia Mmelalamika Eti Anaweza Chukua Ambulance Alizogawa Hospitalin, Nahs Dhana Ya Mabadiliko Hamkuielewa
kwahiyo unahisi hizo ndio kazi na majukumu ya mbunge?
 
Britanicca hayo ni mahaba kwa Kagasheki. Kafanya mambo mazuri, well and good. Amuachie kijiti mwingine aendeleze kwa viwango vya juu zaidi.
 
Word. Well said

Tatizo letu wananchi tumeamua kwa makusudi kubadilisha majukumu ya mbunge kutoka kuwa mwakilishi wetu na kumpa majukumu ambayo yanapaswa kutekelezwa na wale tuliowapa dhamana ya kukusanya kodi.Binafsi siamini kama kusomesha wanafunzi ni jukumu la mbunge. Kama ni jukumu lake basi alipe ada kwa wanafunzi wa jimbo zima.
 
Angekuwa kwel anayafanya hayo yote sizan kama raia wangempiga chin!!

Vip mbona ambulace kazikusanya tena?
 
Kama haya yote alikuwa anatoa kwenye mfuko wake mwenyewe, basi hafai hata kidogo. Uwepo wa viongozi wa namna hii unaifanya serikali inayokusanya kodi zetu ilale saaana na kuwafanya wachache kuiibia serikali. Kazi ya mbunge sio kugawa haya mavitu, ni kuwawakilisha raia na kuisimamia serikali. Sasa huduma ambayo ilipaswa itolewa na serikali inatolewa na mbuge (sijui kwa raha ipi), basi mbunge ndiye serikali na endapo atakula fedha za umma ni vigumu kumuwajibisha maana anavokwimba katika eneo moja anavileta kwa mkono mwingine. Hii sio kwa kagasheki tu, nadhani raia nchi hii wanadhani mbunge anawajibika kuleta maji, kujenga barabara badala ya KUISIMAMIA serikali ifanye hayo na mengine zaidi ya hayo. Sasa Bukoba mjini, wambane mbunge wao mteule ahakikishe anaibana serikali inavileta hivyo vitu badala ya kumtegemea binadamu. Obama anasema Africa needs strong institutions not individuals!!!!!!!
Mbunge Sued Kagasheki,
1. Mikopo Kwa Kina Mama,
2. Vijana Wanapatiwa Pikipiki Kwa Kurejesha Ela Taratibu, Mwaka Huu Kawapatia Pikipiki 300,
3. Ukarabati Wa Hospitali Ya Mkoa Na Kuwapatia Ambulance Na Kugharamia Mafuta Yake,
4. Bill Ya Umeme Ya Hospitali Zote Na Vituo Vya Watoto Yatima Bado Analipa Yeye
5. Kuwapatia Fursa Vijana Kucheza Ligi Yenye Thaman Ya Mil 35 Kwa Miez 6,
6. Kubadilisha Furniture Za Shule Zote Za Serikali Kila Zinapochakaa
7. Katoa Fursa Ya Ajira Kupitia Vick Fish,
8. Kapambana Na Fisad Aman Anatory Katika Sakata La Viwanja Bukoba
9. Kina Mama Wamepewa Fursa Ya Ufugaji Kila Mama 5 Ng'ombe 1 Bule
10. Kuweka Mitego Ya Radi Kila Shule Kuzuia Vifo Vilivyotokea Siku Za Nyuma, Kaweka Tv Na Umeme Shule Zote, Na Kujenga Darasa Moja Moja Kila Shule,
Je Mlitaka Afanye Nin Zaid Ya Icho? Pia Mmelalamika Eti Anaweza Chukua Ambulance Alizogawa Hospitalin, Nahs Dhana Ya Mabadiliko Hamkuielewa
 
Ambulance huko kwenu Bkb nilisoma mahala kuwa kashaichukua na kuondoa yaliyokuwa yameandikwa...kumbuka ilikuwa ya msaada walivyosema.
 
Kwanini Sasa Aendelee Kutoa Misaada Kwa Wanafiki,

Kwani hana kazi ingine ya kufanya? Ubunge sio yeye tu ndio maana kuna uchaguzi.

Akachunge ng'ombe, kumbuka aliachishwa kazi kiongozi gani anasimamishwa kazi.

Pole mwana familia, lazima na wewe ulikuwa unakula vya wananchi kichinichini na kijuu juu.
 
umesahau wewe,
11. chuo cha ntungamo, bltc, katoke anasomesha watoto kadhaa akiwepo yatima takriban 30,
13. nenda KEMEBOS, MILDLAND UGANDA, NSHAMBYA fanya utafiti ujue amesomesha wanafunz wangapi kwa msaada wake
14. pia kasaidia kwenye tehama pale josiah kibira university college, kafanya mengi swahiba, JAPO ANASAIDIWA NA WAZUNGU,

Umenena misaada ya watu wema ulivyoandika ma mleta mada ni misaada alinebea jina lake.

Si ni mhaya au aliamia bkb?

Nilikuwa simjui hadi alipofukuzwa kazi ndio nikayajua ya Bukoba kuwa napo wapo wapenda vyeo.
 
Back
Top Bottom