Jimbo jipya la uchaguzi

Vawulence

JF-Expert Member
Jan 4, 2009
1,928
2,101
Walemavu 'walilia ’ jimbo lao la Uchaguzi Imeandikwa na Jasmin
Shamwepu, Dodoma;
Tarehe: 4th December
2010 @ 22:50 Imesomwa
na watu: 28; Jumla ya
maoni: 0 SHIRIKISHO la Vyama vya
Watu wenye Ulemavu
Tanzania (SHIVYAWATA)
limeiomba serikali
kufikiria uanzishwaji wa
Jimbo la Uchaguzi kwa ajili ya watu wenye ulemavu
tofauti na ilivyo sasa. Ombi hilo lilitolewa na
Mwenyekiti wa
SHIVYAWATA, Lupi
Maswanya alipokuwa
akisoma taarifa yake
kwenye Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye
Ulemavu Duniani
yaliyoadhimishwa juzi
kitaifa mkoani Dodoma. Alisema pamoja na
kuwepo nafasi tatu za
watu wenye ulemavu,
lakini bado wabunge hao
hawawezi kuwajibishwa
na vyama vya watu wenye ulemavu kutokana
na wabunge hao kutotoka
katika vyama hivyo. Lupi alisema watu wenye
ulemavu wanatakiwa
kupata nafasi za
kuwatetea watu wenye
ulemavu bungeni na
ambao wanatokana na walemavu wenyewe
tofauti na ilivyo sasa
ambapo watu wenye
ulemavu huteuliwa
kupitia Umoja wa
Wanawake Tanzania (UWT). Alisema
wanaiomba serikali
kuhakikisha inatoa nafasi
za watu wenye ulemavu kwa
kuwashirikisha kikamilifu
kwa kupewa fursa katika
vyombo mbalimbali vya
kutoa uamuzi kuanzia
ngazi ya Serikali za Mitaa hadi Serikali Kuu bila
kuwasahau katika uteuzi
wa nafasi mbalimbali za
kiutendaji. “Tunaiomba serikali itenge na kutoa ruzuku
kwa mujibu wa sheria
ndani ya bajeti ya serikali
ya kila mwaka kwa ajili ya
shughuli zote za watu
wenye ulemavu hapa nchini, jambo ambalo
litatuwezesha kujikwamua
kimaisha,” alisema Lupi . Alisema kiasi kinachotolea
na serikali sasa cha Sh
milioni 2.5 kwa kila chama
ni kidogo, kwani
hakiendani na maisha
halisi ya sasa hivyo kinatakiwa kiongezwe ili
kuweza kuvifanya
vyama vya watu wenye
ulemavu kufanya kazi kwa
ufanisi. Aliiomba serikali kupitia
Wizara ya Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) kuhakikisha
halmashauri zote nchini
zinatenga na kutoa ruzuku kila mwaka kwa
ajili ya shughuli za watu
wenye ulemavu ndani ya
maeneo husika.

My take:
Kuna mtu ameona upenyo hapa anataka kuutumia. Kwani viti maalumu hamna walemavu!!?
 
Kuna mama mmoja anaitwa Mkanga si ndio anayewakilisha walemavu bungeni? Tatizo pengine ni jinsi anavyopatikana kuwawakilisha hawa wananchi bungeni, kwani huyu mama amekuwa mbunge kwa miongo mingi sasa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom