Kamakabuzi
JF-Expert Member
- Dec 3, 2007
- 2,892
- 1,343
Leo saa saba mchana Baba Mtakatifu Benedict wa 16 ametangaza kuanzishwa kwa Jimbo jipya nalo ni Jimbo Katoliki la Kayanga.
Jimbo hilo limemegwa kutoka jimbo la Rulenge na litachukua eneo zima la Wilaya ya Karagwe yenye dekania za Karagwe na Kyerwa.
Pia baba Mtakatifu amemteua Padre Almichius Rwechungura kuwa Askofu wa Jimbo hilo. Kabla ya uteuzi huo, alikuwa makamu wa askofu wa Jimbo la Bukoba.
Askofu wa sasa wa Jimbo la Rulenge amewatangazia rasmi habari hiyo waumini wa Parokia ya Kayanga itakayokuwa makao makuu ya JImo hilo.
Jimbo la zamani la Rulenge linahamisha makao makuu kwenda Ngara mjini na kuitwa Jimbo la Rulenge- Ngara.
WOTE HONGERENI NA MUWE TAYARI KUTIMIZA YOTE TANAYOEDANA NA TUKIO HILI
TUMSIFU YESU KRISTU.

Last edited by a moderator: