Jikumbushe mpambano wa Ubunge kati ya Mwl. na Mkemia Magufuli na Mkulima Phares Kabuye

Kabuye alikuwa matata bungeni nikiwa dogo kabisa babangu alikuwa anatoa attention kumsikiliza Kabuye siku akiongea Bungeni ,so alikuwa na mizizi jimboni na hakika bila kugawa jimbo mh angekuwa anakuja pension
 
Jana niliweka uzi kama huu huu Mods Wakafuta kama mara mbili yani kuna ubaguzi leo tena nimeweka wa Magufuri kauli yake ya kusogeleana umefutwa tena lakini wengine wakipost uzi ahhh hakuna shida,
Sijui hawa Jamaa wanabaguanaje mi nilishaacha kupost maana either wanautafutia wa kuunganisha ama unafutwa. Siyo peke yako mkuu
 
UCHAGUZI WA UBUNGE JIMBO LA BIHARAMULO
Mnamo Mwaka 1985 Mwalimu wa Kemia shule ya sekondari Sengerema John Pombe Magufuli aligombea ubunge wa jimbo la Biharamulo akichuana na Mkulima Phares Kabuye. Kabuye alishinda na kutangazwa Mbunge, na Mwalimu Magufuli akarudi Sengerema kufundisha.

Mwaka 1990 Mwalimu Magufuli alichuana tena na Mkulima Kabuye kwa mara ya pili. Kabuye alimshinda tena Magufuli na kutetea kiti chake.

Mwaka 1995 wakati wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi, jimbo la Biharamulo liligawanywa na kupatikana majimbo mawili (Biharamulo Magharibi na Mashariki). Kabuye aligombea Magharibi akashinda. Magufuli nae akagombea Mashariki na kushinda kwa mara ya kwanza baada ya mpinzani wake wa muda mrefu kwenda magharibi. Baadaye jimbo la Biharamulo Mashariki lilibadilishwa na kuitwa Chato.

Miaka kadhaa baadaye Phares Kabuye alifariki kwa ajali Morogoro. RIP Phares Kabuye. "Bila kuigawa Biharamulo mara mbili nadhani sasa hivi John Pombe Magufuli angekuwa mwalimu mstaafu"

Nini maoni yako?

Source: Daniel Matipa
ajabu leo huyo mwalimu wa kemia ndio Rais wa nchi si mwalimu mstaafu, hapo ndo utajua kwanini wanasema mwacheni MUNGU aitwe MUNGU.
 
Alikuwa anafundisha na huo mzuzu, Maana sasa hivi unaweza kujikuta umefukuzwa,Walimu wengi videvu vyao ni vipara.
 
Huyu Kabuye hakuacha mtoto agombee hata ubunge kwa sasa hivi?

Nimevutiwa sana alivompeleka puta mwalimu mkemia. Chezea mkulima wewe
 
Magufuli ni mchapa kazi yaani ni result oriented hivyo ni mtendaji zaidi kuliko mwanasiasa; hivyo hana hulka ya kupendwa!! Ukimuwekea mpinzani kwenye chaguzi chances za kushindwa ni kubwa kuliko kushinda ndio maana handlers wake wanalilia asiwe na mpinzani!!
Mkuu umeongea fact kabisa, binafsi pia naona hawezi zile story za uongo uongo kama wanasiasa wengine na huongea kitu halisi kama ni kizuri au kinamfurahisha msikiaji umepeta ila kama ni kibaya au hakitamfurahisha msikilizaji inakula kwako na hapa ndipo wanasiasa wanapotuchotaga akili mara nyingi hutuambia yale yanayopendeza masikioni mwetu ili wazidi kupeta tu hata kama sio kweli au kiuhalisia hawafanyi hivyo.

Juzi wakati anarudisha form ya urais Dodoma kwemye hotuba yake alirudia kuponda awamu zilizopita, alisema awamu ya tano tumenunua ndege 11, hao wengine walishindwaje kwani sisi ni malaika? Halafu haikupita hata dk 1, nadhani aligundua kuwa kitu alichokisema ingawa ndio ukweli lkn kuna watu atakua amewakwaza hasa Ma-rais wastaafu ghafla akasema lkn anawashukuru watangulizi wake kuanzia awamu ya kwanza kwa kutegeneza mazingira ambayo yamewasaidia wao kuweza kutekeleza haya wanayoyatekeleza sasa.

Kweli the man is not politician na kukiwa na level playing field bila figisu figisu zozote na wanasiasa wengine anaweza kupoteza mapema sana.
 
Jana niliweka uzi kama huu huu Mods Wakafuta kama mara mbili yani kuna ubaguzi leo tena nimeweka wa Magufuri kauli yake ya kusogeleana umefutwa tena lakini wengine wakipost uzi ahhh hakuna shida,
Una damu ya kunguni! Uwage unawarushia mods hela ya vocha.
 
Toka jimbo la Chato lianzishwe Magufuli hakuwahi kuwa opposed na vyama vingine kwa kufanya figisu figisu wakati wa mchakato hivyo alikuwa akipita bila kupingwa tu.

Ndiyo maana hata kufanya siasa hawezi maana kazoea vya kunyonga
Well said
 
kati ya wa watu waliokuwa wanachekesha sana bungeni ni mzee kabuye hasa kipindi cha mwisho alipokuwa TLP
 
UCHAGUZI WA UBUNGE JIMBO LA BIHARAMULO
Mnamo Mwaka 1985 Mwalimu wa Kemia shule ya sekondari Sengerema John Pombe Magufuli aligombea ubunge wa jimbo la Biharamulo akichuana na Mkulima Phares Kabuye. Kabuye alishinda na kutangazwa Mbunge, na Mwalimu Magufuli akarudi Sengerema kufundisha.

Mwaka 1990 Mwalimu Magufuli alichuana tena na Mkulima Kabuye kwa mara ya pili. Kabuye alimshinda tena Magufuli na kutetea kiti chake.

Mwaka 1995 wakati wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi, jimbo la Biharamulo liligawanywa na kupatikana majimbo mawili (Biharamulo Magharibi na Mashariki). Kabuye aligombea Magharibi akashinda. Magufuli nae akagombea Mashariki na kushinda kwa mara ya kwanza baada ya mpinzani wake wa muda mrefu kwenda magharibi. Baadaye jimbo la Biharamulo Mashariki lilibadilishwa na kuitwa Chato.

Miaka kadhaa baadaye Phares Kabuye alifariki kwa ajali Morogoro. RIP Phares Kabuye. "Bila kuigawa Biharamulo mara mbili nadhani sasa hivi John Pombe Magufuli angekuwa mwalimu mstaafu"

Nini maoni yako?

Source: Daniel Matipa
Kuna njia nyingi za kupita. Sisi binadamu tumefumbwa tusione baadhi ya mambo. Hivyo acha hizo fikra mfu za isingekuwa hivi ingekuwa vile. Kwani wewe ni malaika?
 
Back
Top Bottom