Jikumbushe mpambano wa Ubunge kati ya Mwl. na Mkemia Magufuli na Mkulima Phares Kabuye

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,305
12,968
1593515686299.png

UCHAGUZI WA UBUNGE JIMBO LA BIHARAMULO
Mnamo Mwaka 1985 Mwalimu wa Kemia shule ya sekondari Sengerema John Pombe Magufuli aligombea ubunge wa jimbo la Biharamulo akichuana na Mkulima Phares Kabuye. Kabuye alishinda na kutangazwa Mbunge, na Mwalimu Magufuli akarudi Sengerema kufundisha.

Mwaka 1990 Mwalimu Magufuli alichuana tena na Mkulima Kabuye kwa mara ya pili. Kabuye alimshinda tena Magufuli na kutetea kiti chake.

Mwaka 1995 wakati wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi, jimbo la Biharamulo liligawanywa na kupatikana majimbo mawili (Biharamulo Magharibi na Mashariki). Kabuye aligombea Magharibi akashinda. Magufuli nae akagombea Mashariki na kushinda kwa mara ya kwanza baada ya mpinzani wake wa muda mrefu kwenda magharibi. Baadaye jimbo la Biharamulo Mashariki lilibadilishwa na kuitwa Chato.

Miaka kadhaa baadaye Phares Kabuye alifariki kwa ajali Morogoro. RIP Phares Kabuye. "Bila kuigawa Biharamulo mara mbili nadhani sasa hivi John Pombe Magufuli angekuwa mwalimu mstaafu"

Nini maoni yako?

Source: Daniel Matipa
 
Kabuye alikuwa machachari sana sana pia. Hapa nashangaa kumbe alikuwa Mkulima!
Unashangaa Kabuye kuwa mkulima? Ulitemea awe msomi mwenye phd? Hapana unakosea Elimu na maarifa ni vitu sahihi maishani mwa binadam wengi hufikiri kuwa na elimu kubwa ndio utakuwa kiongozi machachari.a
 
Back
Top Bottom