Jikoni na Mwifwa, upishi wa mboga(samaki)

Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
46,918
122,182
Habari za muda huu wana JF.

Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia afya njema hadi muda huu.

Napenda kutoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki walioondokewa na wapendwa wao huko Morogoro mapema asubuhi ya leo.

Wapo wengi ambao ni mabachela kama mimi walipenda wapike chakula kizuri cha usiku(Dinner) kama Mwifwa, ila kwa mapenzi yake Muumba wao hajawajalia kufika muda huu wakiwa na pumzi zao kam sisi. MUUMBA WAPOKEE WAJA WAKO NA UWASITIRI KATIKA SEHEMU SALAMA WANAZOSTAHIKI. na UWAJALIE MAJERUHI WOTE WAWEZE KUPONA HARAKA

Naama sasa nije kwenye mada. Huu ni mtiririko wa upishi wa mboga zangu aina ya samaki kwa ajili ya chakula cha usiku siku ya leo.

Mahitaji:
-Nyanya
-Karoti
-Pilipili hoho
-Vitunguu
-Mafuta ya Alizeti
-Chumvi
-Samaki waliokaangwa

1.Hapa ni mkusanyiko wa materials yote tayari kwa kuyaosha.
IMG_20190810_190007.jpg
 
3. Nimechemsha maji na kuloweka samaki waliokaangwa ili walainike.

4. Nimekaanga vitunguu, karoti na hoho kwa pamoja kwa mafuta hadi vikaiva kabla ya kuweka nyanya nilizokatakata.

5. Nimeweka nyanya nilizomenya na kukatakata(sina kifaa cha kusagia) kwenye sufuria yenye vitunguu, karoti na hoho vilivyoiva ili nipate mchanganyiko wa supu nyanya zitakapoiva.
IMG_20190810_194251.jpg
 
7. Nimetia chumvi na kusubiri kwa dakika kadhaa hadi samaki waive pamoja na mchuzi/supu yenye mchanganyiko wa nyanya, karoti, kitunguu na hoho.

8. Sasa mzigo umeiva uko tayari kuliwa kwa chakula aina ya wali, ugali au chochote utakachoona kinafaa kuliwa kwa mboga hizi. hapa nitakula kwa ugali.
IMG_20190810_195552.jpg
 
11. Ugali tayari umeiva na nimeupakua kwenye sahani tayari kwa kuliwa.

Karibuni sana tule ugali wa kibachela ambapo hakuna kuhoji hata kama haujaiva vizuri, ukizidisha chumvi kwenye mboga unauchuna na kula kibishi maana hauna wa kumuuliza kwa nini chakula kimekuwa cha namna hii kama wale ambao wana wake zao.
IMG_20190810_202218.jpg
 
Back
Top Bottom