Jikoni Leo -Bamia,Kwanini Wanaume wengi Hawali?

hapo ukinipa na ugali aisee nitahitaji winchi nitolewe......
napenda mno bamia.....
yaani wakati mwingine napika hadi na nyama
 
LEO NDIO NIMEJUA BAMIA KWA KIINGEREZA INAITWA ''LADIES FINGER''




Nilijua inaitwa okra lakini kumbe marekani ndio wanaita hivyo ila kwa kiingereza Ladies finger.

Kwa nini ziliitwa ladies finger?inasemekana ni kwasababu ya umbo lake lilivyo kama vidole vywa mwanamke.

Bamia hukatwa na kupikwa kwa mapishi tofauti tofauti

Ukaipika kwa urefu kwa maana ya kukata kikonyo na ncha yakekisha kuiunga na nazi.

Hizi zimewekwa tayari kwa kuokwa.Zimepasuliwa katikati halafu kwa ndani ukawekwa mchanganyiko wa vitunguu maji,jeera,coriender,pilipili ya unga,chumvi,mafuta ya kula,tangawizi na nazi vikachanganywa na kutiwa humo.Hii ni recipe ya kihindi ndio huwa wantengeneza hivi.

Huu sio mlenda bali zimekatwa ndogo ndogo zikaungwa vizuri kama zinavyoonekana...njaa inaanza kuniuma sasa maana ninavyopenda bamia.

Mlenda pale unahusika.....ukichanganya na majani ya maboga,nyanya chungu saafi unapika ladies finger zako.

India wanakula sana bamia....hii ni salad ambayo imetengenezwa baada ya kuziosha vizuri ladies finger zako.Unakata kikonyo unaziweka kwenye sufuria na maji kidogo halafu unazichemsha kwa dk 3 hvi ila zibaki kijani kama zilivyo.Unakatakata nyanya vidogo vidogo,vitunguu,pilipili,unatia chumvi,limao kama unavyotengeneza kachumbari.Baada ya hapo unakata bamia kama zinavyoonekana unatia hiyo salad yako tayari kuliwa.
Faida ya kula Ladies finger bamia
1.Inasemekana ni chakula kizuri kwa watu wenye msongo wa mawazo,wanaojisikia weak n.k
2.Ni chakula kizuri kwa wanaotaka kupunguza mwili.
3.Mbegu za bamia zina protine nyingi na mafuta
4.Inasaidia mmeng'enyo wa chakula na kupata choo vizuri
5.Zina vitamin A na C
6.Madini ya potassium,calcium na magnesium


Kula bamia zako wala usizichukulie poa kisa zinateleza,ziko bomba kiafya.

Mkuu Mzizi Mkavu mambo gani haya kuzichechemua enzymes zetu mapema asubuhi?? Hutaki tufanye kazi tuanze kuutafakari ugali wa mchana kwa VIDOLE VYA KIKE aka Bamia??? Njaa imeanza kuniuma tayari...
 
Bamia nazipenda sana,tena bamia unazikaanga na biliganya,pilipili wowo,unaweza kuchanganya na nyanya ukipenda,ukila na ugali acha kabisa
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom