Jiko lako huenda likawa ni tiba na kinga yako ama angamizo la afya yako

hiv positive living

Senior Member
Jan 6, 2020
153
217
Hellow wapendwa poleni na majukumu ya siku nzima ya leo,,,

Nitashare nanyi baadhi ya aina ya vyakula/ tiba lishe ambavyo(yo) mimi huvitumia ,/nisivyovitumia;
1.sili ugali /wali/(vyakula vya wanga vyote)
Ila nacheat kidogo kwenye ndizi
2.sili mkate/andazi/vitumbua(vyakula vyote vya ngano)
3.vinyaji mfano soda, situmii, vyakula vya sukari pia mfano cake ,juice iloongezwa sukari , juice ya miwa ,
4.situmii kahawa kabisa
5.bites, pipi, pia situmii n.k
Kuna vingine tutaendelea kushare

Kwa miaka ya Nyuma ikiwa unapatwa una HIV basi cd4 juu ya 250 tulikuwa hatupatiwi ARV, safari yangu ya tiba lishe ilianzia hapa
Niliogopa dawa, niliogopa side effects vile navyoenda nawakuta watu wamechoka haswaaa
Hivyo mwaka nilojigundua niliishi kwa hofu na woga mwingi sana, mwaka wa pili nikanza kuona kidogo nipo sawa mwaka wa 3 ndipo nilipofanya maamuzi yaliyoniweka kwenye nafasi nzuri mpkaa sasa nayo ni "HEALTHY EATING"
Nilihakikisha nabadili mfumo mzima wa ulaji na kuishi
Nikapanga ratiba nzuri ya vyakula ,
Nikajiepusha na stress(oppsss hii ndio mbaya HIV inasubiri)
Nikabadili vinywaji + vipodozi
Nikazingatia muda wa kazi na kupumzika
Nikajiweka karibu na Mungu zaidi

Kwa uchache sana ndio haya
Tutaelekezana kwenye comments kulingana maswali yatakayoulizwa mkawe na mda mwema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi ukiacha vyakula vya unga both sembe na ngano pamoja na mchele hivi mwili utakuwa na nguvu kweli me naona kujitesa tu
 
Hivi ukiacha vyakula vya unga both sembe na ngano pamoja na mchele hivi mwili utakuwa na nguvu kweli me naona kujitesa tu

Unakuwa na nguvu kama kawaida kabisa!

Labda kama kazi unayofanya kama ni nguvu kama vile fundi ujenzi , mbeba zege, Mkulima, n.k

Kama unafanya kazi ngumu hapo utachoka kweli.

Lakini mtu ambae asubuhi anaenda kazini kwa gari toka nyumbani,

Akifika ofisini kazi yake ni ya kukaa kutwa nzima na kufanya kazi kwenye kompyuta au kuandika kwenye makaratasi huyo asipokula wanga atakuwa sawa kabisa na afya yake itakuwa njema na akila wanga baada ya muda ataanza kuona madhara yake!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi Nina mwezi wa 3-4 sasa tangu niliacha kula ugali kabisa,

Na nilikuwa napenda sana kula ugali au wali wa nazi.

Nimeacha kula vyakula vya wanga ikiwemo wali,

Kunywa chai na vitafunwa nimeacha isipokuwa mara moja moja nakulaga mayai tu.

Chai ya sukari naona hata Mwaka umefika sasa tangu niache!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asubuhi niamkapo nakunywa maji ya uvuguvugu yenye limao 2

Baadae nakunywa maziwa kikombe kikubwa cha karibia 1/2 lita bila kitafunwa.

Mchana embe dodo mdondo au ndizi 2 mbivu au mafenesi

Jioni mboga ya majani mchicha/tembele , samaki wa kukaanga au nyama au kuku

Ukiweza kutokula usiku ni nzuri zaidi

Kwa mfumo huu naamini pia unamwaka mzima hujaumwa kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asubuhi niamkapo nakunywa maji ya uvuguvugu yenye limao 2

Baadae nakunywa maziwa kikombe kikubwa cha karibia 1/2 lita bila kitafunwa.

Mchana embe dodo mdondo au ndizi 2 mbivu au mafenesi

Jioni mboga ya majani mchicha/tembele , samaki wa kukaanga au nyama au kuku

Ukiweza kutokula usiku ni nzuri zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwenye maziwa uweke chia seed ama habat soda ama mlonge
U will thank me later

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh labda yawafaa wenye kupunguza uzito ama mahitaji maalumu

nadhani makundi yote ya vyakula yana faida cha msingi 'kiasi'
Unatumia kiasi gani?.!
 
Mwenzenu diet ishanishinda mkuu but I real wish to have diet, what should I do?
 
Back
Top Bottom