Jiko la mkaa laua tena Njombe ni baada ya mwingine kulala na jiko kwenye kibanda cha biashara

Edita Mangita (40) mkazi wa mtaa wa Matema kata ya Maguvani mjini Makambako amefariki dunia baada ya kujifungia na jiko la mkaa Katika kibanda chake cha biasahara.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamisi Issa amesema tukio hilo limetokea Julai 28,2021 ambapo marehemu Edita aliamua kubaki na kulala katika kibada chake cha biashara Ili kuwahi wateja wake wa asubuhi.

Aidha kamanda Issa amewataka wananchi wa mkoa wa Njombe kuacha kulala na majiko ya mkaa ndani huku akitoa wito kwa wataalamu wa afya kuendelea kutoa elimu kuhusu madhara hayo Ili jamii.

Hivi karibuni mjini Njombe kulitokea kifo cha watu wawili wapenzi baada ya kulala na jiko la mkaa ili kupunguza baridi katika chumba chao.

Kamanda Issa ametaja tukio lingine la mwanamke mmoja Imelda Mgeni ametelekeza mtoto mwenye umri wa miezi mitatu kwa mume wake naye kwenda kusikojulikana.
Huko Njombe hatuna namna ni kuanza kujenga nyumba na kuweka AC la sivyo tutazika wengi maana jamii kubwa haielewi kwamba mkaa ni majanga,usipokufa unaamka full uchovu.
 
Kwa hii nchi yetu sijui labda azaliwe mwingine
Tanesco na Serikali ilitakiwa wa sort mikoa na Wilaya zenye baridi Ili wawe wanawauzia watu umeme kwa bei ndogo msimu wa baridi ambao huanza mwezi wa 5 hadi 8 Ili kuwasaidia kukabiliana na baridi,majengo yao yawe na mifumo ya kukabili baridi.
 
Edita Mangita (40) mkazi wa mtaa wa Matema kata ya Maguvani mjini Makambako amefariki dunia baada ya kujifungia na jiko la mkaa Katika kibanda chake cha biasahara.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamisi Issa amesema tukio hilo limetokea Julai 28,2021 ambapo marehemu Edita aliamua kubaki na kulala katika kibada chake cha biashara Ili kuwahi wateja wake wa asubuhi.

Aidha kamanda Issa amewataka wananchi wa mkoa wa Njombe kuacha kulala na majiko ya mkaa ndani huku akitoa wito kwa wataalamu wa afya kuendelea kutoa elimu kuhusu madhara hayo Ili jamii.

Hivi karibuni mjini Njombe kulitokea kifo cha watu wawili wapenzi baada ya kulala na jiko la mkaa ili kupunguza baridi katika chumba chao.

Kamanda Issa ametaja tukio lingine la mwanamke mmoja Imelda Mgeni ametelekeza mtoto mwenye umri wa miezi mitatu kwa mume wake naye kwenda kusikojulikana.
Waliofariki njombe sio wapenzi walikuwa wanasaidiana nauli
 
Back
Top Bottom