Jiko la mkaa laua tena Njombe ni baada ya mwingine kulala na jiko kwenye kibanda cha biashara

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Edita Mangita (40) mkazi wa mtaa wa Matema kata ya Maguvani mjini Makambako amefariki dunia baada ya kujifungia na jiko la mkaa Katika kibanda chake cha biasahara.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamisi Issa amesema tukio hilo limetokea Julai 28,2021 ambapo marehemu Edita aliamua kubaki na kulala katika kibada chake cha biashara Ili kuwahi wateja wake wa asubuhi.

Aidha kamanda Issa amewataka wananchi wa mkoa wa Njombe kuacha kulala na majiko ya mkaa ndani huku akitoa wito kwa wataalamu wa afya kuendelea kutoa elimu kuhusu madhara hayo Ili jamii.

Hivi karibuni mjini Njombe kulitokea kifo cha watu wawili wapenzi baada ya kulala na jiko la mkaa ili kupunguza baridi katika chumba chao.

Kamanda Issa ametaja tukio lingine la mwanamke mmoja Imelda Mgeni ametelekeza mtoto mwenye umri wa miezi mitatu kwa mume wake naye kwenda kusikojulikana.
 
Kwa baridi ya Njombe ilivyo itaendelea kuchukua roho za watu kila siku.

Nimeona fursa ambayo mwenye pesa anaweza kuwekeza kule nayo ni kujenga mifumo ya joto (heater) ndani ya nyumba. Hii itasaidia watu kuachana na majiko ya mkaa.
TANESCO mnaweza kushirikiana na wanao ishi nchi zenyebaridi sana ili kuangalia namna ya kuleta uwekezaji utakao tatua swala hilo. Msikalie kuongeza gharama tu
 
Kuna baridi sana njombe! Usipoangalia korodn zinapotelea tumboni! Ujinga mwingine wa kule ni chawa!

Usipokuwa makini iringa na njombe unaweza kumsalimia mtoto shikamo mzee kumbe kichwani yanayoonekana meupe ni mayai ya chawa.
Tuwaombee tu kwakweli!
Mkuu tuombe radhi sio kweli hata kidogo

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
kuna video niliona sijui ni njombe au makete, nguo zilizoanikwa zimeganda kwa barafu
Hiyo itakuwa ni Makete moja hiyo! Huko ni kawaida wakati wa msimu wa baridi kama huu kukuta theluji imetapakaa kwenye majani na miti majira ya asubuhi.

Kuhusu hivyo vifo, nadhani elimu iendelee kutolewa badala ya viongozi kutoa matamko tu ya kukemea.
 
Kwa baridi ya Njombe ilivyo itaendelea kuchukua roho za watu kila siku.

Nimeona fursa ambayo mwenye pesa anaweza kuwekeza kule nayo ni kujenga mifumo ya joto (heater) ndani ya nyumba. Hii itasaidia watu kuachana na majiko ya mkaa.
Wakati huo TANESCO wanakuwa wapi na bili zao hizo hahaaaaa! Labda iwe ya solar
 
Edita Mangita (40) mkazi wa mtaa wa Matema kata ya Maguvani mjini Makambako amefariki dunia baada ya kujifungia na jiko la mkaa Katika kibanda chake cha biasahara.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamisi Issa amesema tukio hilo limetokea Julai 28,2021 ambapo marehemu Edita aliamua kubaki na kulala katika kibada chake cha biashara Ili kuwahi wateja wake wa asubuhi.

Aidha kamanda Issa amewataka wananchi wa mkoa wa Njombe kuacha kulala na majiko ya mkaa ndani huku akitoa wito kwa wataalamu wa afya kuendelea kutoa elimu kuhusu madhara hayo Ili jamii.

Hivi karibuni mjini Njombe kulitokea kifo cha watu wawili wapenzi baada ya kulala na jiko la mkaa ili kupunguza baridi katika chumba chao.

Kamanda Issa ametaja tukio lingine la mwanamke mmoja Imelda Mgeni ametelekeza mtoto mwenye umri wa miezi mitatu kwa mume wake naye kwenda kusikojulikana.
Ninafahamu adha inayowapata ndugu zetu wa kanda hizo kutokana na baridi. Lakini, huwa pia ninajiuliza, huwa hii misiba ya namna hii huwa haisikiki ili wengine wachukue tahadhari? Mbona vipo vitu vingi tu ambavyo tungependa tuvifanye au tupate lakini tunaviacha kabisa ama tunafanya kwa tahadhari kutokana na hatari inayoweza kutokea?
 
Back
Top Bottom