Jiji limemshinda William Lukuvi?

Uchafu uliokithiri jijini,
Msongamano wa magari unaokera,
Ongezeko la Ombaomba Barabarani,
Kuongezeka kwa watu wanaofanya biashara kwenye maeneo mbalimbali kiholela mfano Manzese, na sehemu kadhaa za barabarani
Pamoja na mengine mengi....Ni ishara kuwa Jiji hili limemshinda Mheshimiwa huyu ambaye pia ni mbunge wa Isimani?


Ha ha ha ha. Ni mmoja wa wale waliotajwa katika kile kitabu cha mafisadi wa elimu!! Ngoja ni break kidogo nirudi ninukuu wasifu wake toka ndani ya kile kitabu nitumbukize hapa!!
 
Ha ha ha ha. Ni mmoja wa wale waliotajwa katika kile kitabu cha mafisadi wa elimu!! Ngoja ni break kidogo nirudi ninukuu wasifu wake toka ndani ya kile kitabu nitumbukize hapa!!

Kuleta ya kwene kitabu ni kutafuta majawabu rahisi kwa maswali magumu. Hakuna uhusiano.
 
ila kama wananchi wa Dar es salaam tupo "comfortable/relaxed" /tunafurahia hali hii, hakuwezi tokea miujiza.
historia inaonyesha changes nyingi zinatokana na wananchi kutoridhishwa na mifumo mibovu na ya kinyonyaji na hivyo kuonyesha kwa vitendo kutoridhishwa huko. iwe kwa maandamano, migomo au namna yoyote ile.

inaonekana hapa Dar everybody is happy, watu wanalalamika chinichini tu oooh mara Lukuvi, oooh mara diwani, ooooh mara meya nk. siku zinakwenda na watu wanajinafasi na wananawili na wanazidi kujijenga. mwisho wa siku wanakuwa hawakamatiki kwani wameshaiba vya kutosha
Hatujaridhika mkuu na Ndio maana tumeanza kwa kupaza sauti zetu kupitia JAMII FORUM na hii ni kuonyesha kuwa tumechoka.Naamini wahusika wameshasikia haya yote lakini wakiweka pamba masikioni wajue kila kitu kina mwanzo na mwish.Ipo siku ambayo Hatua za juu kutoka kwa wananchi zitachukuliwa.
 
Tatizo sio Lukuvi ila ni miundo mbinu ya siku nyingi toka wakati ule wa ukoloni mpaka leo bado yanafanya yale yale pamoja na kuongezeka kwa watu katika dar lakini hakuna barabara za kutosha na vitu kama hivyo, sio Lukuvi ni utaratibu mbaya wa serikali na mambo yake

Tujikune tunapoweza basi kuliko kulaumu miundombinu.Hata matakataka yanayotupwa jiji zima nayo yanahitaji miundombinu mipya?
 
Hatujaridhika mkuu na Ndio maana tumeanza kwa kupaza sauti zetu kupitia JAMII FORUM na hii ni kuonyesha kuwa tumechoka.Naamini wahusika wameshasikia haya yote lakini wakiweka pamba masikioni wajue kila kitu kina mwanzo na mwish.Ipo siku ambayo Hatua za juu kutoka kwa wananchi zitachukuliwa.

sina hakika na hili ila nafikiri uchafu kwa kiasi kikubwa unachangiwa na wenyeji wa mji furani
mfano, watu wanaongelea miji ya Arusha, Mwanza, Dodoma Moshi, Iringa, Mbeya nk kuwa ni misafi, lakini miji mingi ya ukanda wa Pwani sina hakika na Tanga, kuna tatizo. hapa dar kuna mitaa iliyojaa "wenyeji" na "walowezi" kuna uchafu ulio kithiri na watu hawajali, wapo comfortable na hata bei za kupanga zipo juu ilhali kuna mitalo ya maji machafu inapita hapo inatoa harufu kali.
sina hakika labda kufanya research
 
Kuleta ya kwene kitabu ni kutafuta majawabu rahisi kwa maswali magumu. Hakuna uhusiano.

Sawa mkuu ila hapa jamvini verification/proof/triangulation/validation ni muhimu sana ili tusisumbukue kujadili kwa nini jamaa kashindwa jiji. Simple, hana uwezo!!! hivyo usuhsiano upo!! Refer Causal Relationships in Econometrics !!!!! Google it if you have not done Econometrics!!!
 
Tatizo la hawa viongozi ni kwamba kila anayekuja anaanzisha operesheni zake. Hakuna operesheni ama mipango maalum na endelevu ya Jiji. Kama ipo basi haifanyiwi kazi ipasavyo.
 
Kumbe ni kamradi kamebuniwa ka kuinuana wakati jiji linazidi kudidimia kila siku.Shame on us!

Ni kamradi fulani ndani ya system yao, kuna mkuu mmoja wa wilaya alilalamika kupelewa wilaya iliyo pembezoni mbali na kwao wakati umri wa k-retire umefika,jibu alilopewa ni kwamba wanamtayarishia mafao manene ya kumsafirisha yeye na famila yake atakapoacha kazi mpaka kumfikisha kwao, akauona ukweli huo,akaripoti na baada ya miezi minne akaacha kazi
 
Jiji limewashinda wote... uongozi wa Jiji.. manispaa, Viongozi na wakaazi woote.. wa kulaumiwa ni serikali amabayailiacha kuzingatia umuhimu wa kazi za wataalam mipango miji( amabo wanatengeneza master plans) na kuitekeleza kwa wakati tangu miaka ya nyuma. Laiti zingezingatiwa leo hii kusingewa na msongamano ambao haudhibitiki.. isingeingia gharama kubwa kufidia na kuhamisha wananchi; na ingerahisisha uwiano mzuri wa mgawanyo wa huduma mabilimbali ndani ya jiji. hii la usafi vilevile lingewezekana kutatuliwa.

Zaidi ya asilimia 70 ya jiji ni makazi holela..hata zikiwekwa pipa za taka mitaani...zitaondelewaje wakati maeneo mengi yanafikika kwa taab na magari taka? Manispaa za Mwanza na Moshi znasifika kwa usafi wamejizatiti kwa mipangilio ya mji yao.

Mwacheni Lukuvi aendelee kung'aa na pamba zake bana!!

Kalaghabaho!!
 
Kwani Lukuvi ni Meya? He has more on his plate than the city of Dar-es-Salaam
 
Tatizo wananchi wenyewe wa jiji la Dar ni wachafu Lukuvi ataweza wapi?? huko mitaani kwenu,,mnamwaga takataka barabarani halafu mnamlaumu Lukuvi unataka yeye aje akuonyeshe jinsi ya kutunza taka?? Jipangeni wenyewe kwenye mitaa yenu halafu ndipo muone kama kutakua na uchafu....angalieni moshi kule ukitema mate tu ovyo jirani yako anakushitaki serikali za mitaaa
 
Uchafu uliokithiri jijini,
Msongamano wa magari unaokera,
Ongezeko la Ombaomba Barabarani,
Kuongezeka kwa watu wanaofanya biashara kwenye maeneo mbalimbali kiholela mfano Manzese, na sehemu kadhaa za barabarani
Pamoja na mengine mengi....Ni ishara kuwa Jiji hili limemshinda Mheshimiwa huyu ambaye pia ni mbunge wa Isimani?

Mimi nadhani jiji limetushinda sisi wakazi wa Dar, kuna mambo ambayo watawala wanaweza kuyafanya ila mengine ni sisi tuishio jijini. Mfano utakuta mtu anakula miwa katika basi anatupa taka hovyo, machupa ya maji yanatupwa hovyo nk. Nadhani ukifanyika utafiti kuangalia jinsi wakazi wa jiji hili wanavyoishi majumbani mwao itakuwa ni vituko tu, nahisi kuna wengine hata mashuka hawafui, hawatandiki vitanda, neti za kuzuia mbu chafu etc.

Kuhusu foleni nadhani mamlaka zinahusika, ingawa sioni suluhisho la haraka kwani miundo mbinu yenyewe haikidhi mahitaji, mfano asubuhi wote mtaelekea aidha mjini (posta) au kariakoo, jioni wote mtatoka aidha mjini (posta) au kariakoo foleni inakuwa njia moja siku zote unless kuwe na msafara wa kiongozi!
 
Tatizo wananchi wenyewe wa jiji la Dar ni wachafu Lukuvi ataweza wapi?? huko mitaani kwenu,,mnamwaga takataka barabarani halafu mnamlaumu Lukuvi unataka yeye aje akuonyeshe jinsi ya kutunza taka?? Jipangeni wenyewe kwenye mitaa yenu halafu ndipo muone kama kutakua na uchafu....angalieni moshi kule ukitema mate tu ovyo jirani yako anakushitaki serikali za mitaaa

Bravo Mnyakyusa! tubadilike sisi kwanza, haingii akilini mbwa/paka anagongwa na gari mtaani, kila mtu akipita anaangalia pembeni mpaka mzogo unaanza kutoa harufu halafu unasema Lukuvi!
 
mimi sikatai kuwa sehemu ya mabadiliko,lakini tunachoongelea hapa ni UCHAFU/KERO za jiji na Responsibilities za mkuu wa koa,Mameya na Wakurugenzi wa Manispaa.
__________________

Charity nakupongeza kwa uelewa wako - KUNYWA JUICE BARIDI KWA NIABA YANGU - KWA HILI TUKO PAMOJA


 
Lukuvi asilaumiwe kwa matatizo ya jiji ,mfumo wa sasa wa manispaa tatu kila moja na utawala wake kamili na jiji na ofisi ya mkuu wa mkoa inakuwa kama kambare hakuna mdogo wote wana masharubu na kila manispaa inapanga mambo yake ni vizuri jiji likaundwa upya kwa kuweka mfumo mzuri na kulifanya kuwa madaraka na mapato ya kutosha kutokana na vianzia vilivyopo katika jiji mfano bandari ili liweze kutoa huduma muhimu kwa jiji lote na kuboresha miundombinu na mamlaka zinazotoa huduma kama dawasa, tanesco na tanroad mkoa wa dar .ni vizuri ziwe coordinated na jiji na mtendaji wake mkuu apewe meno ya kutosha na kuwe na masterplan itakayo ongoza ukuaji wa dar kwani kwa sasa iliyopo imeshakwisha muda wake.
Hivi tunavyobwabwaja humu ndani tunajua vizuri job description ya RC?
 
Mimi naona sisi hatujui hata kidogo kazi za RC na majukumu yake katika jamii
Josh hebu tujuze vyema kazi na majukumu ya RC.
ILA MIMI nilizani kazi yake inajumuisha usimamizi wa shughuli zote za maendeleo ya mkoa husika, kusimamia ulinzi na usalama kikamilifu, kusimamia Usafi na mazingira ya mkoa husika, kuwa msemaji mkuu wa shughuli za kiserikali katika mkoa aliopo.
sasa tumpime kaka Lukuvi a.k.a mr UPPE, je tangu amefika amesimamia lipi hasa hapa Jijini Dar ? je anaweza kufikia hata nusu ya utendaji wa makamba ama Kandoro ?
 
Mi naona unamuonea Lukuvi bure. Labda utuambie ni nani aliyelimudu. Makamba? Ditopile?Kandoro?Chipungahelo?............

Mi naona hakuna mwenye afadhali! Wote wamelishindwa kama huyu bwana mkubwa Lukuvi.

....Lowassa alitoa amri ikatekelezwa,...
I bet hata Mrema angetoa siku zake saba ingetekelezeka.
Tushazoea 'viboko' sie, bila amri hakuna kinachotekelezeka.

(pamoja na mapungufu yao) wenye amri hawapo tena madarakani.
 
Naona wapenda miujiza wanazidi kushangaa kwanini hawajapokea miujiza yao kutoka kwa 'nabii' Lukuvi. Lakini what esle can they expect wakati taratibu zote zinaenda kwa mfumo wa ajali badala ya mipango inayosimamiwa kikamilifu? Nahisi zile ajali wao ndo wanaona ni miujiza. Lakini utamkonvins vp mtu huyu aliyezoea miujiza kuwa taratibu endelevu hazitakiwi ziende hivo? Nadhani utata unaongezeka hapa.
 
Uchafu uliokithiri jijini,
Msongamano wa magari unaokera,
Ongezeko la Ombaomba Barabarani,
Kuongezeka kwa watu wanaofanya biashara kwenye maeneo mbalimbali kiholela mfano Manzese, na sehemu kadhaa za barabarani
Pamoja na mengine mengi....Ni ishara kuwa Jiji hili limemshinda Mheshimiwa huyu ambaye pia ni mbunge wa Isimani?

Hivi wananchi wake wanajisikiaje? kuwa na mbunge aliya mkuu wa mkoa dar es salaam.
 
Back
Top Bottom