Jiji limemshinda William Lukuvi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jiji limemshinda William Lukuvi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sinafungu, Mar 3, 2010.

 1. sinafungu

  sinafungu JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2010
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 1,430
  Likes Received: 577
  Trophy Points: 280
  Uchafu uliokithiri jijini,
  Msongamano wa magari unaokera,
  Ongezeko la Ombaomba Barabarani,
  Kuongezeka kwa watu wanaofanya biashara kwenye maeneo mbalimbali kiholela mfano Manzese, na sehemu kadhaa za barabarani
  Pamoja na mengine mengi....Ni ishara kuwa Jiji hili limemshinda Mheshimiwa huyu ambaye pia ni mbunge wa Isimani?
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,484
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Wadanganyika wanashangaza sana. Ndio yaleyale ya kutegemea kuvuna madafu kwa kupanda chelewa au kubisha hodi kwene picha ya mlango.

  Yaani ulitegemea Lukuvi out of his sleeves atafanya kitu flani siku moja and voila msongamano wa magari utatoeka, au uchafu utapotea kimiujiza, au ombaomba watageuka ghafla kuwa Bill Gates, au vibanda uchwara vya machinga vitageuka shopping malls za kufa mtu...?

  Lakini wa kumlaumu ni nani ikiwa wenyewe ni sisi na tuna mawazo kaa haya ya kusubiria miujiza kutoka kwa nabii Lukuvi??
   
 3. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 54,214
  Likes Received: 31,322
  Trophy Points: 280
  Mi naona unamuonea Lukuvi bure. Labda utuambie ni nani aliyelimudu. Makamba? Ditopile?Kandoro?Chipungahelo?............

  Mi naona hakuna mwenye afadhali! Wote wamelishindwa kama huyu bwana mkubwa Lukuvi.
   
 4. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,292
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  hili jiji mniachie mimi:):)
   
 5. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,935
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mimi naona huyu Lukuvi ndio limemshinda kabisaaa.Wenzake hawakuliweza lakini yeye amazidi.Jiji linanuka uvundo.ameshindwa kabisa kuwasimamia wenyeviti wa mitaa.Hata Morogoro inaishinda Dar kwa mbali sana,yani ni pasafi sana huwezi kuamini.
  Kwani mikoa mingine inaweza wana nini na yeye lukuvi anashindwa kwa nini?
   
 6. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #6
  Mar 3, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  jamani eeh, Lukuvi shule yake hamuwezeshi kufanya mambo kwa kujiamini , kwahiyo ameathiriwa na hilo, anashindwa kusimama mbele ya umma wa watu wa jiji hili na kukemea akiamini kuwa kila mtu anajua kasoro yake ya Kielimu, huyu std VII, hana ujasiri.
  hili jiji linataka watu wenye courage
   
 7. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,292
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  si ndo maana nimesema mnikabidhi mimi jamani???/!....hiyo nafasi haimfai mwingine niwekeni mimi
   
 8. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,935
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Tudhibitishie kama kweli unaweza.......
  anza kwa kuchukua fomu ya kugombea ubunge kupitia CCJ jimbo la Kinondoni.........
   
 9. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 54,214
  Likes Received: 31,322
  Trophy Points: 280
  Kwani Geoff ana ushirika na kina Lowassa?
   
 10. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #10
  Mar 3, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  kwani CCJ na Lowassa ni ndugu moja ?
   
 11. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #11
  Mar 3, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,292
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  ndiyo.nina usharika na eddo
   
 12. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #12
  Mar 3, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,011
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Hapana, Geof agombee udiowani ili baadaye achaguliwe kuwa Meya, hapo ndipo atashughulika na jiji lakini akiwa Mbunge wa Kinondoni hatoweza
   
 13. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #13
  Mar 3, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180
  Mhishimiwa Lukuvi alikuwapo Dodoma; ilimshinda pamoja na udogo wa mji ule! Kulikuwa na shimo barabarani karibu kabisa na geti la kuingilia kwenye jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa lilodumu zaidi ya mwaka mzima!
  Yaani watu wanaotakiwa kutumwa na yeye hawana hata uthubutu wa kuogopa kutotimiza wajibu wao na msimaizi hana thubutu ya kuwasimamia kutimiza wajibu wao!
   
 14. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #14
  Mar 3, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,632
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Nadhani mnamuonea mnyalukolo bure, kwani kutofukiwa kwa mashimo kwenye geti la kuingilia ofisi ya mkuu wa mkoa huko Dodoma ndio ishara kuwa alishindwa kazi? Mbona huko Bagamoyo watu wameiba mamilioni ya mapesa toka kwenye mradi wa barabara ya Msata -Bagamoyo ; na hata kwenye halmashauri yenyewe ya Bagamoyo and yet huko ndiko anakotoka mkuu wa nchi; Je kutoogopa kwa hawa mafedhuli [ DED huteuliwa na Rais] kuwa huko ndiko anatoka kiongozi wa nchi kuna maana Rais ameshindwa kutimiza wajibu wake?
   
 15. Mwamanda

  Mwamanda Senior Member

  #15
  Mar 3, 2010
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 132
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Lukuvi asilaumiwe kwa matatizo ya jiji ,mfumo wa sasa wa manispaa tatu kila moja na utawala wake kamili na jiji na ofisi ya mkuu wa mkoa inakuwa kama kambare hakuna mdogo wote wana masharubu na kila manispaa inapanga mambo yake ni vizuri jiji likaundwa upya kwa kuweka mfumo mzuri na kulifanya kuwa madaraka na mapato ya kutosha kutokana na vianzia vilivyopo katika jiji mfano bandari ili liweze kutoa huduma muhimu kwa jiji lote na kuboresha miundombinu na mamlaka zinazotoa huduma kama dawasa, tanesco na tanroad mkoa wa dar .ni vizuri ziwe coordinated na jiji na mtendaji wake mkuu apewe meno ya kutosha na kuwe na masterplan itakayo ongoza ukuaji wa dar kwani kwa sasa iliyopo imeshakwisha muda wake.
   
 16. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #16
  Mar 3, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,831
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  Geoff please!!! unataka uwekwe??? wewe si kidume? nani akuweke? au una maana gani hapa
   
 17. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #17
  Mar 3, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,935
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Sasa unataka kutuambia kuitwa mkuu wa mkoa maana yake nini? hao wakuu wa wilaya si wote wanaripoti kwake? ndio maana hata akisafiri mkuu wa wilaya mmojawapo anakaimu nafasi yake.na nijuavyo mimi ukija kwenye masuala ya Mkoa hata raisi yupo chini ya serikali ya mkoa.
  msitake kutetea upuuzi.Jiji limeoza linanuka na all the blame ni kwa Lukuvi na hao wenzie walioondoka.
   
 18. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #18
  Mar 3, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,484
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Tuko ukarasa mmoja.

  Blame the damn system!!

  . Kama individual yupo sehemu fulani anaboronga na system haimuonyi ni wazi system ndio ipo responsible kikwazo. Mi ninavolitazama tatizo, mambo mengi yameenda kombo kutokana na planning. Kwamba wapangaji walilala hapa katikati au hawakueka projections za kisayansi.
   
 19. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #19
  Mar 3, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,935
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Hapana haonewi.Sio lazima akoroge lami kwa mikono yake ila alishindwa kusimamia wa chini yake kulifukia shimo hilo.na hii inaonyesha kuwa mambo madogo yaliyopo mlangoni anashindwa itakuwaje mambo makubwa kama jiji la Dar?
   
 20. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #20
  Mar 3, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,831
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  Kuna mamatizo matatu hapa

  • la kwanza ni uwezo wa lukuvi akiwa kama lukuvi, hili nadhani liko wazi kwamba lukuvi hana ile calliber ya kuongoza miji yenye matatizo kama Dar, ni personality au elimu... i dont know
  • la pili ni ugumu wa kuongoza Dar kutokana na mfumo wake, labda hatuhitaji mkuu wa mkoa at all... tujiulize meya wa jiji letu ana kazi gani? RAS wetu ana kazi gani? polisi wamegawaje mkoa? elimu wamegawaje huu mkoa?
  • La tatu ni siasa kuwepo kila sehemu hata pasipostahili, siku hizi hata magari ya usafi hayapati tender kama hakuna kaushikaji fulani na makada!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...