Jiji la Tanga laeleza namna vitambulisho vya wajasiriamali vilivyosababisha kukosa mapato

Super Handsome

JF-Expert Member
Jul 16, 2013
3,846
6,439
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Selebosi akisisitiza jambo wakati wa kikao cha baraza la Madiwani cha kuwasilisha taarifa ya utendaji wa kata kulia ni
Kaimu Mkurugenzi Ramadhani Possi

HALMASHAURI ya Jiji la Tanga imeeleza namna vitambulisho vya wajasiriamali vilivyotolewa na Rais John Magufuli vilivyowasababishia kukosa mapato huku vyanzo vyake vya mapato 15 kufutika na hivyo kushindwa kutekeleza miradi ya maendeleo.

Kauli hiyo aliitoa na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Selebosi wakati wa kikao cha baraza la Madiwani cha kuwasilisha taarifa ya utendaji wa kata kilichofanyika Jijini hapa na kusema hali ya Halmashauri imekuwa mbaya kutokana na vitambulisho hivyo kugawiwa kwa wafanyabiashara wasio walengwa.

Alisema kuwa Jiji hilo lilikuwa na jumla ya vyanzo vya mapato 38 ambavyo vilikuwa vinatarajiwa kuliingiza Halimashauri hiyo bajeti ya Bil 15 lakini ugawaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara wasio stahiki imesababisha kasoro hiyo.

Alidai chanzo cha kupelekea hali hiyo kimesababishwa na Watendaji wa kata na Mitaa kwa kushindwa kusimamia kwa ukaribu ugawaji wa vitambulishi hivyo kwa watu wanaostahili na badala yake wamewagawiwa hata wafanyabiashara wasihusika.

“Watendaji mmetuangusha mmegawa vitambulisho hata kwa wafanyabiashara wasiostahili na mmefanya hivyo ili kuvimaliza lakini ni athari kwetu hasa Halmashauri hatuna fedha na miradi mingi itakwama”Alisema Seleboss.

Aidha alisema watendaji wamechangia kukwamisha ukusanyaji wa mapato ambapo yamefikia asilimia 65% huku ikiwa bado mwezi mmoja kumalizika kwa mwaka wa serikali uishe ilihali angalau ukusanyaji huo ulitakiwa ufikie 80%.

Alisema kuwa ukosefu huo wa mapato umesababisha Halimashauri hiyo kushindwa kutekeleza shughuli za kijamii kama usafi wa masoko pamoja na marekebisho ya taa za barabarani.
“Watendaji wameshindwa kutafsiri nia ya Rais kwani vitambulisho vimetolewa hadi kwa wavuvi pamoja na wafanyabiashara wakubwa wenye maduka sasa wote wamegeuka na kuwa wajasiriamali”alisema Mustafa.

Hata hivyo akiongelea upande wa leseni za biashara Meya Mustafa alisema kuwa wamepoteza mapato ya kiasi cha sh Mil 700 zilizokuwa zikusanywe kutokana na maombi ya leseni hizo lakini sasa wafanyabiashara wengi wamerudisha leseni hizo na kukata vitambulisho vya wajasiriamali.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Ramadhani Possi alisema kuwa ufinyu wa bajeti umesababisha miradi mingi ambayo walikuwa wamepanga kuitekeleza kushindwa kutekelezwa kwa wakati .

“Kwa sasa tunajipanga kuboresha miundombinu ya shule zetu kwa kujenga madarasa mapya ukarabati ya vyoo pamoja na madawati ambapo tunafanya kila pale tunapopata fedha japo kidogo”alisema Possi.
Kaimu Mkuu wa wilaya ya Tanga Selemani Zumo aliwataka watendaji wa Jiji kuhakikisha wanafanyakazi kwa uwadilifu na kujituma pamoja na kujua mipaka ya kazi zao.
Alisema kuwa haiwezekani watendaji hao wakawa ni sehemu ya migogoro baina yao na viongozi wa kisiasa ambao wao wapo kwa ajili ya kuhakikisha wanasimami maslahi ya wananchi ambao ni wapiga kura wao.
Awali akichangia mada katika baraza hilo Diwani wa kata ya Mabawa Mwasabu Ngare alisema baadhi ya taa za barabarani haziwaki na hali hiyo inaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la vibaka na wananchi kupoteza mali zao.

Mjume hauwawi!
Nawasilisha!
 
Attachments

  • selebosi.JPG
    selebosi.JPG
    103.2 KB · Views: 23
Msitafute visingizio. Kama mmeshindwa kuuza vitambulisho mnalo hilo litakukabeni hadi yawatoke ya kuwatoka.
 
Mfanyabiashara mkubwa anapiga hesabu
Leseni atalipia fedha kadhaa
Akiwapata vijana watatu/wanne, akawanunulia vitambulisho pamoja na posho inakuwa chini ya kodi kwa mwaka.
Basi amarudisha leseni na biashara inaendelea.
Huko ni Tanga. Najua ni sehemu nyingi kuna hili janga
 
Jiwe anafundishwa practical business management 101.
 
Mzee wa kukurupuka ametulia tu anasubiri kutumbua watakaoshindwa kutekeleza agizo lake
Kuna mmoja huko tabora,amekamata wabibi na wabubu wauza ugoro ,kaenda kuwasweka ndani akidai kwanini hawakati vitambulisho.
Kilichomkuta nasikia kakutwa kalala nje kapakatwa na wanyama wawili aina ya fisi na hadi sasa hali yake sionzuri.
 
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Selebosi akisisitiza jambo wakati wa kikao cha baraza la Madiwani cha kuwasilisha taarifa ya utendaji wa kata kulia ni
Kaimu Mkurugenzi Ramadhani Possi

HALMASHAURI ya Jiji la Tanga imeeleza namna vitambulisho vya wajasiriamali vilivyotolewa na Rais John Magufuli vilivyowasababishia kukosa mapato huku vyanzo vyake vya mapato 15 kufutika na hivyo kushindwa kutekeleza miradi ya maendeleo.

Kauli hiyo aliitoa na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Selebosi wakati wa kikao cha baraza la Madiwani cha kuwasilisha taarifa ya utendaji wa kata kilichofanyika Jijini hapa na kusema hali ya Halmashauri imekuwa mbaya kutokana na vitambulisho hivyo kugawiwa kwa wafanyabiashara wasio walengwa.

Alisema kuwa Jiji hilo lilikuwa na jumla ya vyanzo vya mapato 38 ambavyo vilikuwa vinatarajiwa kuliingiza Halimashauri hiyo bajeti ya Bil 15 lakini ugawaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara wasio stahiki imesababisha kasoro hiyo.

Alidai chanzo cha kupelekea hali hiyo kimesababishwa na Watendaji wa kata na Mitaa kwa kushindwa kusimamia kwa ukaribu ugawaji wa vitambulishi hivyo kwa watu wanaostahili na badala yake wamewagawiwa hata wafanyabiashara wasihusika.

“Watendaji mmetuangusha mmegawa vitambulisho hata kwa wafanyabiashara wasiostahili na mmefanya hivyo ili kuvimaliza lakini ni athari kwetu hasa Halmashauri hatuna fedha na miradi mingi itakwama”Alisema Seleboss.

Aidha alisema watendaji wamechangia kukwamisha ukusanyaji wa mapato ambapo yamefikia asilimia 65% huku ikiwa bado mwezi mmoja kumalizika kwa mwaka wa serikali uishe ilihali angalau ukusanyaji huo ulitakiwa ufikie 80%.

Alisema kuwa ukosefu huo wa mapato umesababisha Halimashauri hiyo kushindwa kutekeleza shughuli za kijamii kama usafi wa masoko pamoja na marekebisho ya taa za barabarani.
“Watendaji wameshindwa kutafsiri nia ya Rais kwani vitambulisho vimetolewa hadi kwa wavuvi pamoja na wafanyabiashara wakubwa wenye maduka sasa wote wamegeuka na kuwa wajasiriamali”alisema Mustafa.

Hata hivyo akiongelea upande wa leseni za biashara Meya Mustafa alisema kuwa wamepoteza mapato ya kiasi cha sh Mil 700 zilizokuwa zikusanywe kutokana na maombi ya leseni hizo lakini sasa wafanyabiashara wengi wamerudisha leseni hizo na kukata vitambulisho vya wajasiriamali.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Ramadhani Possi alisema kuwa ufinyu wa bajeti umesababisha miradi mingi ambayo walikuwa wamepanga kuitekeleza kushindwa kutekelezwa kwa wakati .

“Kwa sasa tunajipanga kuboresha miundombinu ya shule zetu kwa kujenga madarasa mapya ukarabati ya vyoo pamoja na madawati ambapo tunafanya kila pale tunapopata fedha japo kidogo”alisema Possi.
Kaimu Mkuu wa wilaya ya Tanga Selemani Zumo aliwataka watendaji wa Jiji kuhakikisha wanafanyakazi kwa uwadilifu na kujituma pamoja na kujua mipaka ya kazi zao.
Alisema kuwa haiwezekani watendaji hao wakawa ni sehemu ya migogoro baina yao na viongozi wa kisiasa ambao wao wapo kwa ajili ya kuhakikisha wanasimami maslahi ya wananchi ambao ni wapiga kura wao.
Awali akichangia mada katika baraza hilo Diwani wa kata ya Mabawa Mwasabu Ngare alisema baadhi ya taa za barabarani haziwaki na hali hiyo inaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la vibaka na wananchi kupoteza mali zao.

Mjume hauwawi!
Nawasilisha!
Asante
 
For what I know kila aliyepewa kitambulisho amesajiliwa kwa jina, aina ya biashara, kiasi cha mauzo kwa siku, namba yake ya simu, kijiji pamoja na kata anayotokea. Kwahyo kama kuna wafanya biashara waliotoa taarifa feki inabidi wafatwe wanyangaywe vitambulisho na wafunguliwe mashitaka. Tatzo ni kufanya maamuzi bila kutoa semina elekezi kwa watendaji. Sasa mara inabidi mauzo yako kwa mwaka yasizidi milioni nne, mtendaji mwingine anakwambia mtaji wako usiwe unazidi milioni nne, yani kiukweli watawalaumu bule watendaji ila nao awajui walitendalo.
 
Back
Top Bottom