Udhaifu wa zoezi la sensa jijini Mwanza umeingia hatua nyingine tofauti na ya jana ya kuchelewesha malipo ya makarani wa sensa iliyowekwa hapa.
Udhaifu huo wa jana haukuishia kufanya makarani wachelewe kupatiwa posho yao ya kuanzia kufanya sensa, lakini pia hawakupewa sare yaani utambulisho utakaowarahisishia kujulikana na kupokelewa majumbani.
Matokeo yake ni kwamba, makarani wameenda nyumba hadi nyumba huku hawana sare na hivyo kufanywa wafukuzwe na baadhi kudhaniwa vibaka, majambazi au machangudoa. Hivyo, si tu kwamba wamekataliwa sehemu nyingi bali pia wamefukuzwa kwa vitisho kadhaa kwa kuelezwa wazi kwamba kuingia eneo la mtu bila kitambulisho au sare ukjifanya wewe ni karani wa sensa.
Hivyo, inaweza kutoka picha kwamba Mwanza wamegoma kuhesabiwa lakini ukweli ni kwamba maafisa wengi hawana sare kama ilivyo kwa mikoa mingine na kwa hili wananchi wa Mwanza wana haki ya kulinda miji yao isivamiwe na mtu asiyejulikana kwa kisingizio cha kuwa karani wa sensa.