Jiji la Mwanza ndilo jiji kubwa kabisa lenye kiwanja cha ndege chenye hadhi duni dunia nzima

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
May 30, 2017
2,869
3,188
Usafiri wa anga ni mojawapo ya kipimo na kigezo kikubwa cha jiji kuwa la kimataifa. Hata hivyo, siyo majiji yote makubwa duniani (yenye wakazi angalao kuanzia 600,000) yana "viwanja vya ndege vya kimataifa" kutokana na kuwa karibu sana na majiji yenye viwanja vya hadhi ya juu.

Mfano: Eneo la Ruhr nchini Ujerumani lina majiji mengi ya Cologne, Düsseldorf, Duisburg, Dortmund na Essen, Bochum, Gelsenkirchen, Wuppertal na Bonn lakini kuna viwanja vya kimataifa vitatu pekee - Düsseldorf; Cologne-Bonn na Dortmund.

Nchini Zambia, jiji la pili kwa ukubwa nchini humo Kitwe, halina uwanja kutokana na kuwa karibu (km 30) na jiji la tatu, Ndola lenye uwanja. Aidha, hata hapa Tanzania, Manispaa ya Morogoro na Mji wa Kibaha haina huduma za usafiri wa ndege kama miji mingine kutokana na kuwa karibu na Dar.

Ukiangalia kwa undani jiografia ya Tanzania, utashangaa kuona kwamba Dar (Mwalimu Nyerere) na Zanzibar (Abeid Karume) pamoja na KIA na hivi karibuni Mbeya (Songwe), vina viwanja vizuri vyenye majengo ya abiria mazuri kuliko uwanja wa Mwanza, unaowakilisha na kituo kikuu cha Kanda ya Ziwa, huku ukiwa kiunganishi kikuu cha Bukoba, Musoma, Shinyanga, Geita, Bariadi, Kahama na Kigoma na hata Tabora.

Hebu hata nyie fikirieni, jiji la Mwanza lenye wakazi wapatao 940,000 (2017) linaunganisha wakazi zaidi ya milioni 16 (kwa sensa ya 2012), ambao ni wengi kuliko nusu ya nchi (nchi zipatazo 30) za barani Afrika. So jiji hili halikufaa kuwa katika hali yake hiyo kwa muda mrefu.

IMG_2239.PNG

Katika uchunguzi wangu wa muda mrefu:
  • Hakuna jiji lolote barani Afrika hata lisilo makaa makuu ya nchi na lenye watu wengi kuliko Mwanza, lenye kiwanja kibovu.
  • Hakuna jiji lolote barani Afrika hata lisilo makao makuu ya nchi, lenye wakazi wanaolingana na jiji la Mwanza, lenye kiwanja kibovu.
  • Hakuna jiji lolote barani Afrika lisilo makao makuu ya nchi lenye wakazi angalao zaidi ya 500,000 lakini lina uwanja mbaya kama wa Mwanza.
NB: Ninajua tangu 2014, kumekuwepo Mradi wa Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa lakini fedha zinazotengwa zimekuwa kidogo tangu 2014. Hivyo, anachofanya JPM, ni kuusaidia Mji huu na aibu ya kudharauliwa kwa muda mrefu.

Ifuatayo ni orodha yote ya viwanja vya ndege vya kimataifa vya majiji yenye wakazi wanaokaribiana na jiji la Mwanza, katika Bara la Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara. (Nimeweka Sub-Sahara Afrika kutokana na kwamba, mabara mengine viwanja vyao ni matawi ya juu, hata kama kamji ni kadogo).
 
Attachments

  • IMG_2243.JPG
    IMG_2243.JPG
    57.1 KB · Views: 354
  • IMG_2244.JPG
    IMG_2244.JPG
    28.7 KB · Views: 240
  • IMG_2245.JPG
    IMG_2245.JPG
    16.5 KB · Views: 311
  • IMG_2247.JPG
    IMG_2247.JPG
    11.8 KB · Views: 224
  • IMG_2248.JPG
    IMG_2248.JPG
    67.8 KB · Views: 214
  • IMG_2249.PNG
    IMG_2249.PNG
    88.8 KB · Views: 215
  • IMG_2255.JPG
    IMG_2255.JPG
    87.7 KB · Views: 214
  • IMG_2257.JPG
    IMG_2257.JPG
    6.6 KB · Views: 270
  • IMG_2258.JPG
    IMG_2258.JPG
    30.6 KB · Views: 186
  • IMG_2261.JPG
    IMG_2261.JPG
    22.3 KB · Views: 272
  • IMG_2264.JPG
    IMG_2264.JPG
    67.4 KB · Views: 219
  • IMG_2265.JPG
    IMG_2265.JPG
    52.8 KB · Views: 301
  • IMG_2267.JPG
    IMG_2267.JPG
    12.7 KB · Views: 339
  • IMG_2272.JPG
    IMG_2272.JPG
    52.3 KB · Views: 288
  • IMG_2273.PNG
    IMG_2273.PNG
    41 KB · Views: 197
  • IMG_2276.JPG
    IMG_2276.JPG
    24.4 KB · Views: 348
  • IMG_2293.JPG
    IMG_2293.JPG
    58.2 KB · Views: 197
Watu wa Mwanza mmeambiwa pale Kigongo ferry panajengwa daraja ili kurahisisha usafiri kutoka Chato International Airport uwanja wa Mwanza siyo wa muhimu sana kwa sasa
 
Chato international airport kinatosha...hamna haja ya kuharibu rasimali nyingi za nchi namna hii.

Kuna mikoa baadhi ya maeneo hamna hata dispensary.. wamama wajawazito na wagonjwa wengi wanatembea kilometa nyingi kutafuta huduma ya afya. Hela zielekezwe huko ndiko.kunakohitajika zaidi.

Ukiulizwa katika population yote ya mwanza ni percent ngapi ya wananchi wanatumia usafari wa anga sina uhakika kama hata inafika 0.001%..

Sasa kwanin hela isielekezwe penye uhitaji mkubwa
 
Usafiri wa anga ni mojawapo ya kipimo na kigezo kikubwa cha jiji kuwa la kimataifa. Hata hivyo, siyo majiji yote makubwa duniani (yenye wakazi angalao kuanzia 600,000) yana "viwanja vya ndege vya kimataifa" kutokana na kuwa karibu sana na majiji yenye viwanja vya hadhi ya juu. Mfano: Eneo la Ruhr nchini Ujerumani lina majiji mengi ya Cologne, Düsseldorf, Duisburg, Dortmund na Essen, Bochum, Gelsenkirchen, Wuppertal na Bonn lakini kuna viwanja vya kimataifa vitatu pekee - Düsseldorf; Cologne-Bonn na Dortmund.
Nchini Zambia, jiji la pili kwa ukubwa nchini humo Kitwe, halina uwanja kutokana na kuwa karibu (km 30) na jiji la tatu, Ndola lenye uwanja. Aidha, hata hapa Tanzania, Manispaa ya Morogoro na Mji wa Kibaha haina huduma za usafiri wa ndege kama miji mingine kutokana na kuwa karibu na Dar.
Ukiangalia kwa undani jiografia ya Tanzania, utashangaa kuona kwamba Dar (Mwalimu Nyerere) na Zanzibar (Abeid Karume) pamoja na KIA na hivi karibuni Mbeya (Songwe), vina viwanja vizuri vyenye majengo ya abiria mazuri kuliko uwanja wa Mwanza, unaowakilisha na kituo kikuu cha Kanda ya Ziwa, huku ukiwa kiunganishi kikuu cha Bukoba, Musoma, Shinyanga, Geita, Bariadi, Kahama na Kigoma na hata Tabora.
Hebu hata nyie fikirieni, jiji la Mwanza lenye wakazi wapatao 940,000 (2017) linaunganisha wakazi zaidi ya milioni 16 (kwa sensa ya 2012), ambao ni wengi kuliko nusu ya nchi (nchi zipatazo 30) za barani Afrika. So jiji hili halikufaa kuwa katika hali yake hiyo kwa muda mrefu.

Katika uchunguzi wangu wa muda mrefu:
  • Hakuna jiji lolote barani Afrika hata lisilo makaa makuu ya nchi na lenye watu wengi kuliko Mwanza, lenye kiwanja kibovu.
  • Hakuna jiji lolote barani Afrika hata lisilo makao makuu ya nchi, lenye wakazi wanaolingana na jiji la Mwanza, lenye kiwanja kibovu.
  • Hakuna jiji lolote barani Afrika lisilo makao makuu ya nchi lenye wakazi angalao zaidi ya 500,000 lakini lina uwanja mbaya kama wa Mwanza.
NB: Ninajua tangu 2014, kumekuwepo Mradi wa Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa lakini fedha zinazotengwa zimekuwa kidogo tangu 2014. Hivyo, anachofanya JPM, ni kuusaidia Mji huu na aibu ya kudharauliwa kwa muda mrefu.

Ifuatayo ni orodha yote ya viwanja vya ndege vya kimataifa vya majiji yenye wakazi wanaokaribiana na jiji la Mwanza, katika Bara la Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara. (Nimeweka Sub-Sahara Afrika kutokana na kwamba, mabara mengine viwanja vyao ni matawi ya juu, hata kama kamji ni kadogo).

View attachment 626045 View attachment 626053 View attachment 626054 View attachment 626055 View attachment 626056 View attachment 626057 View attachment 626059 View attachment 626060 View attachment 626061 View attachment 626062 View attachment 626063 View attachment 626064 View attachment 626065 View attachment 626066 View attachment 626067 View attachment 626068 View attachment 626069 View attachment 626071 View attachment 626077
Ahaaaaaa Hata Bukoba inaizidi mwanza
 
sawa mtafiti ngoja waje watafiti wenzako wakujibu kwa hoja.
Hiyo ambayo ningependa ili kujadili vyema pressing issues ambazo tunazioverlook kwa makusudi na kuleta aibu kubwa kwa umma wa Watanzania hasa waishio mbali na Dar.
 
Chato international airport kinatosha...hamna haja ya kuharibu rasimali nyingi za nchi namna hii.

Kuna mikoa baadhi ya maeneo hamna hata dispensary.. wamama wajawazito na wagonjwa wengi wanatembea kilometa nyingi kutafuta huduma ya afya. Hela zielekezwe huko ndiko.kunakohitajika zaidi.

Ukiulizwa katika population yote ya mwanza ni percent ngapi ya wananchi wanatumia usafari wa anga sina uhakika kama hata inafika 0.001%..

Sasa kwanin hela isielekezwe penye uhitaji mkubwa
Hayo ni rahisi kuyaongea kwa sababu bila kumung'unya maneno tuna matatizo mengi. Lakini mbona imeanzishwa miradi mingi isiyo muhimu sana kama huu? Je unafahamu kuwa, Mwanza ndiyo inayoongoza nchini kwa kuwa na wasafiri wengi wa ndani kuliko mji wowote hapa Tanzania, ukitoa Dar?
Je hali ya umasikini iko kwetu tu Tanzania kuliko nchi zote duniani?
 
Ahaaaaaa Hata Bukoba inaizidi mwanza
Asante sana, Najua uwanja wa Bukoba umejengwa Hivi karibuni na ndiyo muone ni mji gani umekuwa ukitengwa sana kimaendeleo hapa nchini.
Watu wengi huwa wanaelewa kuwa, jiji la Mwanza kwa kiwango kikubwa sana, maendeleo yake tame toka a na msukumo mkuu wa wakazi wake kulinganisha na miji mingine.
 
Back
Top Bottom