Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,188
Usafiri wa anga ni mojawapo ya kipimo na kigezo kikubwa cha jiji kuwa la kimataifa. Hata hivyo, siyo majiji yote makubwa duniani (yenye wakazi angalao kuanzia 600,000) yana "viwanja vya ndege vya kimataifa" kutokana na kuwa karibu sana na majiji yenye viwanja vya hadhi ya juu.
Mfano: Eneo la Ruhr nchini Ujerumani lina majiji mengi ya Cologne, Düsseldorf, Duisburg, Dortmund na Essen, Bochum, Gelsenkirchen, Wuppertal na Bonn lakini kuna viwanja vya kimataifa vitatu pekee - Düsseldorf; Cologne-Bonn na Dortmund.
Nchini Zambia, jiji la pili kwa ukubwa nchini humo Kitwe, halina uwanja kutokana na kuwa karibu (km 30) na jiji la tatu, Ndola lenye uwanja. Aidha, hata hapa Tanzania, Manispaa ya Morogoro na Mji wa Kibaha haina huduma za usafiri wa ndege kama miji mingine kutokana na kuwa karibu na Dar.
Ukiangalia kwa undani jiografia ya Tanzania, utashangaa kuona kwamba Dar (Mwalimu Nyerere) na Zanzibar (Abeid Karume) pamoja na KIA na hivi karibuni Mbeya (Songwe), vina viwanja vizuri vyenye majengo ya abiria mazuri kuliko uwanja wa Mwanza, unaowakilisha na kituo kikuu cha Kanda ya Ziwa, huku ukiwa kiunganishi kikuu cha Bukoba, Musoma, Shinyanga, Geita, Bariadi, Kahama na Kigoma na hata Tabora.
Hebu hata nyie fikirieni, jiji la Mwanza lenye wakazi wapatao 940,000 (2017) linaunganisha wakazi zaidi ya milioni 16 (kwa sensa ya 2012), ambao ni wengi kuliko nusu ya nchi (nchi zipatazo 30) za barani Afrika. So jiji hili halikufaa kuwa katika hali yake hiyo kwa muda mrefu.
Katika uchunguzi wangu wa muda mrefu:
Ifuatayo ni orodha yote ya viwanja vya ndege vya kimataifa vya majiji yenye wakazi wanaokaribiana na jiji la Mwanza, katika Bara la Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara. (Nimeweka Sub-Sahara Afrika kutokana na kwamba, mabara mengine viwanja vyao ni matawi ya juu, hata kama kamji ni kadogo).

- Hakuna jiji lolote barani Afrika hata lisilo makaa makuu ya nchi na lenye watu wengi kuliko Mwanza, lenye kiwanja kibovu.
- Hakuna jiji lolote barani Afrika hata lisilo makao makuu ya nchi, lenye wakazi wanaolingana na jiji la Mwanza, lenye kiwanja kibovu.
- Hakuna jiji lolote barani Afrika lisilo makao makuu ya nchi lenye wakazi angalao zaidi ya 500,000 lakini lina uwanja mbaya kama wa Mwanza.
Ifuatayo ni orodha yote ya viwanja vya ndege vya kimataifa vya majiji yenye wakazi wanaokaribiana na jiji la Mwanza, katika Bara la Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara. (Nimeweka Sub-Sahara Afrika kutokana na kwamba, mabara mengine viwanja vyao ni matawi ya juu, hata kama kamji ni kadogo).
Attachments
-
IMG_2243.JPG57.1 KB · Views: 354
-
IMG_2244.JPG28.7 KB · Views: 240
-
IMG_2245.JPG16.5 KB · Views: 311
-
IMG_2247.JPG11.8 KB · Views: 224
-
IMG_2248.JPG67.8 KB · Views: 214
-
IMG_2249.PNG88.8 KB · Views: 215
-
IMG_2255.JPG87.7 KB · Views: 214
-
IMG_2257.JPG6.6 KB · Views: 270
-
IMG_2258.JPG30.6 KB · Views: 186
-
IMG_2261.JPG22.3 KB · Views: 272
-
IMG_2264.JPG67.4 KB · Views: 219
-
IMG_2265.JPG52.8 KB · Views: 301
-
IMG_2267.JPG12.7 KB · Views: 339
-
IMG_2272.JPG52.3 KB · Views: 288
-
IMG_2273.PNG41 KB · Views: 197
-
IMG_2276.JPG24.4 KB · Views: 348
-
IMG_2293.JPG58.2 KB · Views: 197