Jiji la Mwanza lachaguliwa na ATCL kama Kitovu cha Ndege za Tanzania zinazokwenda Ulaya

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
May 30, 2017
2,869
3,188
Jiji la Mwanza limeteuliwa na ATCL kuwa Kituo cha mwisho cha safari za ndege kutoka Tanzania kwenda Ulaya.

Sababu ya kuteuliwa kwa Mwanza haijatolewa lakini uchunguzi wangu unaonyesha kuwa Jiji la Mwanza ndilo the northernmost kwa majiji yote nchini hivyo ni rahisi kwa ndege zinazokwenda nje kupitia hapo kutokea JNIA - KIA - mwanza.

ATCL yaongeza safari za Dar- Dodoma


ATCL+pic.jpg

By Habel Chidawali, Mwananchi hchidawali@mwananchi.co.tz
IN SUMMARY

  • ATCL imeongeza safari za ndege katika mkoa wa Dodoma na Mbeya ambapo Dodoma ikiongeza usafiri huo kwa siku za Jumatatu, Jumatano na Ijumaa watakuwa wakienda mara mbili kwa siku.


    Dodoma. Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) limeongeza safari zake kwa mkoa wa Dodoma ambapo sasa itakuwa ni kila siku wakati Jumatatu, Jumatano na Ijumaa itakuwa mara mbili kwa siku.

    Mkurugenzi wa ATLC, Ladislaus Matindi amesema hayo leo Jumatatu Machi 18, 2019 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuwa uamuzi huo unatokana na mahitaji makubwa ya watu kwenda na kutoka Jijini Dodoma.

    Matindi amesema Jiji la Dodoma sasa lina mahitaji mengi ya kiserikali hivyo wananchi kuwa na mahitaji ya kuja na kutoka.

    Kiongozi huyo amesema hadi sasa ATCL imejiimarisha kikamilifu na kuwa na mawakala sehemu mbalimbali duniani na wanaendelea kufanya mawasiliano na mataifa na mashirika mengine ili kujiimarisha.

    "Tumeshazungumza na mashirika na mataifa tofauti duniani ambako sasa tutaanza kurusha ndege zetu huko, lakini kikubwa tutaanza kurusha ndege kutokea Mwanza kwenda Ulaya," amesema.

    Mwenyekiti wa bodi ya ATCL, Emmanuel Korosso ameiomba Serikali kutupia macho katika viwanja vya ndege vya Dodoma na Songwe ili kuruhusu ndege zitue hata nyakati za usiku.
 
Waweke wheelchairs hapo airport
Wagonjwa kila mara wanaambiwa ni mbovu mbovu imekuwa mwimbo.. na mengineyo

Sehemu ya kucheck-in kwa kweli wajiongeze..

Vile vishato vya kupakia abiria havitoshi kabisa.. abiria wanasimama nje ya ndege kama vile wapo kituo cha mwendokasi..

Mengine nayo wajiongeze haswa

Kila la kheri kwao
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom