Jiji la Mwanza halina umeme siku ya tano leo

The Finest

JF-Expert Member
Jul 14, 2010
21,605
6,071
Nimeongea na ndugu jamaa na marafiki zangu wanasema ni hali ya kusikitisha iliyoko katika jiji la Mwanza na siku ya Tano kama sio wiki sasa hawajauona umeme, maisha yanazidi kuwa magumu waliokuwa wakifanya biashara ya samaki wameacha hawajui hatma itakuwa nini hawawezi kumudu kununua mafuta kwani nayo yamepanda bei, wengine wameingia hasara kubwa kutokana na umeme kutokuwepo muda wote huo.
 
C mwanza tu huku moshi mara chache sn lbd kwa wiki mara 2 umeme unawaka sa 7 uciku sa 9alfajiri unakatika, yani maisha yamekua magumu magumu magumu hayaelezeki! Cijui ni kwanini watz ni wapole namna hii. Kilichobakia kwa wa tz ni kufa kwa shida sbb ya upole we2
 
kosa la wakazi wa jiji la mwanza ni kuikataa CCM - sasa wakae gizani ili liwe fundisho kwao.
 
hapa arusha maeneo ya kwa morombo mbauda siku ya tano tangu j 2 walipoukata jioni mpaka leo hakuna ula mjini unawaka sasa sijui wanazani ss hatuna kazi na umeme hofu yangu waizi wataongezrka wito kwa serikali na tanesco wajaribu kubalance kidogo hata huku tupate
 
hali ya mwanza inatisha kila mtu analalamika suala la umeme hivi nini mpango wa tanescoa na ngereja akisaidia na mkuu wake wa kaya???
 
mi ninavyojua, kulikuwa hakuna umeme lakini ile jana mchana waliurudisha!

Mkuu haujarudi.Jana kupitia Star TV habari kwa kina Wananchi walikuwa wanalalamika sana.Jiji limebaki na 4 MW ambazo zinatumika hospitali za Bugando na Sekoutoure tu
 
si waandamane!!!
Mzee wangu,
Hebu Assume Wananchi wenye Jazba wa Mwanza wanaandamana mpaka wanafika mahali kwenda kuchoma moto miundombinu yote ya kusafirisha na kuzalisha Umeme na kuchoma moto ofisi za Tanesco Mwanza, Nini kitatokea baada ya hapo???
 
Tumezoea kuorodhoshewa miradi na Ngeleja kila wakati.Kwa jinsi wabunge walivyokuwa wanagonga meza wakati bajeti ya nishati inapitishwa tungetarajia mgawo ungekoma lakini wapi.Ni mateso matupu chini ya magamba haya.
 
Tumezoea kuorodhoshewa miradi na Ngeleja kila wakati.Kwa jinsi wabunge walivyokuwa wanagonga meza wakati bajeti ya nishati inapitishwa tungetarajia mgawo ungekoma lakini wapi.Ni mateso matupu chini ya magamba haya.
Hasira za kukataa kupitisha bajeti ya kipindi kile, vile vile najaribu kufikiria kama wanaingiza siasa kwenye suala hili especially huko Mwanza watazidi kuumbuka
 
..Kama tunafika mahali ambapo suala la Umeme linafanywa kuwa la Kisiasa zaidi basi tunahitaji maombi.
Ni kawaida ya watawala wauaji hawajali kutoa adhabu hovyo hovyo. hata bei za mazao hushushwa ili kuadhibu waliowakataa.
Biashara: "Ukitaka kufaulu kwenye biashara uwe mwanaCCM" Sumaye mjini moshi 1990s!
 
Acha tupate fundisho,2015 tutajua nini cha kufanya!Ila kwa wakazi wa mwanza poleni sana,ila mnae kamanda wenje japo magamba wanamziba mdomo bado yu nanyi!Wakibana sana ni kuingima mtaani.
 
Back
Top Bottom