HALMASHAURI YA JIJI MBEYA KUWENI NA HURUMA!
Katika hali ya kushangaza, halmashauri ya jiji la Mbeya imepanga kununua gari la kifahari la kutembelea Meya wa jiji la Mbeya ambaye pia inasemekana ni mchungaji eti.
Yote haya yanapangwa wakati watoto wengi wa shule za msingi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza wameshindwa kuanza masomo yao kwa sababu ya ukosefu wa miundo mbinu ikiwemo madarasa na madawati.
Nashauri kiwango cha shilingi milioni mia moja na hamsini kilichopangwa kutumiaka kwa ajili hiyo kielekezwe kujengea madarasa badala ya kununua gari la meya la kifahali ukizingatia kuwa tayari lipo gari lingine analotembelea sasa.
Na ikumbukwe kuwa wanafunzi zaidi wataongezeka mwakani na miundo mbinu ikiwa bado haijaongezwa ni hatari kwa ustawi wa watoto wetu.
Nafahamu halmashauri hii inaongozwa na CHADEMA na naamini CHADEMA ni wasikivu huenda wakaliona hili.
Wenu katika kujenga Mbeya yetu ni mimi mwananchi na mwanachama wa ACT Wazalendo!