Uchaguzi 2020 Jiji la Mbeya, Hata kama mnampenda Mbilinyi (Sugu) msimchague. Ili mpate maendeleo chagueni CCM

Mtu Asiyejulikana

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
1,694
3,981
Mimi naongea haya kwa moyo safi. Nimetoka Mbeya jana. Mara nyingine kabla ya jana nilienda Mbeya mwaka 2018.

Leo hii baada ya ziara ya Mh.Rais Jijini Mbeya na kusuluhisha mambo yake na Wanamkoa huo ndo mambo yameanza kubadilika.angalau sasa barabara zinajengwa na maendeleo mengine.

Jiji la Mbeya lilisuswa toka 2015 na ni kutokana na misimamo yao ha hovyo dhidi ya CCM na Mh.Rais. kitu ambacho kilimkwaza sana Mh.Rais na yeye akaamua kulisusa jiji hilo ili kuwakomoa wananchi wanaojifanya wao wana Dunia yao.

Ushauri wangu:
Ili Jiji la Mbeya liendelee msimchague Joseph Mbilinyi. Mtasababisha matatizo mengine kwa jiji hilo.kwa saza wekeni maendeleo mbele.Sugu mnaweza mpatia kazi nyingine lakini si ubunge.

Kama mnampenda sana hata mumpatie cheo cha kaka wa Mwanjelwa but si ubunge. Chagueni mtu ambaye anakubalika na CCM.Ili sasa matakwa yenu yafike mbele ya Rais kwa urahisi na kufanyiwa kazi.

Mwaka 2020 bado Rais ni John P. Magufuli hilo linaeleweka. Sasa tumieni nafasi hii kwa mambo ya maendeleo.
 
Unaweza kuwa umeongea upuuzi. Ila ukweli ni kuwa 90% naishi mtaani na wapiga kura rahisi sio wapiga kura wa jamiiforum. Ukweli asilimia kubwa wanaikubali CCM
 
Endelea kuwadanganywa wapuuzi wenzio.wenye akili watatambua ninachosema. Wana Mbeya wengi nadhani wanaona mabadiliko yaliyoko sasa baada ya wao kurekebisha uhusiano wao na Mh. Rais. Mimi nmewashauri wajifunze kutokana na makosa.

Wakiendelea na Ujinga wa kujifanya wana misimamo watakuja kunambia.mkoa utasimama kwa miaka mitano mingine. Sasa sidhani kama wapo tayari kwa hilo.

We endelea tu kuchezesha hayo makalio hapo ...ntakupata tu.



Kwa ID yako hiyo na upupu ulioleta tunaanza kujua waliomshambulia Lissu wanatoka upande gani?

Tukuulize swali? Majimbo mangapi na majiji mangapi yanaongozwa na CCM lakini kwa maendeleo hazifikii hiyo Mbeya?
 
Kwahiyo hapo ndipo akili yako ilipoishia?
Si ajabu kusikia nawewe umehitimu na kupewa cheti cha kidato cha 4.
Badala ya kumsema Rais ambaye fedha zote ziko mkononi mwake atende bila ya upendeleo wewe unawaambia wanaMBEYA wawacjague CCM ambao wameiharibu nchi kwa miaka 59 sasa.
 
Mtu Asiyejulikana,
Hizo akili zenu za kuongozwa na rimoti zitawapeleka pabaya! Maendeleo ya kweli yanaletwa na wananchi wenyewe, wale viongozi wa karibu na wanaofanya kazi kwa ushirikiano na wananchi ndo wakuleta maendeleo1

Hizo laana zenu ya kuwabagua viongozi ambao wamechaguliwa na wananchi ndio zinazalisha makapi kama wewe

Huko walikochagua upinzani kodi hamchukui, kwanini maendeleo msipeleke?
 
#wasiojulikana wanataka Jimbo la mbeya city lakini Ngoja nikuulize majimbo ya CCM nimengi kuliko ya vyama vingine Mbona sasa msianzie mliko na wabunge kisha kukawepo mfano ili kama tofauti ipo tusirudie tena kuchagua hivyo vyama visivyoleta maendereo?
 
Lazima tufike mahali tukubali kwamba maendeleo si hisani bali ni haki ya watanzania. Maendeleo yanaletwa na mipango inayotumia kodi za wananchi na si michango ya chama tawala au cha upinzani. Tukifika mahali tukaelewa hili basi hakuna sababu yakuogopa ni nani wananchi wamchague kuwa mwakilishi wao. Kusimamia haki za kikatiba ndiyo uzalendo na si kujipendekeza kwenye vyama.
 
Chuki ya Rais vs Sugu inahusiana vipi na matumizi ya kodi kuleta maendeleo? Rais huwa nachuki na ubaguzi kwa wapinzani (rejea matamshi katika baadhi ya ziara zake). Ni majimbo mangapi chini ya CCM yapo hoi kimaendeleo!
Mnajificha kwenye haya mambo,semeni wazi kuwa 2020 kuna majimbo mnayataka kwa namna yoyote hata KUUA watu ili tu myachukue. Hit list yupo SUGU,BULAYA,MDEE,MBOWE,LEMA,MSIGWA,HECHE...Kwa Lisu mlifanikiwa kwa Risasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaweza kuwa umeongea upuuzi. Ila ukweli ni kuwa 90% naishi mtaani na wapiga kura rahisi sio wapiga kura wa jamiiforum. Ukweli asilimia kubwa wanaikubali CCM

Wananchi wangeikubali ccm tungeona wakijitokeza kujiandikisha kupiga kura. Sasa hivi ukimuuliza mtu kama anaikubali ccm inabidi aseme anaikubali kwa ajili ya usalama wake. Kwani hao wanaikubali ccm kinawashinda nini kuingia huku jf? Huwezi kusema unakubalika kisha silaha yako ikawa ni kuwakomoa watu wasiokukubali kwa kuwanyima maendeleo kama mleta uzi anavyosema.
 
Mtu Asiyejulikana,
Kwani maendeleo ni maamuzi ya rais? Ni hivi, hatuko tayari kumchugua mwanaccm yoyote, sisi tutamchagua huyo huyo Sugu, na ili hasira ya rais itimie vizuri, mshaurini abomoe miundombinu iliyopo ili wana Mbeya atukomoe vizuri. Hatuwezi kumsujudia binadamu yoyote kwa ajili ya maendeleo ambayo ni haki yetu.
 
Kususa kupeleka maendeleo pahala ..ni kukosa Hekima na pia ni ujinga wa Kiwango cha juu kabisa.

Inatuonesha jinsi gani taswira zetu na roho zetu zilivyo ki uhalisia...

Mwafrika halisi ndio pigo zetu hizo.

Watu wasipewe changamoto...
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom