Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Jiji kubwa barani africa, Lagos, Nigeria, limetangaza kuwa litafunga baadhi ya misikiti, na makanisa na vilabu vya usiku ili kupunguza kelele zinazowaadhiri wakaazi milioni 20 wa jiji hilo.
Serikali ya jimbo la Lagos, ilisema hatua hiyo itafanya jiji lililo pwani ya Nigeria kutochafuliwa na kelele kufikia mwaka 2020.
Ni tatizo kubwa katika jiji hili "alisema Adebola Shabi, mkurugenzi mkuu wa shirika la kutunza mazingira la Lagos.
Alisema tafiti zimeonyesha kwamba viwango vya juu vya kelele vinachangia uhalifu, ghasia na kuathiri afya zetu.
Shirika hilo limefunga zaidi ya makanisa 70 na misikiti 20, na vilabu na mikahawa mwaka huu.
Maafisa wakipokea malalamiko zaidi kutoka kwa wakaazi, kuhusu viwango vya kelele kinachatakiwa na iwapo kitazidi, serikali huchukua hatua na kufunga klabu, kanisa au baa ambako kelele hiyo hutoka.
Hata hivyo watu wengi huogopa kulalamika kuna kanisa na msikiti katika barabara ninayoishi zinashindana nani anatoa sauti ya juu "Charlie Chukwu aliambia shirika la habari AP.
Chukwu alisema hakuwasilisha malalamiko yake kwa maafisa wa Serikali,kwavile unachukuliwa kama unapinga Ukristo au Uislamu na unakuwa adui wa wakaazi mtaani.
Chanzo : Mtanzania