Jiji la Dar ndio Jiji muhimu zaidi kwa uchumi wa Tanzania

EllySkyWilly

JF-Expert Member
Aug 28, 2020
2,204
2,083
Jiji la Dar ndio jiji muhimu zaidi kwa uchumi wa Tanzania.

Kwasababu asilimia 99 ya vitu vyote vinavyo tumiwa na watanzania hadi wale wa vijijini vinatokea Dar es Salaam
1. Mafuta ya magari na bodaboda zote
2. Viatu na nguo toka nje ya nchi
3. Mafuta ya kula na taa
4. Vifaa vya ujenzi vyoteee

Naomba wengine mnisaidie kumalizia.

Hivyo basi ndugu zangu Dar ndio kitovu maendeleo ya Tanzania. Mkuu wa mkoa wa Dar akisema aamue kuifunga Dar wiki moja tu hata wale bibi zetu wa vijijini kuna huduma watazikosa.
 
Unataka kusema Nini? Maana bado hueleweki, Kama hujui Dar inatoa Sana kuliko kupokea, yaani Kuna vitu vingi zaidi vinavyotoka mikoani kuja Dar kuliko kutoka Dar kuja mikoani. Ndio maana jiji linakua kwa Kasi.

Ili kupunguza msongamano, Mji Mkongwe wa Bagamoyo uboreshwe na shughuli baadhi ya bandari zifanyikie bandari ya Bagamoyo. Kisha ijengwe relief kuunga na Reli ya Kati SGR na Reli ya Tazara. Pia bandari ya Mtwara na Tanga zipanuliwe ili mikoa ya kusini itumie bandari ya mtwara na mikoa ya kaskazini itumie bandari ya Tanga. Hapo msongamano utapungua zaidi.

Jiji la Dar likifungwa watakaoumia zaidi Ni Wakazi wa Dar na sio wa mikoani.
 
Unataka kusema Nini? Maana bado hueleweki, Kama hujui Dar inatoa Sana kuliko kupokea, yaani Kuna vitu vingi zaidi vinavyotoka mikoani kuja Dar kuliko kutoka Dar kuja mikoani. Ndio maana jiji linakua kwa Kasi...
Hahaa "Unataka kusema nini"?umemuona jamaa kama anazunguka zunguka lkn hanyoosh kiswahili minaona kama anataka azungumzie hizi adha zinazoikumba Dar kipundi cha mvua kama hiki
 
Back
Top Bottom