Jiji la Dar es Salaam na ahadi hewa za madiwani na wabunge wa upinzani

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,225
2,000
Baada ya Uchaguzi Mkuu 2015 kumalizika tulisikia shangwe na vigelele kutoka kambi ya Upinzani baada ya kupata ushindi wa madiwani wengi katika Halmashauri/Jiji ambao waliwezesha kukabidhiwa kisheria kuongoza Halmashauri/Jiji.

Kwa mfano kwa Jiji la Dar Es Salaam tulisikia Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akisema ushindi huo utawawezesha kuwafichua na kuwafikisha katika vyombo vya dola wale wote waliohusika na mchakato wa kuuza hisa za shilika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) na pia ushindi huo utawawezesha kulisafisha Jiji kuanzia kwenye ufisadi, mipango Jiji mpaka uchafu kwenye barabara na mitaani.

Kuna baadhi ya watu walishangilia sana kusikia kauli za madiwani na wabunge wa upinzani kuhusu faida ya kusimamia miji na majiji bila kufahamu Serikali za Mitaa ni zao la Serikali Kuu ambayo katiba ya nchi inasema

Tuliona semina elekezi zikifanywa na Lowassa kwa madiwani wa upinzani wanaotoka katika Halmashauri na Majiji yaliyo chini ya upinzani.

Mwaka mmoja umepita na sina shaka hata waliokuwa wakishangilia ukiwauliza kilichofanywa na madiwani mpaka sasa katika Halmashauri au Majiji yaliyochini ya Upinzani hawawezi kukupa jibu sahihi kwa sababu jibu sahihi halipo.

Kwa sasa zimebaki kelele tu za kisiasa zinazosema, serikali kuu inaingilia maamuzi ya serikali za mitaa lakini ukiuliza kwani sheria inasemaje na nani mwenye jukumu kisheria la kutafsiri hizo sheria, huwezi kupata jibu sahihi kwa sababu jibu sahihi halipo bali kuna majibu tu ya kisiasa.

Mbaya zaidi, Saed Kubenea na wabunge wengine wa vyama vya upinzani katika Majimbo ya Dar es Salaam kwa kupitia Ibara ya 100(1-2) ya Katiba ya Tanzania wamepewa kinga kikatiba ya kutoshitakiwa mahakamani kutokana na jambo lolote walilolisema au kulifanya ndani ya Bunge au walilolipeleka Bungeni kwa njia ya maombi, muswada, hoja au vinginevyo lakini mpaka sasa wapo kimyaaaaa.

Watu wenye akili timamu walifahamu vizuri kilichokuwa kinaongewa ni ahadi hewa kwa sababu kimantiki na kisheria, serikali za mitaa ni zao la Serikali Kuu. Bila mkono wa Serikali Kuu, hata kazi za serikali za mitaa haziwezi kufanyika. Kauli za aina ya kina Kubenea za kusema hatuwezi kushirikia na Serikali Kuu kupitia kwa Wakuu wa Wilaya na Mkoa zilikuwa ni kauli hewa kwa sababu siasa za Tanzania zimejengwa kwenye msingi unaosema, presidential winner-take-all. Wakuu wa wilaya na Mikoa ni wawakilishi wa Rais wa Tanzania.

Wajanja ndani ya upinzani kama Meya wa Jiji la Dar, Isaya Mwita, Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kwiyeko na Mbunge wa Jimbo la Ukonga mh Mwita Waitara wameona umuhimu wa kushirikiana na serikali kuu kupitia Mkuu wa Wilaya na Mkoa.

Moja ya jukumu kuu la Serikali Kuu kisheria kwa Serikali za Mitaa ni kuzijengea uwezo wa kutekeleza majukumu kwa mujibu wa sheria. Uwezo huo ni katika nyanja za fedha, utumishi, usimamizi wa sheria na nidhamu, Kutunga Sera na Sheria, Kutoa miongozo ya viwango vya kutolea huduma na kuhakikisha serikali Kuu inafuatilia na kutathmini kazi za Serikali za Mitaa kama ilivyoainishwa katika Sheria za Serikali za Mitaa Sura 287 na 288 Toleo la 2002 awali Sheria Na 7 na 8 za mwaka 1982.

Hii inaonyesha kwa mujibu wa ibara ya 145 na 146 Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Serikali Kuu ni Mzazi wa Serikali za Mitaa na Serikali za Mitaa zinahitaji malezi kutoka Serikali Kuu. Bila Serikali Kuu hakuna Serikali za Mitaa lakini Serikali Kuu inaweza kuwepo bila Serikali za Mitaa. Hii ina maana kuwa, kazi za madiwani na wabunge haziwezi kufanikiwa bila kupata baraka za wakuu wa wilaya na mkoa lakini kazi za wakuu wa wilaya na mkoa hazihitaji baraka za madiwani au wabunge.

Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam imetoa picha halisi ya matatizo mbali mbali na hasa ya ardhi yaliyopo kwa wakazi wa Dar. Wananchi walikuwa wanajipanga katika mstari kwa makumi kama sio mamia ili kupata nafasi ya kueleza matatizo yao kwa Mkuu wa Mkoa wakati tunaambiwa Jiji liko mikononi mwa vyama vya upinzani.

Haya ni matatizo ambayo mengi yamekuwepo kabla ya Uchaguzi Mkuu ambayo wananchi waliaminisha yatatatuliwa na madiwani au wabunge wa vyama vya upinzani.

Madiwani na wabunge wa upinzani wenye mawazo ya aina ya Kubenea lazima waelewe bila kushirikiana na Serikali Kuu, ahadi hewa hazitaondoka na kwa kudhihirisha ukweli huu, Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Mh Joshua Nassari amewakumbusha wapinzani wenzake akisema, ni ujinga kutoshirikiana na serikali iliyoko madarakani hasa serikali ya Rais Magufuli na akamaliza kwa kusema, Ni muhimu wapinzani wafikirie next generation na sio next election kama wanataka kufanikiwa katika uwanja wa siasa.
 
mbugu91

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
256
1,000
Kushirikiana na serikali hii inakubidi uwe mnafiki,kujipendekeza nak. kwakuwa wapinzani hatuyawez haya itabidi tu ziwe ahadi hewa. Nyie wenye serikali yenu endeleeni na kutimiza ahadi zenu.
 
Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,389
2,000
Pale Bukoba chini ya Lwakatare ni sawa na CCM tu ..hakuna jipya na hakuna tofauti kilichobaki sahivi wanajificha kwenye uvungu, ukimuuliza maswali mawili matatu anakula kona fasta
 
Lituye

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
1,113
2,000
Mimi sijakuelewa mtoa mada kabisa unacho eleza hapa, unalaumu upinzani halafu unasema kumbe tatizo lipo CCM sasa kuna haja gani ya kulaumu upinzani wakati unajua tatizo ni hicho chama cha Majangiri?

Ndio tuamini Zika imeshaleta madhara kwa taifa!
 
Ngushi

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
9,085
2,000
Majimbo yapi ya ccm yanamabadiliko?
Mtatapa tapa sana ila jiji ndio hivo lishachukuliwa!
Majaliwa ndio anaona kuna mabadiliko ndio maana hataki kwenda dodoma kama alivyotuaminisha
 
kimbendengu

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
4,087
2,000
VIJIJI VYOTE VYA WILAYA YA CHEMBA HAVINA BOMBA LA MAJI KUANZIA T.A.N.U MPAKA C.C.M
 
Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
35,869
2,000
Serikali kuu itoe ushirikiano kwa hizo halmashauri ndio mafanikio yataonekana.
Mbona mizengwe mingi?
 
King klax

JF-Expert Member
Jul 10, 2015
2,790
2,000
Hii sirikali inaongozwa na CCM, ni ajabu kulalamika kwamba upinzani utaleta maendeleo
 
WILLIAM MARCONI

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
2,056
2,000
Serikali kuu itoe ushirikiano kwa hizo halmashauri ndio mafanikio yataonekana.
Mbona mizengwe mingi?
Vijiji vyote na vitongoji manispaa ya Moshi vina maji, dhahanati, umeme na lami hadi migombani na shule ni nyingi na zina madawati. Vilijengwa chini ya CCM wakati Serkali inaendeshwa kikabila kutegemea watendaji serkalini, mawaziri na hata waziri mkuu kutoka Kanda hiyo. Kuna asiyejua hili?
 
WILLIAM MARCONI

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
2,056
2,000
Kwani Shinyanga na Dodoma kuna maendeleo gani?
Hakuna. Linganisha na Moshi wao walipendelewa na CCM hiiihii kwa vile watendaji na mawaziri wote nyeti walikuwa wanatoka Kanda hiyo. Sasa Geita nao wanahitaji barabara za lami na hospitali na airport.

Sumaye akiwa Waziri Mkuu bajeti Mbeya Airport ilikatwa ijengwe Arusha Airport pamoja na KIA kuwa hapohapo. Wabunge walisema sana lakini watendaji ni wa Kanda hiyo, AA ikajengwa nani hajui? Asingengangamala Prof. Mwandosya airport ya Mbeya isingejengwa.

Geita na Lindi wasipongangamala barabara za lami na umeme vijijini vitaendelea kwenda Kaskazini hadi milimani.
 
Kitaturu

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
6,070
2,000
Mimi sijakuelewa mtoa mada kabisa unacho eleza hapa, unalaumu upinzani halafu unasema kumbe tatizo lipo CCM sasa kuna haja gani ya kulaumu upinzani wakati unajua tatizo ni hicho chama cha Majangiri?

Ndio tuamini Zika imeshaleta madhara kwa taifa!
Na katika andiko lake kaeleza kwa uwazi kabisa kuwa serikali za mitaa ni zao la serikali kuu

Na hii maana yake ni kuwa, zinaposhindwa serikali za mitaa automatically imeshindwa serikali kuu!!

Huyu mtu anayejiita MsemajiUkweli ni wa ajabu sana na anatuchukulia wasomaji na wachangiaji wa JF ni wajinga wa kiwango chake.

Jamaa anacheza na kuzungusha zungusha sentensi na maneno utadhani anajadili jambo la maana kweli kumbe maskini ametumwa tu na mkuu wake wa kitengo cha propaganda uchwara cha LumumbaCCMbombadia!!
 
mchekanapori

Member
Aug 3, 2012
50
125
Baada ya Uchaguzi Mkuu 2015 kumalizika tulisikia shangwe na vigelele kutoka kambi ya Upinzani baada ya kupata ushindi wa madiwani wengi katika Halmashauri/Jiji ambao waliwezesha kukabidhiwa kisheria kuongoza Halmashauri/Jiji.

Kwa mfano kwa Jiji la Dar Es Salaam tulisikia Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akisema ushindi huo utawawezesha kuwafichua na kuwafikisha katika vyombo vya dola wale wote waliohusika na mchakato wa kuuza hisa za shilika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) na pia ushindi huo utawawezesha kulisafisha Jiji kuanzia kwenye ufisadi, mipango Jiji mpaka uchafu kwenye barabara na mitaani.

Kuna baadhi ya watu walishangilia sana kusikia kauli za madiwani na wabunge wa upinzani kuhusu faida ya kusimamia miji na majiji bila kufahamu Serikali za Mitaa ni zao la Serikali Kuu ambayo katiba ya nchi inasema

Tuliona semina elekezi zikifanywa na Lowassa kwa madiwani wa upinzani wanaotoka katika Halmashauri na Majiji yaliyo chini ya upinzani.

Mwaka mmoja umepita na sina shaka hata waliokuwa wakishangilia ukiwauliza kilichofanywa na madiwani mpaka sasa katika Halmashauri au Majiji yaliyochini ya Upinzani hawawezi kukupa jibu sahihi kwa sababu jibu sahihi halipo.

Kwa sasa zimebaki kelele tu za kisiasa zinazosema, serikali kuu inaingilia maamuzi ya serikali za mitaa lakini ukiuliza kwani sheria inasemaje na nani mwenye jukumu kisheria la kutafsiri hizo sheria, huwezi kupata jibu sahihi kwa sababu jibu sahihi halipo bali kuna majibu tu ya kisiasa.

Mbaya zaidi, Saed Kubenea na wabunge wengine wa vyama vya upinzani katika Majimbo ya Dar es Salaam kwa kupitia Ibara ya 100(1-2) ya Katiba ya Tanzania wamepewa kinga kikatiba ya kutoshitakiwa mahakamani kutokana na jambo lolote walilolisema au kulifanya ndani ya Bunge au walilolipeleka Bungeni kwa njia ya maombi, muswada, hoja au vinginevyo lakini mpaka sasa wapo kimyaaaaa.

Watu wenye akili timamu walifahamu vizuri kilichokuwa kinaongewa ni ahadi hewa kwa sababu kimantiki na kisheria, serikali za mitaa ni zao la Serikali Kuu. Bila mkono wa Serikali Kuu, hata kazi za serikali za mitaa haziwezi kufanyika. Kauli za aina ya kina Kubenea za kusema hatuwezi kushirikia na Serikali Kuu kupitia kwa Wakuu wa Wilaya na Mkoa zilikuwa ni kauli hewa kwa sababu siasa za Tanzania zimejengwa kwenye msingi unaosema, presidential winner-take-all. Wakuu wa wilaya na Mikoa ni wawakilishi wa Rais wa Tanzania.

Wajanja ndani ya upinzani kama Meya wa Jiji la Dar, Isaya Mwita, Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kwiyeko na Mbunge wa Jimbo la Ukonga mh Mwita Waitara wameona umuhimu wa kushirikiana na serikali kuu kupitia Mkuu wa Wilaya na Mkoa.

Moja ya jukumu kuu la Serikali Kuu kisheria kwa Serikali za Mitaa ni kuzijengea uwezo wa kutekeleza majukumu kwa mujibu wa sheria. Uwezo huo ni katika nyanja za fedha, utumishi, usimamizi wa sheria na nidhamu, Kutunga Sera na Sheria, Kutoa miongozo ya viwango vya kutolea huduma na kuhakikisha serikali Kuu inafuatilia na kutathmini kazi za Serikali za Mitaa kama ilivyoainishwa katika Sheria za Serikali za Mitaa Sura 287 na 288 Toleo la 2002 awali Sheria Na 7 na 8 za mwaka 1982.

Hii inaonyesha kwa mujibu wa ibara ya 145 na 146 Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Serikali Kuu ni Mzazi wa Serikali za Mitaa na Serikali za Mitaa zinahitaji malezi kutoka Serikali Kuu. Bila Serikali Kuu hakuna Serikali za Mitaa lakini Serikali Kuu inaweza kuwepo bila Serikali za Mitaa. Hii ina maana kuwa, kazi za madiwani na wabunge haziwezi kufanikiwa bila kupata baraka za wakuu wa wilaya na mkoa lakini kazi za wakuu wa wilaya na mkoa hazihitaji baraka za madiwani au wabunge.

Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam imetoa picha halisi ya matatizo mbali mbali na hasa ya ardhi yaliyopo kwa wakazi wa Dar. Wananchi walikuwa wanajipanga katika mstari kwa makumi kama sio mamia ili kupata nafasi ya kueleza matatizo yao kwa Mkuu wa Mkoa wakati tunaambiwa Jiji liko mikononi mwa vyama vya upinzani.

Haya ni matatizo ambayo mengi yamekuwepo kabla ya Uchaguzi Mkuu ambayo wananchi waliaminisha yatatatuliwa na madiwani au wabunge wa vyama vya upinzani.

Madiwani na wabunge wa upinzani wenye mawazo ya aina ya Kubenea lazima waelewe bila kushirikiana na Serikali Kuu, ahadi hewa hazitaondoka na kwa kudhihirisha ukweli huu, Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Mh Joshua Nassari amewakumbusha wapinzani wenzake akisema, ni ujinga kutoshirikiana na serikali iliyoko madarakani hasa serikali ya Rais Magufuli na akamaliza kwa kusema, Ni muhimu wapinzani wafikirie next generation na sio next election kama wanataka kufanikiwa katika uwanja wa siasa.
Kwanza kabisa umemshambulia sana Kubenea bila shaka amekuchukulia, ipo siku utathibitisha hapa, pili hayo yoote mengine uliyoyasema hapo ni sawa na umejitia mwenyewe kijiti jichoni, alafu unaomba kusaidiwa kukitoa.. umekubali kutumika bila kujali heshima yako itakavyo potea mtaani kwenu huko.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom