vamda
JF-Expert Member
- Aug 1, 2012
- 865
- 535
Habari watanzania wezangu.
Jiji la DSM limewataka wajasiriamali watume maombi ili wapewe nafasi.
Nimesikia waombaji ni wengi kuliko wanaohitajika. Jiji limesema kwamba waombaji waambatanishe barua toka serikali za mitaa.
Kigezo cha barua ya Serikali ya mtaa peke yake hakitoshi kumhalalisha mwombaji aonekane kuwa ni raia wa tanzania maana barua hiyo inaonesha mhusika ni mkazi wa eneo hilo. Haithibitishi uraia wake.
Vitumike vigezo vya mwombaji aambatanishe kitambulisho cha uraia na pia kitambulisho cha ujasiriamali. Vinginevyo jiji mtapata shida ya kuwapitisha waombaji. Au kibongobongo utumike utaratibu wa rushwa au upendeleo usiokuwa na tija.
Jiji DSM, wajasiriamali wanawategemea muwatendee haki. Rudisheni heshima ya jiji kuwa mahali salama kama lilivyokuwa hapo awali. RUSHWA na UPENDELEO wekeni pembeni. Kila la kheri kwenye mchakato wa kuwachagua wajasiriamali watakaoenda kuhudumia stendi mpya ya MBEZI BUS TERMINAL.