Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,278
Jiji la Dar es salaam linapoteza mapato mengi kwasababu ya ubovu wa miundombinu ya barabara. Muda mwingi ambao ungetumiwa kufanya shughuli za uzalishaji unapotea barabarani kwenye foleni.
Wakazi wa Jiji la DSM wanapatwa na msongo wa mawazo asubuhi wanapokwenda kwenye majukumu yao, pia jioni wanaporudi kwenye makazi yao, kwasababu ya foleni inayosababisha wanakaa muda mrefu kwenye makutano ya barabara, hali inayopelekewa na ubovu wa miundombinu.
Hii yote ni kwasababu ya kiburi cha serikali ya CCM, miundombinu hii mibovu ya leo miaka mitatu iliyopita, waziri husika alikuwa ni Magufuli, ambaye uwaziri wake wa ujenzi ndiyo uliowaletea matatizo hata Leo, na tangu amekuwa Rais wa nchi hajaonesha utayari wa kumaliza tatizo hili, na wala hana utashi huo.
Watanzania sasa ni wakati wa kutafakari mustakabali wa nchi, Kwa kuamua kufanya mabadiliko makubwa ya kisiasa, ambayo ndiyo msingi wa maendeleo ya nchi yetu.