Jiji la Arusha na "Traffic-Jams" za Jumatatu mpaka Jumatatu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jiji la Arusha na "Traffic-Jams" za Jumatatu mpaka Jumatatu!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ndegeulaya, May 15, 2011.

 1. ndegeulaya

  ndegeulaya Member

  #1
  May 15, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadau, em tujadili kidogo na hili la Arusha:

  Hivi ? Huu msongamano wa magari (traffic-jams) katikakati ya jiji la Arusha kwa takribani siku zote za juma mfululizo (yaani Jumatatu mpaka Jumatatu), je, tatizo ni magari ndo yameongezeka jijini, ama ni barabara ndo zimekuwa chache ...!

  Kwa mfano, hivi karibuni nilishuhudia kuanza na mpaka kukamilika kwa ukarabati mkubwa wa kufukia mashimo (pot-holes), ama niseme mradi wa kurudiwa kuwekwa upya kwa lami ukiendelea katika barabara kuu ya Arusha-Dodoma, kuanzia eneo maarufu lijulikanalo kama Kona ya Mbauda (ambalo kimsingi ndipo eneo unapoanza kuingilia jijini Arusha kutokea mikoa ya bara), mpaka eneo la Friends-corner (ambalo kimsingi ndipo kiunga cha kuingilia/ama kutokea Stendi kuu ya Mabasi ambayo iko katikati ya jiji la Arusha, lakini bila mafanikio yoyote katika kumaliza/na ama hata kupunguza kidogo basi angalau msongamano wa magari ..

  My take:

  Je, kulikuwa na haja ya kupoteza nguvu na raslimali nyingi kufanya ukarabati kwa existing tarmac road inayoingia katikati ya jiji, ama ingekuwa ni bora x100 kufanyiwa ukarabati (japo kwa kiwango hata cha changarawe tu) na kufunguliwa kwa barabara, say ile iunganishayo kati ya Majengo ya chini na Sakina ili angalau kupunguza msongamano usio wa lazima wa magari yalazimikayo kuingia mpaka katikati ya jiji, ili hatimaye yaje ku'turn-around' kutokea katikati ya jiji na kuelekea Sakina?

  Huu ni mfano mmoja tu, na nna imani iko mifano na alternatives nyingine nyingi tu katika kujaribu kutatua/ na ama angalau kupunguza tu tatizo hili katika jiji letu la Arusha ...

  Nawasilisha mada jamvini, karibuni wadau kwa michango yenu.-
   
Loading...