Jiji la Arusha kumsaka meya wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jiji la Arusha kumsaka meya wake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Shaycas, Nov 8, 2010.

 1. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2010
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Mussa Juma,Arusha
  KAMPENI za kumsaka Meya wa jiji la
  Arusha, zimeanza mjini hapa baada ya
  kumalizika uchaguzi mkuu na
  wagombea wa vyama vitatu vya
  Chadema, CCM na TLP wanatajwa
  kuwania nafasi hiyo.
  Habari za uhakika kutoka ndani ya
  vyama hivyo, zimebainisha kwamba
  upande wa Chadema anayetajwa
  kuwania nafasi hiyo ni Estomii Mallah,
  CCM Poul loter Laizer na TLP anatajwa
  Michael Kivuyo kuwania nafasi hiyo.
  Hata hivyo, uwezekano wa Kivuyo
  kupata nafasi hiyo, unaonekana ni
  mgumu kwani kati ya madiwani wa
  kuchaguliwa 20, TLP kuna diwani
  mmoja tu, huku Chadema ikiwa na
  madiwani tisa pomoja na mbunge na
  CCM madiwani 10.
  Diwani huyo wa TLP hata hivyo kura
  yake moja ni muhimu katika vyama
  vyote hatua ambayo sasa inaweza
  kumfanya awe naibu meya wa jiji hasa
  kutokana na uzoefu wake wa udiwani
  kwa miaka 10 sasa.
  Hata hivyo, Kama TLP wataunga mkono
  Chadema, huenda Malla atakuwa Meya
  wa Jiji la Arusha na na kusababisha
  Halmashauri ya Jiji kuongozwa na
  vyama vya upinzani.
  Akizungumzia hali hiyo, kiongozi
  mmoja wa CCM, alisema mpasuko wa
  viongozi wa CCM wilaya ya Arusha
  ambao unawagusa baadhi ya
  madiwani pia huenda ukasababisha,
  Laizer aliyewahi kuwa Meya kukosa
  nafasi hiyo.
  Hakuna kiongozi wa Chadema au TLP
  ambao walikubali kwa sasa kutoa
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Huu upangaji wa maandishi sifahamu unaitwaje kitaalamu, lakini naogopa unapoteza nafasi kubwa unnecessarily!

  Juu ya suala la Meya wa Arusha, dawa ni kuunganisha nguvu hapo...vINGINEVYO maana hasa ya madiwani itapungua nguvu kama watakuwa chini ya bosi wao wa CCM.
  nI KWELI KAMA VYAMA TUNATOFAUTIANA, LAKINI KAMA WAPINZANI TUNATAKIWA KUWA WAMOJA!

   
 3. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #3
  Nov 8, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Madiwani wa Arusha hilo wameshaliona na kwamba wameshajipanga kuhakikisha kuwa Mh. Malla ndiye meya wao kwa kipindi cha miaka mitano...
   
 4. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #4
  Nov 8, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Ninavyomfahamu Mrema wa TLP, kama kweli CCM wana madiwani 10 basi TLP watamwagiza diwani wake aunge mkono CCM. Lakini mbona tulisikia CHADEMA walipata madiwani 13, hii idadi ya 9 umepata wapi?
   
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  Nov 8, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280

  khee kumbe uchaguzi bado unaendelea..mwee
   
Loading...