Jiji la Arusha kinara Darasa la Nne Taifa ,Dr. Madeni hashikiki

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
HALMASHAURI ya Jiji la Arusha limempongeza Rais John Magufuli kwa uteuzi wa Mkurugenzi Dk.Maulid Madeni anayepigana usiku na mchana kutatua changamoto za shule za Msingi na sekondari za jiji hilo na kusababaisha kung'ara katika matokeo ya darasa la nne na saba kitaifa kwa kipindi cha
miaka mitatu mfululizo.


Pia jiji hilo limempongeza rais Magufuli kwa kutoa elimu bure nchi nzima jambo lililosababisha kuongezeka kwa kufaulu na ari kwa wanafunzi kuendelea kusoma.

Akizungumza jijini hapa na Waandishi wa Habari ofisini kwake, Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Omari Kwesiga, alisema tangu mkurugenzi huyo afike kwenye halmashauri hiyo shule zao za Msingi na Sekondari zinafanya vizuri katika mitihani yao ya ndani na kitaifa


Alisema mwaka juzi 2018 katika matokeo ya darasa la nne na saba. Halmashauri ya jiji hilo ilishika nafasi ya kwanza kitaifa na mwaka huu katika matokeo ya darasa la nne waliofanya mwaka 2019 pia amekuwa wa kwanza.


“Hii hakika tunamshukuru Rais wetu Magufuli kwanza kwa kutoa elimu bure inayowezesha kila motto kupata elimu, lakini kubwa kuliko lote tunamshukuru sana Rais kutuletea Dk.Madeni anayetembelea kila shule kuuliza changamoto inazotukabili na kuzitatua,”alisema na kuongeza:

“Wanafunzi waliofanya mitihani darasa la nne mwaka 2019 katika Jiji letu na kutuletea sifa hii, walikuwa 13,031 kati yao wavulana 6,545 na wasichana 6486,”alisema.


Kwesiga alisema chanzo pia cha mafanikio hayo ni kutokana na mikakati kabambe aliyonayo ya kufuatilia shule zao na kuwapa mitihani mingi ya kuwapima katika Shule za Msingi 48 za serikali na 94 za binafsi.

Amesema jiji hilo lina jumla ya wanafunzi wa shule za msingi 13,013 ambapo shule binafsi inawanafunzi 4,091 na shule za serikali zikiwa na wanafunzi wapatao 8940

Kwa mujibu wa Kwesiga,tangu Januari maka huu ianze tayari ameshatembelea shule zaidi ya 15 kuangalia maendeleo na changamoto zilizopo na kuzitatua na bado wanaendelea kuzifuatilia.

Pia alisema mbali na shule zao za mingi kushika nafasi ya kanza kitaifa matokeo ya darasa la nne, pia Jiji hilo limeingia nafasi kumi kitaifa katika matokeo ya kidato cha pili, huku Shule ya Sekondari ya kuta ya Arusha imeshika nafasi ya nane katika matokeo hayo na hiyo ni kwa miaka miwili mfululizo.

Aliapongeza viongozi wenzake,walimu,wanafunzi kwa kujituma na kufanikisha ufaulu mzuri unaoletea sifa Jiji hilo.
Mwisho.
IMG_20200110_093145.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka jana shule bora na mwanafunzi bora alitoka chato mkapinga na kupiga kelele na kupinga

Mwaka huu imekuwa Arusha na Kilimanjaro naona vigere gere vingi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom