Jiji la Arusha katika kashfa nzito, Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Athuman Kihamia matatani

Mwan mpambanaji

JF-Expert Member
Apr 3, 2008
482
131
MKURUGENZI wa Jiji la Arusha Athuman Kihamia ameingia matatani baada ya kujiidhinishia lita 1900 za mafuta kwa ajili ya matumizi ya gari lake ndani mwezi mmoja kinyume cha kanuni,taratibu na sheria za zinazosimamia serikali za mitaa.

Katika bajeti ya Jiji la Arusha Mkurugenzi wake ametengewa lita 70 kwa wiki ambayo ni sawa na lita 280-300 kwa mwezi.

Nyaraka zilizofikia gazeti hili kutoka ndani ya Jiji la Arusha zinadai kuwa Agusti 30 mwaka huu kupitia Afisa Usafirishaji wake Edward J. Mwaliko aliandika dokezo sabili ya kuomba lita 900 za mafuta kwa ajili ya ofisi ya Mkurugenzi kwa mwezi Septemba.

Katika dokezo hilo Kihamia ametia saini Septemba 1 akisisitiza Afisa Manunuzi wa Jiji kushughulikia na kuidhinisha manunuzi ya lita hizo 900 kwa thamani ya shilingi 1,705,500.

Katika dokezo lingine la siku hiyo hiyo ya August 30 kupitia kwa Afisa Usafirishaji Kihamia aliaomba kuidhinishiwa lita 1000 za mafuta ya Dizeli kwa ajili ya matumizi ya ofisi yake.

Dokezo hilo lenye kichwa habari Maombi ya mafuta ya dharura nje ya GPSA (wakala wa huduma za manunuzi serikalini) anaandika kuwa:Ninaomba idhini ya kununua mafuta ya dharura nje ya GPSA lita 1000 (Diesel) kwa ajili ya matumizi ya ofisi ya Mkurugenzi.

Habari zinadai kuwa mafuta hayo yalinunuliwa kampuni binafsi ambayo ina kituo maarufu cha mafuta kilichopo katikati ya mji wa Arusha.( jina linahifadhiwa kwa sasa)

Hata hivyo juu ya dokezo Afisa Manunuzi wa Jiji alimshauri mkurugenzi huyo kuwa kwa mujibu sheria ya manunuzi ya mwaka 2011(PPA.07, 5.50, kanuni ya 130 (1)na GN:446 inataka kufanya manunuzi yetu kupitia kwa wakala wa serikali wa mafuta (GPSA) kwanza kabla ya kwenda kununua kampuni binafsi na kushauri kuwa wafuate taratibu huo.

Akijibu hoja ya Afisa Manunuzi Kihamia alindika tena juu ya dokezo hilo kwa kusisitiza Afisa Manunuzi kutekeleza manunuzi hayo kwa kuwa ni dharura (emergency).

Akijibu hoja hiyo Afisa Manunuzi alimwagiza msaidizi wake kutafuta bei ya kituo hicho binafsi na serikali ili kufanya uwiano .Fedha za kituo hicho zililipwa katikati ya wiki hii kwa njia ya TISS

Kwa mujibu wa habari kutoka ndani ya Jiji zinasema mafuta hayo ni mengi sana kwa matumizi ya gari la Mkurugenzi kwani hesabu zinaonyesha kuwa kwa gari analotumia linaweza kusafiri umbali zaidi ya kilomita 15,000.

“Hiyo ni sawa na umbali kutoka Captown nchini Afrika ya Kusini hadi Cairo nchini Misri ambayo ni kilomita 12,000 na mafuta yakabaki kwenye gari kwa ziada ya kilomita 3,000”alieleza moja wataalamu wa Jiji.

Kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kuwa tangu Mkurugenzi huyu kuteuliwa kumekuwa na matumizi mabaya kwa kuhudumia ofisi ya mkuu wa wilaya(DC) na ofisis ya mkuu wa mkoa (RC) kwenye mafuta ya ziara za viongozi hao ,hata kuwalipia posho wasaidizi wao na polisi wawapo ziarani ndani ya jiji ambazo hazinauhusiano na shughuli rasmi za Halmashauri,pia kulipia tume zinazoundwa na wateule hao Rais.

Uswahiba wa mkurugenzi huyu na RC ndio umemponza hata kuingia kwenye kashfa nzito ya kuagiza mafuta yasiyoelezeka.Kumbuka Jiji la Arusha haina uhaba wowote wa mafuta na hata kutaka mafuta ya dharura lakini kinyume chake ni kuhudumia ofisi zingine.
Dokezo sabili 1.jpg
Dokezo sabili 2.jpg
 
Na hapo ndio mjue faida ya jiji kuwa chini ya upinzani.....

Wangelikuwa wale magamba wenzangu sizani kama tungezipata hizi.......

Huyu akilala hatoamka.......

Akiamka atolala........

Hivi kuna vidagaa bado wanacheza na huyu mzinza wa magogoni ......

Angalau ingekuwa sangara
 
Huyu ameingia kwa pua sasa ngoja tummenye kwa kina hadi aombe poo. The devil inside you is the devil around you...
 
Bado Tabora anasubiriwa kwa kashfa ya hatari sijui atatobolea wapi...amekanyaga oil chafu sasa hakuna pahali atapumua huyu gamba
 
Ukoo wa panya baba mwizi, mama mwizi ,mtoto mwzi.Ooh ni ile ile..Tumejipanga mwaka huu wataisoma..
 
Kuna harufu ya mchezo mchafu wa kuchafuana unaendelea hapa.time will tell kila Kitu kitajulikana.
 
Na hapo ndio mjue faida ya jiji kuwa chini ya upinzani.....

Wangelikuwa wale magamba wenzangu sizani kama tungezipata hizi.......

Huyu akilala hatoamka.......

Akiamka atolala........

Hivi kuna vidagaa bado wanacheza na huyu mzinza wa magogoni ......

Angalau ingekuwa sangara
wanaviziana tu,ile kufuta posho ya laki tatu ya nauli imewauma sana waheshimiwa madiwani
 
Na hapo ndio mjue faida ya jiji kuwa chini ya upinzani.....

Wangelikuwa wale magamba wenzangu sizani kama tungezipata hizi.......

Huyu akilala hatoamka.......

Akiamka atolala........

Hivi kuna vidagaa bado wanacheza na huyu mzinza wa magogoni ......

Angalau ingekuwa sangara
Afadhali wewe umeelewa kuwa ni mzinza (mhaya Muhamiaji) maana Kuna watu wanamwita ng********ha
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom